TBC katika taarifa yao kwa maelekezo kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa wametoa maangalizo mengi lakini mimi moja ambalo nimeliona kama mgombea Urais kupitia CCM analikiuka sana.
Lile tangazo linasema kuwa kama mgombea atakuwa jukwaani anamwaga sera basi atumie lugha ya Kiswahili tu, kama kutaonekana kuna haja ya kutumia lugha nyingine yaani native ya kikabila basi atafutwe mkalimani hili afasili na kufikisha ujumbe.
Cha kushangaza leo kuazia hile mitaa ya kina Kitwanga hadi Geita hadi kwa akina Msukuma hadi mwanza. Mzee nimemwona anakandamiza Kisukuma kwa sana. Hii lugha ya watani zangu ni nzuri kusikiliza maana hujui wanatumia ule ugali mgumu au nini, maana amekuwa anakandamiza njia nzima. Pia amekuwa anamwita First Lady Mama yule mpole sana tena mwalimu naye anaanza kwanza kwa kukandamiza alafu anaomba kura kwa Rais, Wabunge na Madiwani. Kwa kifupi wamekandamiza njia nzima.
Tunaomba mwongozo kwa vyombo vinavyohusika vitoe tafsiri kuhusu hili kwani linaweza kuchochea ukabila hapa Tanzania, na pia nimponge mgombea wa Urais kupitia CCM kwa kuwa ananadi sera zake bila kutumia lugha ngumu au kutupa mitusi kama baadhi ya wagombea wengine, kwani nimewaona wanakomaa na mtu binafsi, kashfa, mitusi na kujisahau kuwa watanzania wamekusanyika kusikiliza sera atawafanyia nini pindi watakapo mchagua, wanakuta kumbe akipata uongozi atakomaa na mtu flani.