Mgombea ubunge Chalinze kwa tiketi ya CHADEMA awekewa pingamizi

Wanajua ni sehemu ya kujipatia posho jawana watakalopata ndio maana wamepeleka mbulula.
 
CUF banaaa Agrrrrrrrrrrrrr
Hivi jamani, CUF mtakomaa lini? Mmeamua kujifunua kabisa ili tujue hata hiyo pesa ya fomu imetolewa na Shiishiieem?? Haya banaa nyie komaeni angalao muwatikise CDM kidogo huenda hizo kura zikapungua lakini cha moto mtakiona Chalinze. CUF mnaonesha jinsi mlivyo kwisha kabisa kisiasa mnangojea kuwezeshwa mnatamani hata kuwe na viti maalum vya cuf pekee
 
Inamaana wamasai wadzhabe wamang'ati watindiga hawatajakaa wawe wabunge?prof maji marefu anajua kusoma au kuandika?
 
Hakuna Mtanzania kwa wakati huu atakayeweza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya ubunge wakati hafahamu hata kusoma na kuandika achilia mbali mpaka kufikia kuapitishwa na chama kuwa mgombea wake.

Hizi kwangu ninaziona kama ni propaganda ambazo ni kuwapotezea muda hata wachunguzi. Ningeelewa kama pingamizi lingesema amesema ana elimu ya kiwango fulani wakati hana lakini siyo kutokujua kusoma na kuandika.

Hawa wanaoweka mapingamizi ingefaa wawe wanalipa fidia pale mapingamizi yao yanapotupiliwa mbali kwa sababu pingamizi kama hili linapoteza muda katika kushughurikia mambo mengine muhimu.

Ninaamini CHADEMA hawawezi kuwa katika kiwango cha chini kiasi hicho kwenye kuteuwa wagombea wake wa ubunge hasa katika uchaguzi mdogo.
 
Siamini kama mgombea ubunge wa Chadema hajui kusoma na kuandika.
 
siasa za bongo ni kama komedi, jamaa hata propaganda hajui...hivi chadema kinaweza mpitisha mtu asie juwa kusoma na kuandika kiswahili? huu ni upumbavu wa wapga propaganda

Ningeshauri mods awe anachambua nini post ya kuweka humu kwani hawa watu wengine ilibidi warudi kule facebook
 
Back
Top Bottom