Uchaguzi 2020 Mgombea urais wa JMT kupitia CCM, kufanya mkutano wa kampeni Tunduma leo huku kukiwa na mpasuko mkubwa kwa majimbo ya Momba na Tunduma

dikteta2020

JF-Expert Member
Aug 14, 2018
595
3,990
Mgombea urais wa JMT ndugu John Magufuli muda mfupi ujao anatarajia kufanya mkutano wa kampeni hapa Tunduma. Pamoja na mambo mengine yanatatajiwa kutoka maneno makali yasiyo ya kawaida kabisa kutoka kwa mgombea huyo kufuatia mgogoro mkubwa uliopo baina ya wanaccm hapa Tunduma.

Mgogoro huo unapeleka wagombea ubunge wa majimbo ya Tunduma na Momba kukosa uungwaji mkono ndani ya chama hicho na hivyo kuonyesha dalili za waziwazi za CCM kushindwa uchaguzi mkuu ujao ndani ya wilaya hii.

Stay tuned
20201001_103249.jpg

Picha: Baadhi ya wanachama wa CCM wakielekea kwenye mkutano wa kampeni za urais wilayani Tunduma
 
Sacretariaty ya chama inafanya vikao vya ndani ili kuweka mambo sawa.
Chama kikubwa kama CCM lazime kipitie changamoto kama hizi.
 
Hawawezagi kwenda menyewe kwenye mikutano mpaka yapakiwe kwenye malori kama mizigo? Kuna ulazima gani kusomba watu na malori toka vijijini? Walioko eneo la mkutano hawatoshi? Ndo kwenda kujaza vichwa? Asante Mama yetu ulifumbua macho kule Musoma
 
1.Unapewa tshirt na kofia bure !
2.Unapandishwa lori kama ng'ombe!
3.Unaenda kupata burudani ya kiwamgo cha fiesta!

Watanzania hata kama tunapenda vya bure na burudani,tukumbuke uhai nao ni muhimu zaidi!
 
Ivi mafisiem hayawezagi kwenda menyewe kwenye mikutano mpaka yapakiwe kwenye malori kama mizigo? Kuna ulazima gani kusomba watu na malori toka vijijini? Walioko eneo la mkutano hawatoshi? Ndo kwenda kujaza vichwa? Asante Mama yetu ulifumbua macho kule Musoma
Halafu utasikia asante wana Tunduma,mmevunja record haijawahi kutokea😁😁😁😁😁😁!
Hawa watu mshipa wa aibu wanao kweli?
 
Chama kina pesa za kuwalipia safari kwenda huko
Ivi mafisiem hayawezagi kwenda menyewe kwenye mikutano mpaka yapakiwe kwenye malori kama mizigo? Kuna ulazima gani kusomba watu na malori toka vijijini? Walioko eneo la mkutano hawatoshi? Ndo kwenda kujaza vichwa? Asante Mama yetu ulifumbua macho kule Musoma
 
Wananchi wa Tunduma wanafahamu unyama wote alioagiza ili kuwabambika kesi viongozi wa Chadema , akizomewa asimlilie mtu .
 
Umeambiwa kuna ajari imetokea huko

Back
Top Bottom