Poleni sana wanafunzi wa UDSM. Huo ni mwanzo tu wa utungu.Kinachowaponza ni mfumo mpya wa ajira katika sekta za kimataifa.Unapata ajira kwa kufuata chuo chako kipo rank gani duniani.Watoto wa wakubwa na baadhi ya matajiri waliopeleka watoto wao vyuo vya nje ambavyo kwa bahati mbaya vimepitwa na UDSM KATIKA RANKING,wamechukia sana,maana kila waendapo kwenye interviews za mashirika ya kimataifa,wanabwagwa maana vyuo walivyosoma vimepitwa na UDSM.
Walijaribu sana kukihujumu wakati ule kilipokuwa cha 13 barani Afrika,walikinyima pesa za utafiti,wakapunguza pesa za matumizi na walijaribu bila mafanikio kuwachafua wanaomaliza UDSM.Japokuwa chuo kiliporomoka mpaka kuwa cha 25,lakini kikajipanga upya mpaka kimekuwa cha nne Afrika jambo ambalo limewaudhi sana wakubwa.Hongereni sana wanajumuia wa UDSM kwa kuiletea sifa TZ.
Kazi kubwa ya mwanafunzi wa chuo kikuu chochote kile duniani,ni kusoma tena kusoma hasa,unapomnyima umeme mwanafunzi wa chuo kikuu.unamuathiri vibaya mno,kama kuna eneo ambalo halitakiwi kupata mgawo wa umeme ni chuo kikuu,ndio maana vyuo vikuu mikoani havipati mgao wa umeme, nenda Dodoma,Mwanza,Mbeya,Iringa,Arusha hata Moshi,maeneo ya vyuo vikuu hayakatiwi umeme hovyo.
Enzi za mwalimu,UDSM ilipewa umeme daima,hata wakati tunasoma sisi UDSM mwanzoni mwa miaka ya tisini,tulikuwa hatukatiwi umeme,hata mgawo uwe mkubwa kiasi gani,sisi tulipewa umeme maana watawala walijua kazi yetu ni kusoma.Kinachowaponza nyie wanafunzi mnaosoma sasa UDSM,ni ubinafsi wa baadhi ya viongozi Waliowapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kama Kenya,Uganda,India,China hata Ukraine wakidhani watoto wao watapata elimu bora kumbe wamepotea maboya,wameruka majivu yaliyopoa wamekanyaga moto.
Kwa jinsi viongozi wetu walivyo wabinafsi,sitashangaa nikisikia chuo chenu kikifanyiwa vitinbi vingi zaidi,badala ya kukiboresha chuo hicho ili kiwe cha kwanza,viongozi wetu watakipiga vita.Na kwa watanzania wachache wapumbavu nao watawaunga mkono,wasameheni maana hawajui walitendalo.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki UDSM.Jipeni moyo wanajumuia wa UDSM,hapaTanzania kwa viongozi tulionao mtapata dhiki,lakini mkiwa na umoja na kunia mamoja hakika mtayashinda mateso yote yaliyo mbele yenu.Amini nawaambieni,bado kitambo kidogo mateso yenu yote yatakwisha,tuombe Mungu atuvushe salama mwaka 2015 ili mpate kupumzika toka kwenye dhiki kuu mnayopitia,Amina.