Mgomo Chuo Kikuu Mkwawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo Chuo Kikuu Mkwawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 17, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  JINAMIZI la migomo vyuoni linaendelea, safari hii ni zamu ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu cha Mkwawa (MUCE) mkoani Iringa ambao wanafunzi wake waliamua kugoma wakidai kucheleweshewa fedha za mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

  Katika chuo hicho wanafunzi zaidi ya 200 wa mwaka wa kwanza walianza mgomo juzi usiku hali iliyowalazimu askari polisi kutumia risasi zilizokuwa zikirushwa hewani kuwatawanya.

  Usiku wa kuamkia jana, baadhi ya wanafunzi waliingia kwenye mabweni ya wenzao ili kuhamasisha mgomo huo ambapo walitoka nje wakielekea lilipo tawi la Benki ya CRDB hali iliyowatisha askari wanaolinda benki hiyo na kuwalazimu kutumia silaha.

  Hivi karibuni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kilikuwa kwenye mgomo kwa madai mbalimbali ukiwahusisha wahadhiri na wanachuo ambao kwa pamoja hawakuingia madarasani kwa zaidi ya siku tano wakisisitiza kusikilizwa kwa madai yao.

  Hadi kufikia jana hali iliendelea kuwa ni ya mashaka UDOM baada ya kundi la wanafunzi kujipanga kuwatimua viongozi wao wakidai walikuwa wameshindwa kuwawakilisha ipasavyo katika mkutano wao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Wakati hali ikiwa bado tete UDOM jana nje kidogo ya mji wa Iringa wanafunzi wa Mkwawa walikuwa wakitafakari kuanza mgomo wa kuwashinikiza viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) wajiuzulu kwa kuwacheleweshea mikopo yao kutoka bodi kwa ajili ya chakula na malazi.

  Katika mgomo huo, baadhi ya wanafunzi na mwandishi wa habari wa gazeti hili mkoani Iringa Francis Godwin walitiwa mikononi mwa polisi kwa muda na kushikiliwa wakidaiwa kuhamasisha vurugu huku mwandishi huyo akituhumiwa kuingia chuoni hapo kinyume cha taratibu.

  Baada ya kuachiwa, mwandishi huyo alipata muda wa kuzungumza na wanafunzi hao wanaoeleza sababu ya mgomo wao ni kuchelewa kupata fedha za mikopo ambazo ni sh 300,000 kwa kila mmoja zilizotakiwa kuwafikia Januari 14, mwaka huu.

  Pamoja na mgomo huo ambao wao wanafunzi walidai utamalizika pale tu bodi ya mikopo itakapotimiza wajibu wake bado wanafunzi hao walieleza kulilalamikia jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa askari wake kurusha risasi za moto juzi usiku wakati wa kuwatawanya.

  Wanafunzi hao wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya chuo hicho jana walisema kuwa kutokana na kukosa fedha hizo tokea Januari 14 wamekuwa wakiishi kwa shida wakikosa fedha ya kununulia chakula na mahitaji yao mengine.

  Mbali ya hilo wanafunzi hao walilalamikia kulipwa kiasi kidogo cha sh 5,000 wanachopewa kila siku wakisema kwamba kilikuwa hakikidhi mahitaji yao kwani kimepitwa na wakati na kinatakiwa kurekebishwa mara moja na serikali.

  Waliyataja madai mengine dhidi ya uongozi wa chuo na serikali kwamba ni kucheleweshewa vitambulisho vya bima ya afya ambavyo kila mwanafunzi hulipia sh 50,000, kitabu cha muongozo wa masomo na mgao wa umeme.

  Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Chuo hicho cha Mkwawa, Profesa Philemon Mushi, alikanusha taarifa za kutokea kwa vurugu zozote chuoni hapo na akasema kulikuwa hakuna tukio la polisi kutumia risasi.

  Profesa Mushi hata hivyo alisema sokomoko hilo la wanafunzi lilisababisha kukamatwa na kushikiliwa kwa muda kwa wanafunzi wanne ambao hata hivyo waliachiwa huru baadaye.

  Alisema tayari uongozi wa chuo umefanya mawasiliano na Bodi ya Mikopo, ambayo imethibitisha kwamba fedha za wanafunzi hao zilianza kuwekwa kwenye akaunti zao tangu Ijumaa.

  Alisema walikuwa na uhakika kwamba hadi kufikia leo taratibu za kibenki zitakuwa zimekamilika na wanafunzi hao watakuwa wamepata fedha zao.

  Kuhusu kitabu cha muongozo wa masomo na umeme, Profesa Mushi alisema kinaandaliwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kitakapokuwa tayari kitagawanywa kwa wanafunzi hao.

  Kuhusu tatizo la umeme chuoni hapo alisema kuwa limekuwa likisababishwa na mgao wa umeme ambao unaendeshwa nchi nzima na kuwa pale mgao wa umeme utakapokuwepo eneo hilo umeme wa jenereta umekuwa ukitumika kusambaza umeme katika vyumba vyote vya kusomea, bwalo la chakula na maktaba ili kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri.

  Kuhusu mwandishi aliyekamatwa na kuzuiwa kuendelea kutimiza wajibu wake wa kuchukua habari kwa wanafunzi hao mkuu huyo alimwomba radhi mwandishi huyo na waandishi wengine kwa kunyanyaswa na watu wa usalama chuoni hapo na kuwa wanahabari wana wajibu wa kuwasikiliza wanafunzi hao kama sehemu ya kazi yao .

  Mwandishi huyu aliwekwa kizuizini katika ofisi za usalama chuoni hapo kwa zaidi ya dakika 15 akihojiwa na kutakiwa kueleza mamlaka ya kufika chuoni hapo ameyapata wapi bila wao kumruhusu kuongea na wanafunzi hao.

  Kutokana na tukio hilo waandishi wa habari mkoa wa Iringa kupitia klabu yao ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) wameeleza kusikitishwa na uamuzi wa wana usalama hao wa chuo kumzuia mwandishi na kumhoji kwa kuwasikiliza wanafunzi hao na kuwa kufanya hivyo ni kuzuia uhuru wa vyombo vya habari kutoa habari na uhuru wa wananchi kupata habari za uhakika zaidi.

  Katibu wa IPC Frannk Leonard alisema kuwa pamoja na uongozi wa chuo kuomba radhi kwa kitendo hicho bado jamii inapaswa kutambua kuwa vyombo vya habari vina wajibu wa kuhabarisha na kwenda moja kwa moja katika maeneo ya matukio na kupata habari kamili kwa kuzungumza na pande zote badala ya kukaa ofisini kupata habari za upande mmoja.

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo wa wanafunzi chuo cha Mkwawa japo amekanusha madai ya wanafunzi juu ya polisi kutumia risasi za moto kuwatawanya na kuwa hakuna askari polisi aliyekwenda katika mgomo huo Mkwawa na kuwa Jeshi la Polisi si walinzi wa chuo hicho .


  Mgomo wanukia Chuo Kikuu Mkwawa
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Ishaletwa hii mkuu, Mods unganisheni hhi kitu!
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ok sikuiona basi mod waiunganishe tu
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hakuna neno mkuu mimi nilikuwa sijaiona thanks for the information anyway.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  careful next time
   
Loading...