Kagera: Paul Makonda ampa miezi 3 Waziri wa TAMISEMI kuhakikisha soko na stendi vinaanza kujengwa Bukoba

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Wanamuita Comrede Makonda hapoi Wala haboi.

Atoa miezi 3 Kwa Mchengerwa kuhakikisha Soko na Standi Vinaanza mara Moja.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempa miezi mitatu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa, kuhakikisha wanaanza ujenzi wa stendi ya mabasi na soko la kisasa katika Manispaa ya Bukoba Mjini mkoani Kagera.

Agizo hilo limetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mayunga mkoani huko.

Makonda amesema amepokea kero ya ujenzi wa soko lisilokamilika na ameshangazwa Bukoba kukosa stendi ya mabasi ya kisasa.

"Chama kinampa miezi mitatu Waziri Mchengerwa tuone ujenzi wa soko la kisasa na stendi ya mabasi kuanza kujengwa hiki chama sio cha porojo tunatakiwa kutatua kero za wananchi ngoja nimpigie simu Waziri kumjulisha hili,"amesema

Mchengerwa baada ya kupokea simu ya Makonda ambayo wananchi hao walikuwa wakimsikiliza, amesema amepokea maelekezo na tayari, Rais Samia Suluhu Hassan, alishatoa maelekezo kuhusiana na suala hilo na kwa sasa wanaenda kutekeleza kwa kuwa lipo katika ilani ya chama.

Amesema ifikapo Desemba mwaka huu atakuwa ameshafika katika mkoa wa Kagera kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa maagizo aliyopatiwa.
 
Tunapima Ziara ya Jeshi la Mtu Mmoja na ile Operesheni +255 Katiba Mpya Okoa Bandari Zetu 😂
Jeshi la mtu linatetemesha mpaka ngome za walamba asali.

Lakini hii iwe wake up call kwa walamba asali, wahakikishe inapatikana katiba bora sasa.

Sisi tunaojilamba midomo hatuna cha kupoteza. Tukiletewa PCM kwenye ballot box sisi tunatia tiki, wakahangaike naye huku mbele.
CCM daini katiba mpya sasa kabla kibao hakijageuka.
 
Ziara za Nyumbu hazinaga matokeo kaka

Makonda anatoa maagizo na wananchi wamatatuliwa kero zao

Wengine wanapita wakiropoka tu no solution full kiki tu
Kuna mzee wa Kimarangu aliwahi kuniambia.

Glenn kijana wangu, usifikiri wachaga wote ni smart kichwani, kuna wachaga ni wa hovyo kuliko uhovyo wenyewe....nimeshuhudia hili hapa jf🤣🤣
 
Back
Top Bottom