Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 130
- 118
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Thomas Nkola maarufu kwa jina la Mkulima, amepinga vikali uamuzi wa chama hicho kuwatoza wafugaji Sh 15 milioni kutoka kila kanda kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano la Wafugaji Tanzania linalotarajiwa kufanyika mwezi huu mjini Bariadi, mkoani Simiyu.
Amesema michango hiyo si halali kwa kuwa CCWT ni miongoni mwa waalikwa kwenye kongamano hilo kupitia mwaliko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na si waandaaji wakuu wa shughuli hiyo.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Mathayo Mgusa ameandika barua kwa Vyama mbalimbali vya wafugaji ikiwemo Umoja wa Wafugaji mkoa wa Kagera kuchangia kiasi cha fedha Sh 15 milioni kwa ajili ya kongamano hilo.
Amesema kuwa hatua hiyo inaleta taswira potofu kwamba ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan kama mgeni rasmi unaleta mzigo kwa wafugaji, jambo ambalo linamvunja moyo.
Amesema kuwa kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Juni 14 hadi 15 katika Viwanja vya Nyakabidi, wilayani Bariadi, huku kilele chake kikitarajiwa kuwa Juni 16, 2025 na kuhudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan kama mgeni rasmi.
Ametoa wito kwa viongozi wa chama hicho kuzingatia uwazi na kuwaheshimu wafugaji wanaowakilisha, akisisitiza kuwa chama kisitumike kama kichaka cha kuchangisha fedha isivyo halali.
“Matendo kama haya ndiyo yanayopunguza imani ya wafugaji kwa chama na hata kwa serikali. Tuwaambie ukweli, tusitumie jina la Rais au mwaliko wa wizara kujinufaisha,” amesema.