Matema Beach
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 364
- 67
Nape unakumbuka shuka wakati kumekucha. Leo ndio unaona Taifa kwanza chama baadaye? Pole sana bro kwani najua umechelewa sana kaka
Kumekuwa na mijadala kadhaa juu ya namna mambo yanavyokwenda ndani ya CCM hasa kufuatia sakata la madiwani na Meya wa Manispaa ya Bukoba. Kimsingi hali si tete kama inavyojaribu kuelezwa. Taratibu, kanuni, sheria na Katiba ya Chama kupitia vikao vitatumika kulimaliza swala hili kwa amani kabisa. Mwisho wa siku lazima wananchi wa Bukoba na Manispaa yao wapate haki yao ya msingi!
Nimewahi kusema siku nyingi kidogo kuwa NCHI KWANZA VYAMA BAADAE! Tafsiri rahisi hapa ni kuwa masilahi ya wananchi na nchi yao kwanza, masilahi ya Chama na itikadi zetu baadae!
Hivyo kwa kifupi kwa swala la Bukoba lazima masilahi ya wananchi wa Bukoba yatangulizwe mbele na yavuke ushabiki wa kiitikadi. Hatuwezi kupofushwa na mapenzi kwa vyama vyetu tukafumbia macho masilahi mapana ya wanachi wa Bukoba!
Hii haimaanishi sikipendi Chama changu bali ukweli ni kuwa naipenda sana CCM yangu lakini naipenda zaidi nchi yangu!
Mungu ibariki nchi yangu nzuri ya Tanzania
Mungu ibariki CCM iwahudumie vyema Watanzania!
Splendid indeed Mkuu.Mkuu mimi nadhani hatua ya Nape kutaka madiwani waendelee na kazi hadi vikao vya juu vitakapoamua hatma yao ndio yalikuwa maslahi ya Taifa na si Chama!!! Sioni mgogoro wa kuturudisha kwenye uchaguzi.Ubabe wa meya na Kagasheki hauwezi kugharimu kodi za wananchi na muda wao.
Kumekuwa na mijadala kadhaa juu ya namna mambo yanavyokwenda ndani ya CCM hasa kufuatia sakata la madiwani na Meya wa Manispaa ya Bukoba. Kimsingi hali si tete kama inavyojaribu kuelezwa. Taratibu, kanuni, sheria na Katiba ya Chama kupitia vikao vitatumika kulimaliza swala hili kwa amani kabisa. Mwisho wa siku lazima wananchi wa Bukoba na Manispaa yao wapate haki yao ya msingi!
Nimewahi kusema siku nyingi kidogo kuwa NCHI KWANZA VYAMA BAADAE! Tafsiri rahisi hapa ni kuwa masilahi ya wananchi na nchi yao kwanza, masilahi ya Chama na itikadi zetu baadae!
Hivyo kwa kifupi kwa swala la Bukoba lazima masilahi ya wananchi wa Bukoba yatangulizwe mbele na yavuke ushabiki wa kiitikadi. Hatuwezi kupofushwa na mapenzi kwa vyama vyetu tukafumbia macho masilahi mapana ya wanachi wa Bukoba!
Hii haimaanishi sikipendi Chama changu bali ukweli ni kuwa naipenda sana CCM yangu lakini naipenda zaidi nchi yangu!
Mungu ibariki nchi yangu nzuri ya Tanzania
Mungu ibariki CCM iwahudumie vyema Watanzania!
:focus:Nape Nnauye kati ya CCM na CCJ kipi unakipenda zaidi, je kwenye swala kuvua gamba masilahi ya nani? ulizingatia..