GE2025 Mgombea Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi (CCM) apiga kura. Asema hakuna viashiria vya uvunjifu wa amani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,559
Reaction score
3,953
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi tayari amepiga kura katika kituo cha kupigia kura Kariakoo viwanja vya michezo ya watoto Jimbo la Kwahani.

Dk Mwinyi amefika katika kituo hicho saa 2:10 asubuhi ya leo Jumatano, Oktoba 29, 2025 akiwa ameongozana na familia yake, mke wake, Mariam na watoto wake watatu.

G4aPw0CWoAAmtNP.jpg
G4aPu2YW4AAFq7L.jpg

G4aPw33W4AA8cyu.jpg

Baada ya kufika katika kituo hicho, alipanga foleni katika mistari ya wananchi ambao nao walikuwa kwenye foleni kwa ajili ya kupiga kura.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Dk Mwinyi anayetetea nafasi hiyo amesema ametimiza haki yake ya kikatiba na kwamba amefurahishwa kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Nimetekeleza wajibu wangu kikatiba, nimeshapiga kura, tumeridhika na maandalizi yaliyofanywa na Tume kwakweli ni mazuri,” amesema Dk Mwinyi.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi ambao bado wapo nyumbani wajitokeze kupiga kura ili kuwachagua viongozi watakaowatumikia kwa kipindi cha miaka mitano.

Pia, Dk Mwinyi amepongeza amani ambayo imetawala kuanzia wakati wa kampeni mpaka asubuhi hii saa mbili kwani hakuna viashiria vyovyoye ambavyo vinetokea kuashiria uvunjifu wa amani.

"Tumefanya kampeni kwa amani kabisa hatukuona chokochoko, mpaka sasa tunaona amani ipo ni imani yetu hali itaendelea hivi hata baada ya kutangazwa matokeo," amesema Dk Mwinyi.

Ametumia fursa hiyo kuwapongeza wapinzani wake 11 anaoshindana nao kujitokeza kuwania nafasi hiyo akisema jambo hilo linaonesha kukuwa kwa demokrasia katika visiwa hivyo.

Hata hivyo, amesema kulingana na kampeni walizofanya wanaamini wanachi wamewakubali na watashinda katika uchaguzi huu.

Naye Mke wake, Mariam amesema:"Siku ya leo tulikuwa tunaisubiria sana tukisema Oktoba 29, imefika kwa hiyo wananchi tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Shime shime tujitokeze kwa wingi kupiga kura," amesema.
 
Heshima yenu Wazalendo wote, naomba kujua umetimiza haki yako ya kupiga kura leo?
Mimi mapema kabisa nimetiki!
 
Attachments

  • ccmtanzania_e33248ab1b9a4022b2e4b674f4ba20ba.jpg
    ccmtanzania_e33248ab1b9a4022b2e4b674f4ba20ba.jpg
    60.9 KB · Views: 9
  • ccmtanzania_1b51c8c5806a45c79205bb119ff4aa6e.jpg
    ccmtanzania_1b51c8c5806a45c79205bb119ff4aa6e.jpg
    59 KB · Views: 11
  • ccmtanzania_0f84905ed49a41b19efc3886c6baf5ce.jpg
    ccmtanzania_0f84905ed49a41b19efc3886c6baf5ce.jpg
    125.4 KB · Views: 11
Nimepiga kura Kata ya Kati Arusha.
 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi tayari amepiga kura katika kituo cha kupigia kura Kariakoo viwanja vya michezo ya watoto Jimbo la Kwahani.

Dk Mwinyi amefika katika kituo hicho saa 2:10 asubuhi ya leo Jumatano, Oktoba 29, 2025 akiwa ameongozana na familia yake, mke wake, Mariam na watoto wake watatu.

Baada ya kufika katika kituo hicho, alipanga foleni katika mistari ya wananchi ambao nao walikuwa kwenye foleni kwa ajili ya kupiga kura.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Dk Mwinyi anayetetea nafasi hiyo amesema ametimiza haki yake ya kikatiba na kwamba amefurahishwa kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Nimetekeleza wajibu wangu kikatiba, nimeshapiga kura, tumeridhika na maandalizi yaliyofanywa na Tume kwakweli ni mazuri,” amesema Dk Mwinyi.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi ambao bado wapo nyumbani wajitokeze kupiga kura ili kuwachagua viongozi watakaowatumikia kwa kipindi cha miaka mitano.

Pia, Dk Mwinyi amepongeza amani ambayo imetawala kuanzia wakati wa kampeni mpaka asubuhi hii saa mbili kwani hakuna viashiria vyovyoye ambavyo vinetokea kuashiria uvunjifu wa amani.

"Tumefanya kampeni kwa amani kabisa hatukuona chokochoko, mpaka sasa tunaona amani ipo ni imani yetu hali itaendelea hivi hata baada ya kutangazwa matokeo," amesema Dk Mwinyi.

Ametumia fursa hiyo kuwapongeza wapinzani wake 11 anaoshindana nao kujitokeza kuwania nafasi hiyo akisema jambo hilo linaonesha kukuwa kwa demokrasia katika visiwa hivyo.

Hata hivyo, amesema kulingana na kampeni walizofanya wanaamini wanachi wamewakubali na watashinda katika uchaguzi huu.

Naye Mke wake, Mariam amesema:"Siku ya leo tulikuwa tunaisubiria sana tukisema Oktoba 29, imefika kwa hiyo wananchi tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Shime shime tujitokeze kwa wingi kupiga kura," amesema.
Mzalendo mimi nimetumia haki yangu ya kikatiba ya kutopiga kura!! Ahsnt
 
Back
Top Bottom