Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Gairo Ahmed Shabiby amefanya kampeni za kuomba kura kwa kutumia helikopta ambapo amehaidi kuendelea kuboresha sekta ya kilimo cha umwagiliaji. Akiwa katika kampeni zake Shabiby amesema kuwa atahakikisha wananchi wananufaika na kilimo cha umwagiliaji ikiwa kwa sasa tayari mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji yameshaanza kujengwa. Aidha Mgombea huyo akazungumzia suala la ujenzi wa mifereji mikubwa itakayosaidia kuondoa adha ya mafuriko kwa baadhi ya maeneo pindi mvua zinakaponyesha.