Uchaguzi 2020 CHADEMA pelekeni Malalamiko NEC ya Ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi yanayofanywa na Mgombea Urais kupitia CCM

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
276
1,000
Kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili ya uchaguzi unaofanywa na mgombea wa urais kupitia CCM. Ukiukwaji huu ni pamoja na matumizi ya lugha za kikabila, vitisho, kutoa rushwa ya ujenzi wa barabara, nk.

Ni vyema Lissu na CHADEMA mkaandika malalamiko haya ya Ukiukwaji huu wa maadili kwa NEC kwa kuzingatia sheria ili tuzidi kuupima Uhuru wa NEC dhidi ya Boss wao.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,944
2,000
Mbali ya ccm ,wamwandikie malalamiko rasmi mkurugenzi NEC kwa kauli zake kibabe kuwananga wadau uchaguzi na kupigia debe ccm.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,122
2,000
Mkuu hapo ni sawa kabisa na kupeleka kesi ya uharibifu wa shamba la mahindi uliofanywa na ngedere kwa halimu nyani. Kwa kuwa atalitupilia mbali shauri hilo kwa kigezo mshtakiwa alikuwa na haki ya kuishi kutokana tishio la njaa.

CCM na tume ya taifa ni kama jamii ya nyani na ngedere, kwa kuwa lao ni moja, ni kujenga mazingira ya bao la mkono. Zoezi ambalo lilianzia ktk kutengeneza orodha yenye utata mkubwa ya wapigakura zaidi ya 29Mn. Hata ukiisikiliza lugha ya mkurugenzi wa NEC utatambua kabisa yupo 'biased'.

Ndiyo maana inawakera sana Tundu Lissu anaposisitizia suala uwazi ktk kupiga kura na zoezi zima la kuhesabu kura. Hukumu itapaswa itolewe na wananchi wenyewe na wala si hii tume isiyoaminika ambayo ni kama kinyago kilichochongwa kwa taswira ya CCM.
 

crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,415
2,000
Kupeleka malalamiko NEC ya jpm ni sawa na kupeleka kesi ya ngedere kwa nyani.Pale NEC wamejazwa makada hatariii.yule mjaluo aitwaye mahera anaongoza
Yaani hata wewe umeonyesha unamlalamikia nyani wakati kumbe unaungedele pia. Moja ya malalamiko ya msingi kwenye mada hii ni ukabila lakini description yako ya huyo Mahera na wewe umefanya hayo hayo!
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,512
2,000
Mnamfundisha uwoga tu!!!

Aongeze nguvu ya Kampeni, na mbowe SASA aanze kumuunga mkono,

Mbowe amekuwa tofauti Sana na uchaguzi wa 2015? Alitembea kwenye Kampeni na Lowasa kila Jimbo Hadi Kampeni zinaisha

Je, kunakausaliti mbowe anakafanya Ka Siri Siri?
 

Loxodona

JF-Expert Member
Apr 3, 2019
350
1,000
Nadhani upo umuhimu mkubwa sana wa kuwasilisha malalamiko kwa sababu zifuatazo.

1) Hadi Sasa NEC wanajifanya wanatenda haki, Tunataka tupate ushahidi usio na Shaka ya namna haki hiyo inavyotendeka. Je watamwita JPM kwenye Kamati ya Maadili?

2) Mgombea wa CCM amekuwa akivunja taratibu za Ukaguzi Mchana kweupe. Kwa machache tu, amekuwa akitoa ahadi zinazokatazwa na NEC Kama kujenga barabaran wkt huu wa Kampeni, kuahidi pesa n.k. Ameonesha dhahiri kuwa atabagua majimbo yatakayokuwa na wapinzani kwenye kuleta maendeleo na anafokea, anawatisha na kuwavimbia wapigakura wasiomwelewa.

3) Tumeona viongozi wengi wa Serikali wakijihisisha bila Soni na Kampeni. Tunamwona Waziri Mkuu bila Soni akifanya Kampeni Nchi mzima kwa kutumia fedha za walipa Kodi kufanya kampen kwa maslah ya Chama chake.

4) Tunaona Mawaziri bila hofu wakiendelea kutoa ahadi na kutekeleza mambo Mbalimbali kwa lengo la kuushawishi Umma.

5) Tumeona CCM ikipewa support na UDP pamoja na TLP Mchana kweupe, Ila support ya CDM kwa ACT and vice versa ikipigwa mkwara mbuzi. Tunataka tuone NEC itasema Nini kwenye hili.

6) Tumeona Dr. Mahera wa NEC Kama refa akishambulia lango na CDM. Tunataka tufaham, hulka hii refa kushambulia lango la timu moja inatafsiri Nini kadri tunapoelekea ukingoni? Je hatawabeba wagombea wa Chama chake? Mahera anaona bado anasifa ya kuaminiwa??

7) Tumeona Serikali via Police ikijiingiza kwenye kuvuruga Kampeni za CDM kwa kushambulia wafuasi wa CDM kwa matendo yaliyo halali na Kama yanayofanywa na Mgombea wa CCM. Mbaya zaidi NEC inafurahishwa na kushabikia uhuni huo. Tunataka kujua tafsiri yake ipoje.

Yapo mengi, so ni muhimu CDM na ACT wakapeleka malalamiko rasmi dhidi ya Mgombea wa CCM ili yafanyiwe kazi Mana Sasa hivi CCM na Mgombea wao ukiachia mbali kuwa wameshapanic ila ni Kama wapo juu ya sheria.
 
Jan 3, 2020
8
45
Mnamfundisha uwoga tu!!!

Aongeze nguvu ya Kampeni, na mbowe SASA aanze kumuunga mkono....


Hii ndiyo strategy! Mgombea Urais anajinadi yeye ili watu wamchague yeye siyo Mh Mbowe, angalia kampeni za waliotutangulia kwenye demokrasia... Obama alikua akizunguka mwenyewe na timu yake ya kampeni .... ni siku ya Convention tu ndio wanakuwepo “heavy weights” wote

Sayansi ya siasa ya CDM ni ya hali ya juu sana .... pili anakua na uwezo wa kuzunguka kwa haraka na kufanya mkutano popote .... kwa siku! Anakua anakidhi haja za wapiga kura kwa kuwa karibu nao zaidi na uwezo wake unaonekana ... mwisho ccm kwa wingi wao wanaonekana dhaifu kushindana na mtu mmoja kisaikolojia watu hawapendi wengi kumwonea mmoja
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
10,531
2,000
Kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili ya uchaguzi unaofanywa na mgombea wa urais kupitia CCM. Ukiukwaji huu ni pamoja na matumizi ya lugha za kikabila, vitisho, kutoa rushwa ya ujenzi wa barabara, nk...
Umesema kweli.
Ni muhimu kuzidi kuifunua na kuweka WAZI ushetani wa TUME inayojitangaza kuwa huru.
Huu ndio wakati muafaka wa luigalagaza hadharani hiyo TUME.
HAKUNA kuwaachia.
1601531183008.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom