Mgogoro waitikisa CHADEMA!

Mgogoro waitikisa CHADEMA!

Siku za mwisho kila kitu kitasemwa ilimradi mtu anakufa. Magamba wanajua hizi ni nyakati za mwisho na ndio maana wanatapatapa, kwa kuwatumia waandishi wa habari vihiyo. Almost two years to go Magamba.........before we seize state power!!
 
hapo kwenye red, naona unatafuta kuingiza siku mkuu, hivi kwa akili yako mbunge anawezaje kula pesa? Yeye ni mhasibu?
kula pesa siyo lazima uwe mhasibu ukisema waziri amekula pesa kwani yeye ni mhasibu wa wizara? Kilichopo ni kwamba ana shirikiana na wahasibu kula fedha,,
 
Mkitaka kuwalaumu Chadema na kuwashtaki kwa wananchi mwondoeni Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa halmashauri ndipo wananchi tutawaelewa, vinginevyo msitudanganye.
 
MGOGORO mkubwa unakinyemelea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kuelezwa kuwa sekretarieti yake imekayakataa mapendekezo ya Tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo, ukiwamo wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu), ambayo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.

Mradi huo wa maji unaelezwa kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alisema kwamba baadhi ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Karatu uliko mradi huo walihojiwa jana, lakini akasema hapakuwa na mpango wowote wa kufukuzana.

“Ninachoelewa ni kwamba waliitwa wakahojiwa na kitakachofuata ni kupewa maagizo ambayo lazima wayafuate na atakayekiuka ndiye atakayefukuzwa,” alisema Mwigamba.

Soma zaidi: Mgogoro waitikisa Chadema - Siasa - mwananchi.co.tz

Kamradi kamoja tu, namna hii, jee ikitokea bahati mbaya mkapewa japo mkoa mmoja muuendeshe si itakuwa kasheshe?
 
Back
Top Bottom