Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 887
- 2,201
Wengi tuliamini kuwa kuondolewa kwa zuio la mikutano ya kisiasa ya hadhara ingekuja na neema na utulivu wa kisiasa lakini hali imekuwa tofauti baada ya viongozi waandamizi Chadema kutofautiana kimtazamo huku kundi moja linaloongozwa na John Heche kutaka Tundu Lissu ndiye awe M/Kiti wa chama na Mbowe arudi nyumbani.
Kundi lingine linalodaiwa kuongozwa na Halima Mdee aliyefukuzwa uanachama na wenzake 18 bado wanaomuona Mbowe kama nguzo ya Chadema. Aidha, taarifa kutoka ndani ya makundi hayo kupitia group la WhatsApp la kundi la kwanza likijiita "Mageuzi 2025" wanamshutumu Mbowe kukiuka Katiba ya chama na kuifanya chama hicho kuwa mali yake na familia.
Hata hivyo imeelezwa kwamba baada ya Mbowe kunusa taarifa hizo baada ya kuletewa screenshot za mawasiliano ya kundi linalompinga na kudai amelamba asali bila kuwaonjesha wenzie kina Msigwa, amemshitutisha Lissu kukanusha kuwa hana mpango wala hajawahi kuoa kuwa hata Makamu M/Kiti lakini aliombwa na chama. Kauli hii imemuudhi mno Mbowe na kuona kwamba kumbe aliombwa pia kuwa Mwenyekiti wa chama hicho basi Mbowe hana chake.
Taarifa kutoka kwenye familia ya Mbowe zimedai kwamba baada ya Mbowe kuomba ushauri wa kimkakati muasisi wa chama hicho ambaye pia ni babamkwe wake Edwin Mtei, Mzee huyo alimjibu mkwewe kifupi na kumwambia "call him here". Tayari Lissu ameitwa na Mtei na logistic itakayotumika ni "kwenda kumpa pole Mtei Kwa kufiwa na mkewe Mbowe akiwa jela".
Hata hivyo familia ya Lissu wakiongozaa na kaka yake Aluta wamemtahadharisha Lissu kuwa makini na Mbowe huku wakimkumbusha ya Chacha Wangwe. Inaelezwa kuwa aliyebaki bila upande ni John Mnyika na haijulikani ni kwa nini.
My take: Chadema nyumba mnayoijenga ni moja ya nini kugombania fito kiasi Cha kutoaminiana maana mwisho mtauana. Nawasilisha.