Mfwatiliaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,322
- 70
nasikia mkuu wa chuo amekubaliana na matakwa ya wanafunzi kuwa watasogeza mitihani mbele ili waweze kumalizia kutoa vitambulicho vya mitihani kwa nafasi na mambo mengine je ni kweli management imesalimu amri!!!!!!!!!
Tafadhali elewa hoja kuu yahuo mgomo,mmh! huwa nina wasiwasi na migomo inayoanzishwa wakati wa mitihani.Examination fever hiyo jamani!wakiambiwa waende tu kwenye mitihani na vitambulisho vya shule tu badala ya vitambulisho vya mitihani bila kujali kama umemaliza ada au la watakubali?TAFAKARI
Nyantella nafurahi kuwa unafikiria vyema. Nasema hivyo kwa kuwa ili ufikiri kisomi hasa kiinterlectual lazima uangalie pande mbili za shilingi. Umeangalia wanafunzi na pia utawala. Kuna mtu kasema leo ndiyo siku ya mwisho ya kulipa ada na hajalipa au atalipa leo wakati huo huo anasema angepaswa apewe ID kabla hajalipa sidhani kama hiyo ipo duniani. Pili mtu alikua anajua kuwa ana mtihani asijiandae tu kwa kuwa hajapewa ID, ndicho kinampa stress? Jamani wanafunzi wenzangu tujiangalie msiwe kama wale wenzangu wa injinia UDSM wanalazmisha mwezao arudi chuoni ilihali mwenzao kakosea kujitetea toka mwanzo.
Kwa upande wa utawala nadhani lazima kuna tatizo la kupashana habari (information management) wanafunzi hasa wale ambao wanaona elimu ya chuo ni ya kubabaisha tu hivyo kula goodtime huwa wanatafuta loophole hivyo kama taarifa hazitembei itakua ndio kigezo cha kuanzia na kuwa provoke wengine. Wanafunzi wanahitaji kutaarifiwa au kukumbushwa kuhusu kulipa ada kwa wakati kila mara. Alafu kama mwanafunzi ameshalipa apatiwe ID ili awashawishi wengine walipe.
Kuhusu vyombo vya habari. Ninachoamini hakuna kitu kibaya kama kugombana na waandishi wa habari hata kama ni mmoja hasa wanafunzi maana hujui ukitoka chuoni utaenda wapi unatakutana na nani. Na hasa kwa mambo ya sasa ambapo kila kitu kinafanywa siasa hata pale panapohitaji sayansi asilia na ndiyo maana mwenzangu ameuliza kama tunaweza kupambana kuhusu maslahi ya umma au kugombania elimu kama ilivyo kwa maslahi binafsi? Nakumbuka nikiwa secondari umeme ukikatika tulikua tunashangilia lakini nlipotua chuo ilikua umeme unapokatika watu ni vilio lakini is quit diferent this time ingawa siyo kwa wote ila utkuta mwanafunzi wa chuo anafurahi umeme ukikatika anafurahi na kusema afadhali tukose wote, watu hawamsikilizi mwalimu na kutake notes wanasubiri wezao waandike wao watoe copy na kusoma kama mwezake aliyoelewa na kuandika, mtu yuko chuo kikuu lakini yeye ananoye book 2 tu kwa masomo yote na madesa kibao na photocopy ya madaftari ya wenzie mwalimu akifundisha yeye anasikiliza mziki through earphones akisema kibonde tunaanza kulalama, tunakuwa kama serikali bana kupenda kusemwa vizuri tu ikisemwa vibaya inakasirika? Kwani alichosema Kibonde kuhusu wanafunzi wa vyuo vikuu vimeanza kusemwa leo kwani uongo? Magazeti ya udaku yamekua yakieleza yaleyele lakini hawakushambuliwa lakini kwasababu tu aliyasema wakati muafaka ndio tunaanza kulalama.
mmh! huwa nina wasiwasi na migomo inayoanzishwa wakati wa mitihani.Examination fever hiyo jamani!wakiambiwa waende tu kwenye mitihani na vitambulisho vya shule tu badala ya vitambulisho vya mitihani bila kujali kama umemaliza ada au la watakubali?TAFAKARI
Mkubwa ukisoma hii thread utaona nimesema ID zimeanza kugaiwa ghafla last week yaani ni kama kamtego kwakuwa walijua wote tunataka tufanye examz na hivyo walijua tutaangaika tu mpaka tuipate hiyo hela fine, tatizo likawa hiyo process yao ya kuishue ID kama ukilipa ni kero, nenda huku rudi huku, peleka asubuhi njoo jioni, system iko down, mara sijui nenda ofisi ile lakini imefungwa, huku wanamsaidia huyu wewe hapana, kero tupu yaani mimi binafsi nimetumia siku 4 kuanzia alhamisi ID nikafanikiwa kupewa jumapili na wakati jtatu asubui nna mtihani. Na wakati huo huo lugha zao zilikuwa chafu na za dharau sana. Unanimbia nijiandae tu, siwezi coz last tym kwenye test 2 walinizui kufanya test kwa kuwa sikuwa nimeshughulikia ID yangu mapema nikakosa test, leo ntawezaje kusoma na ID sijapata?
Kingine prospectus inaniambia leo ndio siku ya mwisho ya kulipa ada sasa kwanini uninyime kufanya mtihani wakati muda wa kulipa ada bado ninao? Siwezi kuogopa jeshi, waandishi wa habari wala raisi kama wanakosea nitawaambia kosa lao bila kujali uwezo wao, haiwezekani waripoti kitu ambacho sio kweli haukugomea mitihani wala hatugomei mitihani leo.
Mimi najua matatizo ya chuo changu na ninajua kuwa madai yangu ni ya msingi na muhimu ili niweze kusoma vizuri na kumaliza chuo salama coz najua nilichokifuata hivyo basi naomba usinifananishe wala kunihusisha na migomo ya vyuo vingine bali judge me according to the problem at hand an nt otherwise.
Mapambio ya kuhamasishana yanaendelea, moja ya dai la msingi ni kusogeza mtihani huu mbele kwa zaidi ya wiki moja ili management iweze kuandaa ID's zetu na sisi tupate muda wa kujiandaa kwa examz bila stress, hizi ni final examz hawawezi wakazi treat kama test za vidudu.
Mgomo umeingia siku ya pili.