Mgomo wa daladala jijini Mwanza

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
573
140
Kuna habari zimezagaa hapa jijini Mwanza kuwa kulikuwa na mgomo ambao ulitakiwa kuanza mida ya saa mbili asubuhi, kuna waliokubali kuanza mgomo ila kuna wengine ambao walikaidi. picha hii inaonesha gereva wa daladala aliyekaidi kugoma akishambuliwa na wenzio waliogoma! Kwa bahati nzuri aliokolewa na askari polisi!
 
Attachments

  • DSC02850.JPG
    DSC02850.JPG
    44.9 KB · Views: 86
Mabasi ya abiria maarufu hapa kama Express yapo katika mgomo kuanzia leo asubuhi. Nimepita barabara ya airport hadi mjini kati, hali sio nzuri watu wanaosubiri usafiri ni wengi sana huku huduma ikitolewa na mabasi machache ,pikipiki, pickups na wengine tukijifanya tunafanya mazoezi.

Watu niliozungumza nao wanasema madai ya wenye mabasi ni kupinga vitendo vya unyanyasaji vinavyofanwa na polisi wa usalama barabarani...kuna makonda wengi wamo mahabusi hivyo mgomo huu ni shinikizo la kutaka wenzao waachiwe bila masharti. Hata hivyo habari nyingine zinasema ni mgomo wa kudai ongezeko la nauli.

Subiri update!
 
Jana walikuwa wanasambaziana vikaratasi, wajanja tukajua litakalotokea, na tukawa proactive!
 
mgomo huu nimetarifiwa na dogo langu, anatokea kona ya bwiru kuelekea nyakato. wameamu kuhesabu hatua. madai yao ni nauli kupanda, wanasema kwa tsh. 300/= inakula kwao
 
Dah sasa watapandisha mpka lini? Me nilisikia kuwa wanagoma kwa sababu ya kusumbuliwa na matraffick!
 
Kama ni kulalamiki vitendo wanavyofanyiwa na askari wa barabarani ni sawa kabisa kwani hata leo eneo la mzunguko wa Impala -ARUSHA nimemkuta askari wa usalama barabarani akimchapa Dereva wa Hice makofi sasa sijui ndio wanasimamia usalama gani?
 
Hatimaye dala dala zote za jijini Mwanza zimegoma kubeba abiria kwa sababu kuwa wanaonewa sana na matrafiki!
Habari ndo hiyo.
Nawasilisha.....
 
mtu aliye huko anadai wanataka nauli zipande lakini sishangai mwanza ni jiji la revolution kama ilivyo arusha mbeya na kilimanjaro.
 
Hatimaye dala dala zote za jijini Mwanza zimegoma kubeba abiria kwa sababu kuwa wanaonewa sana na matrafiki!
Habari ndo hiyo.
Nawasilisha.....
Mkuu, ina maana huko Mwanza leo ni WALK TO WORK? Na huo mgomo umeanza saa ngapi? Na utadumu kwa muda gani?
 
mtu aliye huko anadai wanataka nauli zipande lakini sishangai mwanza ni jiji la revolution kama ilivyo arusha mbeya na kilimanjaro.
Kwani mazungumzo na mamlaka husika zinazoregulate hilo soko la daladala huko yameshindikana?
 
Nimetoka K'hewa kwa mguu mpaka town,Wengine wanadai wamepandishiwa ushuru na sumatra. Mwenye habari za uhakika atupashe.
 
mtu aliye huko anadai wanataka nauli zipande lakini sishangai mwanza ni jiji la revolution kama ilivyo arusha mbeya na kilimanjaro.
 
Wamegoma kwa sababu ya
1. Manyanyaso ya matrafiki
2. Kupandishiwa kodi na malipo mbalimbali na SUMATRA pamoja na TRA.
Wanahoji kuwa kwa nini serikali ya Tanzania inashindwa kukusanya kodi na mapato mbalimbali kutoka kwa wawekezaji kutoka nchi za nje kwenye makampuni kama Migodini, makampuni ya simu nk? Mafisadi wanapeta lkn watanzania maskini wanaohangaika ndo wanazidi kubanwa kulipishwa malipo ya mateso na manyanyaso. Wanasema sasa basi, serikali na wao na wao na serikali.
 
hili liwe somo kwa wakazi wa kirumba waone jinsi CCM inavyo nyanyasa raia wake kwa utawala wa kibabe
 
mgomo ni njia ya mwisho......je wameshapitia njia zingine?

ccm inasubiri wajicheleweshe kwa kusubiri hizo hatua zingine zichukuliwe kama unavyotutaka tuamini, wametimiza wajibu gani kwa kuwalealea watumishi kwenye serikali waliyoiunda hadi tunapata adha ya usafiri namna hii!!!?
 
Wamegoma kwa sababu ya
1. Manyanyaso ya matrafiki
2. Kupandishiwa kodi na malipo mbalimbali na SUMATRA pamoja na TRA.
Wanahoji kuwa kwa nini serikali ya Tanzania inashindwa kukusanya kodi na mapato mbalimbali kutoka kwa wawekezaji kutoka nchi za nje kwenye makampuni kama Migodini, makampuni ya simu nk? Mafisadi wanapeta lkn watanzania maskini wanaohangaika ndo wanazidi kubanwa kulipishwa malipo ya mateso na manyanyaso. Wanasema sasa basi, serikali na wao na wao na serikali.
Wana point. Huu utaratibuw a serikali kuwa anayelipa kodi ndiye akamuliwe zaidi, utatufikisha pabaya
 
Tangu asubuhi hakuna huduma ya dala dala kwa jiji la Mwanza nasikia madereva wamegoma!! mwenye taarifa zaidi naomba atujuze!!

PIck ups na pikipiki ndio zinaokoa jahazi la usafiri kwa jiji la Mwanza.

9kAQyQbjg==

hicho ki-suzuki pick up kimezidiwa lakini watu ndio wamebanana namna hiyo.....ilikuwa maeneo ya Mabatini asubuhi ya leo

9k=

sio mashindano ya pikipiki ndio hali ilivyo kwa leo maeneo mengi kwa jiji la Mwanza!!!
 
Back
Top Bottom