Mgombea mwenza kumwangusha Magufuli

Mgombea mwenza kumwangusha Magufuli

Kuna chama chenye mipasho kama CHADEMA.Kikianza kuimba wimbo wa mafisadi utafikiri eehe shoga leo kakachachamaa kibarazani.Fisadi likitokea tu kibarazani CHadema inaanza kuimba wimbo wa taarabu Lowasa si fisadi.Unakuja kugundua CHADEMA hamjambo kwa mipasho jiandaeni kupewa na nyie mipasho.Huyu mama ndie saizi yenu.
 
Nitawashangaa sana wazanzibar kama watampa kura huyu mama na kuzima ndoto ya wazanzibar ya kujipatia mamlaka kamili ndani ya muungano. Ndiye amezima ndoto za wazanzibar, ni fursa nzuri wazanzibar kuonyesha hasira zenu maana kinachofanyika huyu anataka kuzawadiwa kwa kuwasaliti maoni yenu leo eti awe makamu wa rais. Mkimchagua mtakuwa mmezika ndoto ya zanzibar kujipatia mamlaka na mtabakia mkilalamika

Thubutuuuu!! Nani ampe huyu kihanyuda cha wakubwa wa chimwaga kula??
 
Sasa wewe Chadema una washauri Ccm.Acheni kuhangaika na mambo yasiyowahusu.Mawazo yako kamshauri Fisadi Lowasa Na Movement ya kidini(kilutheri)

Na huyo wenu movement yake ya ukatoliki na uuzwaji wa nyumba za serikali kwa ndugu zake tena kwa bei isiyo ya soko hamyaoni?Vile vivuko vibovu na mashine za kukatia tiketi nazo? Upotevu wa billion zaidi ya 300kwenye wizara yake kama ulivyoletwa bungeni juzi na maelezo kukosekana nayo ni movement nyingine. Mnapenda kurusha mawe bila kujua mpo kwenye nyumba ya kioo?
 
Kuna sababu 3 zitakazopelekea CCM ianguke kwa kuwa na mgombea mwenza mwanamke:

1. Mfumo dume bado una nguvu katika makabila mengi hususani vijijini. Wananchi wengi hawaamini kama wanaweza kuongozwa na rais mwanamke hivyo kumnyima kura.

2. Kushindwa kwa Bi.Anne Makinda katika kulisimamia bunge lililopita ambalo lilitawaliwa na ubabe na kubebwa CCM. Ni katika bunge hili wananchi wameshuhudia sheria mbalimbali za hovyo zikipitishwa kibabe na serikali chini ya ulinzi mkali wa spika Anne.

3. Mgombea mwenza ndiye alikuwa makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba; chini ya usimamizi wake tulishuhudia kanuni zikivunjwa ili kuichakachua katiba ya wananchi.

Ni katika kipindi hicho tulishuhudia matusi, kejeli, na vitimbi kutoka kwa wajumbe, huku wakitetewa na uongozi wao. Na kutokana na uchakachuaji huo ndipo ukawa ilizaliwa rasmi chini ya mgombea huyu.

Leo hii anaenda kwa wananchi waliotoa maoni ya katiba kutaka achaguliwe urais...ccm na Magufuli mnalo mwaka huu.

hapa naona kura za waislamu kuzipata afanye kazi ya ziada misikiti mingi kwa waislamu huongozwa na wanaume .
 
mama wa kura za facebook bunge la katiba ndio ccm wamemlipa baada ya kusigina katiba pendekezwa ya wananchi hakika ni kimeo kimeo kimeo
 
Hao ndio wale wanaitwa "Bora Viongozi" badala ya "Viongozi Bora"

Ndio maana huu ni wakati wa madiliko pamoja na mambo mengine ni kuweza kubadili mindset na mifumo ya hovyo zikiwemo teuzi za watu wasiokuwa na uwezo wa kuongoza taifa kwa kukosa 'merit' kama hawa.
 
ivi uyu mama anaweza ongea nn mbele ya watu wenye akili!!! ktk east africa uyu mama anaweza kaa meza moja na wakenya na waganda na wanyarwanda akasikilizwa? ana cv yoyote kweli uyu? tupate cv yake tafadhali
 
Tatizo sio Elimu yake wala kusoma hotuba .
Tena ni bora anayesoma. Mkapa Juzi angesoma hotuba yake asingetukana 80% ya watanzania.

Tatizo lililopo ni CCM hakuna jipya . Wote ni wafia neno CCM tu. Wanaona na kusikia raha sana wakisikia neno CCM basi. Mambo mengine hayawahusu kwani yanawagusa malofa na wapumbavu.
 
ha ha,jana watu walishindwa wasemaje baada ya lowasa kumaliza kulihutubia taifa.
nilikua salooni nanyoa,niliwaona vijana wa salooni wamenywea ghafla,,,nikawaonea huruma sana....
 
Back
Top Bottom