madia madia
JF-Expert Member
- Sep 30, 2017
- 717
- 703
Pole sana aisee. Hata mm nlitaka nikwambie umuulize mama Yako atakua anajua but bora ulifanya hivyo. Kikubwa mzee ameathirika kisaikolojia hivyo msamehe Bado ni mlezi wako.Salam za asubuhi wakuu.
Kwanza let me declare my interest kuwa simchukii baba yangu.
Bila kupoteza muda leo nimeona nilitoe tatizo langu hili wanasema mficha maradhi kifo humuumbua.
Mimi ni mtoto wa kiume kwenye familia ya watoto wanne, mimi ndio wa kwanza, watatu waliobaki ni wa kike. Basi katika ukuaji kulikua na tabia ya baba kuwa mkali sana endapo nikikosea jambo nitapigwa fimbo, ngumi za kutosha na maneno makali sana ya kila namna, ambayo yalikuwa yakiingia moyoni kabisa na kujeruhi hisia, nilijipa moyo kuwa huenda ni kwa sababu mimi ni wa kwanza natakiwa niwe mfano.
Ilifika siku baba ametoka safarini usiku, tulichelewa kwenda kumpokea mizigo, kwa maana wakati bodaboda inapiga honi hatukusikia, vile natoka tu kwenda kumpokea nilikutana nae akatua mizigo hapo hapo akaanza kunishushia kipigo hapo hapo, rungu kumbe alikuwa amekuja nazo, nilipigwa magoti mpaka nikashindwa kuamka, alipomaliza akahamishia kipigo kwa mama.
Basi mdogo wangu wa kike akamuandalia chakula akala, baada ya kula akaanza kutukana, alipomaliza kutukana akanitemea mate akaenda kulala[emoji26] .
Nikaendelea na shule hivyohivyo, hatimaye nikapata nafasi ya kujiunga chuo nikawa nimefanikiwa kutoka nyumbani bado mahusiano na baba yakiwa sio mazuri.
Nikipata likizo kwenda nyumbani, mambo ni yaleyale, mpaka ninapoandika sasa hivi nikiwa mtu mzima mzee wangu kauli ya kistaarabu kwangu hana nikikosea kidogo ananidhalilisha, nyumbani kwao yaani kwa bibi na babu ameshanisema sana kuwa mimi sio mtoto mzuri, wakati juhudi zangu zinaonekana kama ni elimu nimejitahidi sana kuipata, now ni msaada kwa wadogo zangu, lolote nitakalofanya kwa mzee ni baya.
Namheshimu sana mzee maana amenihangaikia sana mpaka hapa nilipo, nimejitahidi to make him proud in all means lakini kila ninalofanya inaonekana si lolote si chochote [emoji17] . Nimejitahidi sana kufanya jitihada za kuondoa kero yoyote kwa mzee, huenda ndiyo maana anakasirika Ila bado tu, uso wake unaonekana una chuki. Nikaamua nikae mbali tu maana jitihada zangu zimefail, yaani hata nyumbani huwa naenda akiwa hayupo!
Matukio ni mengi sana kama hayo , wakati mwingine kosa ni dogo tu maneno machafu kabisa nimejaribu kufupisha tu.
Basi waungwana wanasema "Time tells!" . Siku zimekwenda nimekuja kugundua kuwa mimi ni mtoto wa nje! Je nimegunduaje?
Baada ya kuwa mtu mzima na kuona kwamba hali hii si ya kawaida ikabidi nimuulize mama mbona hivi? Mbona mzee anaonesha upendeleo wazi wazi, chuki zisizoisha na maneno machafu? Mpaka leo hii ni salamu tu.
Basi mama akanikalisha chini, akanipa ukweli halisi wa mambo kuwa baba yako yupo mwingine hata yeye anajua kabisa, mama alinionesha na nikiri nilipomuona nilijua huyu ndiye baba yangu mzazi tumefanana sana, akaniambia wala usishangae na mambo yanayoendelea, kubali endelea na maisha mengine.
Let me declare my interest kuwa simchukii mzee wangu ila moyo wangu hauna upendo naye, naappreciate sana mchango wake kwenye maisha yangu.
I am trying my best level to make him proud of me hata kama ni mtoto wa nje, ila he do not appreciate chochote kutoka kwangu, ila ni makosa tu ndio huwa yanaonekana, moyo wangu umekuwa mzito sana kwake.
Imefika mpaka mahali najiona kuwa mimi ni kama mkimbizi fulani, nyumbani hapakaliki hata kwa siku moja, inaniumiza nikiona baba anaelewana na mwanae, ila mimi baba yangu ndio hivyo.
Wajuvi naombeni ushauri wenu niondokane vipi na hali hii, najua humu kuna watu wananizidi umri wameshaona mengi.
Shukrani.
Sasa we mvumilie tu kuna siku tataisha na atakuthamini na kukuomba msamaha. Mtendee hisani yake kama mlezi wala usimchukie ILA jaribu kumuepuka pindi akiwa na hasira