Mgogoro waitikisa CHADEMA!

Mgogoro waitikisa CHADEMA!

Mkuu Ritz
Hivi tutasalimika na hawa viongozi wa Chadema? Waporaji wake za watu; majambazi; mafisadi waongo wote wamo humo kweli kazi ipo.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama,
Dr Slaa kashindwa kuwafukuza ndugu zake wa Karatu kwa ufisadi damu nzito...

Angekuwa Mwita Maranya, kafanya huo ufisadi saizi yupo angekuwa Mugumu Standi na mabegi yake.

Jiulize kwa nini Dr Slaa ambaye anajifanya kupambana na ufisadi kakaa kimya kwenye huu ufisadi.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaha... Mkuu chama naona umeamua kumpigia Ritz baada ya kuku-''beep'' kwa muda mrefu.
Mtahangaika sana lakini mtaishia kuisoma namba japo kimya kimya!

Nimecheka unamwambia Lema akakufanyie kampeni Mugumu.
 
Last edited by a moderator:
Mods uko wapi? unaruhusu uongo hadharani humu jamvin....huyu ritz mwongo sana...soma vizuri mwananchi kama limataja watuhumiwa...

Mkuu acha kukurupuka leta basi huo ukweli wako.
 
Kwani wazabuni wanachaguliwa na nani? Tuchambue kwa kujenga sio kwa nia ya madaraka tu. Halmashauri zinazoongozwa na chadema zilitakuwa kuwa mfano.

mkuu usitegemee hata siku moja halmashauri inayoongozwa na chadema ikawa ya mfano ccm ikiendelea kuwepo madarakani.kwa sababu miradi yote ya halmashauri inategemea mapato kutoka kwa wakusanya kodi ambao ni serekali ya ccm ambao hawatakuwa tayari kuziona halmashauri zinazoongozwa na chadema zinafanikiwa watahakikisha wanatumia mbinu zozote ili chadema waonekane kuwa hawafai.nitatowa mfano mmoja halisi uliotokea mwaka mmoja wilaya ya Biharamlo mkoani kagera wakati mfumo wa vyama vingi umeanza tu kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza kabisa wa mfumo wa vyama vingi.

CHADEMA walifanikiwa kupata kata moja ya udiwani katika kata ya Runazi.baada ya kupata kata hiyo katibu wa ccm wa wilaya siku moja aliitisha mkutano wa hadhara akasema kuwa kata ile ya Runazi ambao wamechaguwa diwani wa upinzani wasahau kamwe kupelekewa huduma za maendeleo. Kauli ambayo iliambatana na kukatishwa kwa shuguri zote za kimaendeleo katika kata hiyo mpaka diwani wa chadema alipokuja kununuliwa na ccm. Ndipo miradi ya kimaendeleo ilipo rudishwa.

Diwani wa chadema alinunuliwa na ccm baada ya kuonekana kuwa katika madiwani wote waliochaguliwa hakuna aliesoma isipo kuwa ni diwani wa chadema tu ambae alikuwa ni form four. Na hilo lilitokea baada ya serekali ya sweden ambao walikuwa wanaendesha miradi kadhaa katika wilaya ya biharamlo kumtaka mkurugenzi wa wilaya aende nchini swiden kwenda kuangalia jinsi wanavyofanya shughuri za kimaendeleo katika safari hiyo mkurugenzi alitakiwa aongozane na mwenyekiti wa halmashauri.

Sharti kuu ilikuwa ni lazima wawe wanajuwa kuongea kingereza.mwenye kiti wa halmashauri alikuwa hajui kuongea kingereza na madiwani wote wa ccm walikuwa hawajui isipokuwa ni wa chadema peke ndiealiyekuwa anaweza kuongea kingereza hivyo ilibidi ateuliwe iliaondoke namkurugenzi kwa niaba ya mwenyekiti wa halmashauri.

Baada ya ziara hiyo kwisha na viongozi hao kurudi, wananchi walishangaa tena katibu yuleyule wa ccm anatangaza kwenye mkutano wa hadhara kuwa diwani wa kata ya Runazi amejiuzuru na kurudi ccm baada ya kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Runazi, baada ya uchaguzi kuitishwa kata hiyo ilirudi ccm.

Hapo ndipo nilipo amini kuwa ccm siyo ya kawaida.
 
cdm si ndo wanaongoza halmashauri na ndio wenye maamuzi mana katika halmashauri madiwani ndio wenye mamlaka ya mwisho....sasa hao wamekula fedha za miradi.....
Tulitegemea cdm mtakuwa mfano wa kuungwa katika halmashauri za wilaya mnazoziongoza lakini mumeonhyesha uzaifu mkubwa kuwa hakuna kitu ni maneno maneno tu ..... Halmashauri tu inawshinda je mtaweza ongoza nchi??????.......

Tumia akili, mbunge na mwenyekiti Wa halmashauri hawahusiki na pesa. Umedanganywa na propaganda za Ritz Na wewe unarukia bila reasoning.

Watu wanaohusika na pesa halmashauri ni mweka hazina, mkurugenzi na Mkuu Wa idara husika.
 
Wanabodi.

Chama cha CHADEMA kimefanya ufisadi mkubwa na kukwamisha miradi mingi ikiwemo Mradi wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu) tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi hiyo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.

Mradi huo wa maji umeleta mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambayo wanatajwa kufanya ufisadi ni Mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa viti maalumu Cicilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini Jubiless Mnyenye.

SOURCE: MWANANCHI DESEMBA 17, 2012.

Mkuu acha kudanganya watu!

Gazeti la Mwananchi si nalo ni la bosi wako? Sasa Unategemea nini kuhusu uhakika wa hizo taarifa!

Watu wanaohusika na pesa halmashauri ni mweka hazina, mkurugenzi na Mkuu Wa idara husika sio mbunge Au mwenyekiti Wa halmashauri!
 
Wanabodi.

Chama cha CHADEMA kimefanya ufisadi mkubwa na kukwamisha miradi mingi ikiwemo Mradi wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu) tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi hiyo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.

Mradi huo wa maji umeleta mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambayo wanatajwa kufanya ufisadi ni Mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa viti maalumu Cicilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini Jubiless Mnyenye.

SOURCE: MWANANCHI DESEMBA 17, 2012.
Mkuu ritz acha umbeya,kadiri ya siku zinavyozidi ,unazidi kujishushia heshima tu jamvini.Una shida gani kunako ubongo,bila kushabikia uzushi unaohusu CHADEMA? aha! aha! mkuu unafirisika,labda uje na ID mpya,hongera kwa kuchagua ujinga.
 
mwananchi nao wameanza kuuza kw ajina la CDM?watapotezwa kisiasa kama Mkama, au Kinana anapoelekezwa.
 
Waungwana chama cha CHADEMA kipo katika kipindi kigumu ambaho uongozi wake haujuwi pa kushika ili kurudi katika mstari wa kawaida. Hali imekuwa mbaya kwa vile vuguvugu la kutaka mabadiliko limeanzishwa na vijana ambao wana nguvu kubwa ya ushawishi ndani ya chama. Haijulikani uongozi wa juu utakuja na kauli gani baada ya kuendesha vikao siku 2 mfululizo pasipo ajenda zenye mshiko; huku matawini waanachama wanajiuliza kulikoni hatima ya chama chao; hasa tuhuma nzito dhidi ya Dr. Slaa zina asilimia kubwa ya ukweli pasipo kupata wazo mbadala kutoka kwa Dr. Slaa na Mwenyekiti wa Chama.
Dalili zipo wazi kuwa CHADEMA imeshindwa M4C badala yake kivitendo wanaendesha M4D ikiashiria mwisho wa CDM na harakati zao kuelekea mjengoni Magogoni.
KILICHOPO SASA HIVI NDANI YA CDM NI MATUMIZI YASIYO NA TIJA KUTUMIA RASLIMALI IKIWEPO RUZUKU NYINGI KUENDESHA VIKAO VYA MAELEWANO BADALA YA KUIMARISHA CHAMA.
 
How much they paying you!? Angalia hapa chini ujione ulivyo mtu wa hovyo ni wewe na Chadema tu.

Results 1 to 30 of 101
 
Mvuto wa thread si rangi rangi na kukuza font. Ni mashiko yaliyo katika hoja.

Mkuu thread zako hazina mvuto. Ndio maana unakazana kuchangia wewe mwenyewe.

Jipange upya.
 
Results 1 to 30 of 101
 
Wanabodi.

Chama cha CHADEMA kimefanya ufisadi mkubwa na kukwamisha miradi mingi ikiwemo Mradi wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu) tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi hiyo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.

Mradi huo wa maji umeleta mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambayo wanatajwa kufanya ufisadi ni Mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa viti maalumu Cicilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini Jubiless Mnyenye.

SOURCE: MWANANCHI DESEMBA 17, 2012.
Naona mambo yameanza kuwekwa hadharani
 
Huyu MAFILILI ni gamba gumu sana na kazi yake ni kumwaga pumba na mashudu humu JF sasa ni muda wake wa kusubiria Xmas ili aende akapokee ujira wake wa pilau ya mchicha pale Lumumba.
 
Last edited by a moderator:
Waungwana chama cha CHADEMA kipo katika kipindi kigumu ambaho uongozi wake haujuwi pa kushika ili kurudi katika mstari wa kawaida. Hali imekuwa mbaya kwa vile vuguvugu la kutaka mabadiliko limeanzishwa na vijana ambao wana nguvu kubwa ya ushawishi ndani ya chama. Haijulikani uongozi wa juu utakuja na kauli gani baada ya kuendesha vikao siku 2 mfululizo pasipo ajenda zenye mshiko; huku matawini waanachama wanajiuliza kulikoni hatima ya chama chao; hasa tuhuma nzito dhidi ya Dr. Slaa zina asilimia kubwa ya ukweli pasipo kupata wazo mbadala kutoka kwa Dr. Slaa na Mwenyekiti wa Chama.
Dalili zipo wazi kuwa CHADEMA imeshindwa M4C badala yake kivitendo wanaendesha M4D ikiashiria mwisho wa CDM na harakati zao kuelekea mjengoni Magogoni.
KILICHOPO SASA HIVI NDANI YA CDM NI MATUMIZI YASIYO NA TIJA KUTUMIA RASLIMALI IKIWEPO RUZUKU NYINGI KUENDESHA VIKAO VYA MAELEWANO BADALA YA KUIMARISHA CHAMA.

Tatizo ukiwa CCM ni lazima upeo wako wa kufikiri unakuwa mfupi kama chupa ya azam cola.
 
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Wilaya ya Karatu, imependekeza kufukuzwa uanachama kwa Diwani wa Kata ya Karatu Mjini, Jubilate Mnyenye, ili kukinusuru chama hicho.

Pendekezo hilo linakuja wakati Kamati Kuu ya Chadema, leo inatarajia kutangaza uamuzi, kuhusu mgogoro wa viongozi wa chama hicho wilayani humo.
Mnyenye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi wa Kusambaza Maji wilayani Karatu (Kaviwasu), alitiwa hatiani na kamati hiyo, akidaiwa kukisaliti chama.

Pia kuhujumu mradi huo, ambao ndiyo nguzo ya chama hicho wilayani Karatu. Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe ,alikiri Kamati ya Utendaji ya chama hicho, kupendekeza kwa Kamati Kuu, imvue uanachama Mnyenye kwa kukisaliti chama.

Alisema Manyenye ametiwa hatiani kutokana na mikwaruzo kati yake na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Maasai na viongozi wengine. Pia kusaliti msimamo wa madiwani wa Chadema katika vikao vya baraza la madiwani.

“Mwenzetu huyu pia, amekuwa akishiriki katika vikao mbalimbali vya vijana wa CCM katika mji wa Karatu, jambo ambalo tunaamini ni makosa,” alisema Darabe.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alipotakiwa kuelezea uamuzi ya Kamati Kuu, alisema, “Mzungumzaji ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, John Mnyika.
“Naomba uwasiliane na Mnyika ndiye tuliyempa jukumu la kuzungumza na vyombo vya habari,” alisema Dk Slaa.

Hata hivyo, Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubunge, alipotakiwa kueleza uamuzi wa kikao hicho, alisema: “Yote yanayohusu kikao yatatangazwa kesho [leo],” alisema.
Wakati Chadema wakisigana, Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kinatumia nafasi hiyo ya mgogoro kujitengenezea mazingira ya kulirejesha jimbo hilo mikononi mwake.

Kuonyesha kuwa kinalitaka kwa dhati jimbo hilo, CCM wilayani Karatu imezindua kampeni za kurejesha jimbo hilo na Halmashauri ya Karatu, vinavyoshikiliwa na Chadema. Tayari chama hicho tawala kimeanza mkakati wake wa kushughulikia tatizo la uhaba wa maji, ambalo sasa limewaingiza katika mgogoro mkubwa viongozi wa Chadema.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Wilaya ya Karatu, Daniel Awakie, alizindua kampeni ya kulirejesha jimbo na halmashauri wakati wa mkutano wa kwanza wa CCM tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wanachama wa chama hicho, ulifanyika kwenye Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu.
 
Back
Top Bottom