Mgombea Ubunge Agawa Simu 800 Kwa Wananchi Musoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea Ubunge Agawa Simu 800 Kwa Wananchi Musoma

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by al-uden, Jul 25, 2010.

 1. a

  al-uden New Member

  #1
  Jul 25, 2010
  Joined: Jul 25, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mgombea Ubunge Agawa Simu 800 Kwa Wananchi Musoma

  Mgombea ubunge wa jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Bw. Nimrod Mkono ameanza kampeni yake ya kugombea ubunge kwa kugawa simu 800 kwa wananchi wake ili apate kupita. Malalamiko hayo yametolewa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM kutoka mkoa huo Bw. Anthony Mtaka wakati akizungumza na Nifahamishe.com.

  Alitoa malalamiko hayo kutokana na kauli ya hivi karibuni ya mbunge Nimrod Mkono ambaye anakitetea kiti chake cha ubunge, alipokaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akikiri kugawa simu na kuahidi kuendelea kugawa zaidi.

  Katika kauli yake, mbunge huyo alisema kuwa ataendelea kugawaza zaidi, kwa madai kwamba zitawasaidia wana CCM kuwasiliana na pia kuweza kukichangia chama chao.

  Akasema kuwa simu hizo ambazo tayari ametoa, zimegawiwa kwa utaratibu halali ulioelekezwa na chama chake kwa kuzikabidhi kwa viongozi wa chama ili wao ndio wazitoe kwa walengwa.

  Mkono alisema kuwa lengo lake ni kugawa simu zaidi ya 800 ili zitatumike kwa kile kilichokusudiwa ambapo wana CCM waliopo vijijini wataweza kutoa fedha kidogo kuchangia Chama cha Mapinduzi.

  Hata hivyo, kauli hiyo ya Mkono imemsikitisha mjumbe huyo ambaye amedai kuwa jimbo la Musoma Vijijini lina matatizo mengi ambayo yanatakiwa kutafutiwa ufumbuzi na sio hizo simu anazogawa.

  "Kauli ya mbunge wetu kwa kweli imenisikitikisha, nilisoma kwenye magazeti akikiri kugawa simu za mkononi huku akiahidi kuendelea kugawa na kuacha matatizo ya msingi jimboni mwake," alisema Bw. Mtaka.

  Alisema kuwa jimbo hilo lina changamoto nyingi za maendeleo ambazo zinafanana na majimbo mengine hapa nchini, hivyo yanahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka na sio kugawa simu za mkononi.

  Alidai tarafa zote za jimbo hilo zikiwemo za Kiagata, Makongoro na Nyanja zina matatizo mengi kama ubovu wa barabara, shule kukosa mabweni, vyoo na mengine mengi yanayohitaji ufumbuzi wa haraka.

  "Badala ya kushughulikia hayo, mbunge anajigamba kwa kugawa simu za promosheni kwa wana CCM, hili kwa kweli mimi kama mwana CCM na kiongozi limenisikitisha sana," alisema.

  Alisema kuwa ni vyema mbunge huyo akashughulikia matatizo ya jimbo badala ya hilo alilolifanya la kugawa simu eti zisaidie wana CCM kuchangia chama chao kabla ya uchaguzi.

  Alisema kukichangia chama sio muhimu, lakini inategemea na mhusika yuko katika mazingira gani na kudai kuwa wananchi wa jimbo hilo wanakabaliwa na matatizo mengi yanayokwamisha maendeleo yao.

  "Yeye kama mwana CCM mwenzangu, nimeona nimkumbushe hayo ili anapoendelea na utaratibu wa kugawa simu, atambue yapo matatizo ya msingi anayopaswa kuyapa kipaumbele," alisema.

  Sakata la ugawaji simu hizo kwa sasa liko mikononi wa Takukuru mkoani humo ambao bado wanaendelea na uchunguzi wao ili kubaini uhalali wa mgawo wa simu hizo.
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hao ndio "si si mafisadi" hawataki mchezo.
   
 3. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hata wewe ukiweza kagawe ulichonacho!
   
 4. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  umepewa bure unatoa bure
   
 5. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kama un audhiwa na hali hiyo unafanya nini ndani ya CCM?

  Wenye CCM hawashangai hayo. Rushwa ni sehemu ya CCM.

  Jitoe haraka ccm
   
Loading...