Mgogoro wa kisaikolojia na baba

Mgogoro wa kisaikolojia na baba

Promethazine

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2017
Posts
262
Reaction score
260
Salam za asubuhi wakuu.

Kwanza let me declare my interest kuwa simchukii baba yangu.

Bila kupoteza muda leo nimeona nilitoe tatizo langu hili wanasema mficha maradhi kifo humuumbua.

Mimi ni mtoto wa kiume kwenye familia ya watoto wanne, mimi ndio wa kwanza, watatu waliobaki ni wa kike. Basi katika ukuaji kulikua na tabia ya baba kuwa mkali sana endapo nikikosea jambo nitapigwa fimbo, ngumi za kutosha na maneno makali sana ya kila namna, ambayo yalikuwa yakiingia moyoni kabisa na kujeruhi hisia, nilijipa moyo kuwa huenda ni kwa sababu mimi ni wa kwanza natakiwa niwe mfano.

Ilifika siku baba ametoka safarini usiku, tulichelewa kwenda kumpokea mizigo, kwa maana wakati bodaboda inapiga honi hatukusikia, vile natoka tu kwenda kumpokea nilikutana nae akatua mizigo hapo hapo akaanza kunishushia kipigo hapo hapo, rungu kumbe alikuwa amekuja nazo, nilipigwa magoti mpaka nikashindwa kuamka, alipomaliza akahamishia kipigo kwa mama.

Basi mdogo wangu wa kike akamuandalia chakula akala, baada ya kula akaanza kutukana, alipomaliza kutukana akanitemea mate akaenda kulala[emoji26] .

Nikaendelea na shule hivyohivyo, hatimaye nikapata nafasi ya kujiunga chuo nikawa nimefanikiwa kutoka nyumbani bado mahusiano na baba yakiwa sio mazuri.

Nikipata likizo kwenda nyumbani, mambo ni yaleyale, mpaka ninapoandika sasa hivi nikiwa mtu mzima mzee wangu kauli ya kistaarabu kwangu hana nikikosea kidogo ananidhalilisha, nyumbani kwao yaani kwa bibi na babu ameshanisema sana kuwa mimi sio mtoto mzuri, wakati juhudi zangu zinaonekana kama ni elimu nimejitahidi sana kuipata, now ni msaada kwa wadogo zangu, lolote nitakalofanya kwa mzee ni baya.

Namheshimu sana mzee maana amenihangaikia sana mpaka hapa nilipo, nimejitahidi to make him proud in all means lakini kila ninalofanya inaonekana si lolote si chochote [emoji17] . Nimejitahidi sana kufanya jitihada za kuondoa kero yoyote kwa mzee, huenda ndiyo maana anakasirika Ila bado tu, uso wake unaonekana una chuki. Nikaamua nikae mbali tu maana jitihada zangu zimefail, yaani hata nyumbani huwa naenda akiwa hayupo!

Matukio ni mengi sana kama hayo , wakati mwingine kosa ni dogo tu maneno machafu kabisa nimejaribu kufupisha tu.

Basi waungwana wanasema "Time tells!" . Siku zimekwenda nimekuja kugundua kuwa mimi ni mtoto wa nje! Je nimegunduaje?

Baada ya kuwa mtu mzima na kuona kwamba hali hii si ya kawaida ikabidi nimuulize mama mbona hivi? Mbona mzee anaonesha upendeleo wazi wazi, chuki zisizoisha na maneno machafu? Mpaka leo hii ni salamu tu.

Basi mama akanikalisha chini, akanipa ukweli halisi wa mambo kuwa baba yako yupo mwingine hata yeye anajua kabisa, mama alinionesha na nikiri nilipomuona nilijua huyu ndiye baba yangu mzazi tumefanana sana, akaniambia wala usishangae na mambo yanayoendelea, kubali endelea na maisha mengine.

Let me declare my interest kuwa simchukii mzee wangu ila moyo wangu hauna upendo naye, naappreciate sana mchango wake kwenye maisha yangu.

I am trying my best level to make him proud of me hata kama ni mtoto wa nje, ila he do not appreciate chochote kutoka kwangu, ila ni makosa tu ndio huwa yanaonekana, moyo wangu umekuwa mzito sana kwake.

Imefika mpaka mahali najiona kuwa mimi ni kama mkimbizi fulani, nyumbani hapakaliki hata kwa siku moja, inaniumiza nikiona baba anaelewana na mwanae, ila mimi baba yangu ndio hivyo.

Wajuvi naombeni ushauri wenu niondokane vipi na hali hii, najua humu kuna watu wananizidi umri wameshaona mengi.

Shukrani.
 
1) Katika maisha yako, don't ever try to make a human being proud! Make God proud and by doing so, he who knows God will be proud, he who doesn't know God did not deserve it in the first palce. Ishi maisha kama Mungu wako anavyotaka na utashangaa vile maisha yako yatakavyokua na maana.

2) Wengine tumechapwa sana na wazazi wetu. Ndo wazee wa Tanzania walivyo. Maadam aliweka paa juu ya kichwa chako, uliishi ukijua una baba, alikupa mavazi, chakula na mengine mengi. Heshima yake ya baba ibaki palepale, we samehe madhaifu yake but never doubt that he is your father (Ukifanya hivyo hata Mungu hatapenda).
Baba yako aliyekuzaa maadam hakukuclaim as a man should do. Mheshimu maana ndo geneology yako ila anayeumba binadamu ni Mungu so usimtelekeze aliyekulea.

3) Support your family ila tengeneza umbali na baba yako ili asikuumize. Just penda mama na dada zako waje kukutembelea na usiende kwenu often. Ukienda usimsumbue just msalimie mpe zawadi zake ondoka.
 
Pole sana mkuu ila kama umeshaondoka hapo nyumbani na kuanza maisha yako basi endelea maana sababu umeshaijua na huwezi kubadilisha kilichotokea. Kama umeshapata uwezo wa kifedha onyesha kumjali sana kwa kumpelekea misaada na pia kumsaidia kwenye kuendesha familia yake kama kumsaidia kulipa umeme maji na pia kama ukipata vijisenti unapeleka vitu kama mpunga au mahindi ambapo yatatumika kama chakula pale nyumbani. Hivyo vitu havina gharama ila nakwambia akishaona unamjali kuliko watoto wake wa damu lazima atakuheshimu sana (ndio binadamu tulivyo kisaikolojia). Fanya haya niliyokuelekeza baadae utakuja kuni-PM matokeo yake
 
Mzee wako inaonekana alikuwa anakuchukia Sana kwa sababu wewe Si mwanae bila wewe kujua. Kikubwa umeshaujua ukweli achana nae. Fanya maisha yako msaidie mama Na wasaidie wadogo zako kwa hali Na mali Ili kumproove wrong Hilo lizee. Na ikibidi msaidie Tu kwa hiari huyo baba ako wala isiwe lazima. Kwa ajili zangu Mimi iko siku ningemlia timing ningemchana live akijifanya bado msela ana nguvu namtandika mangumi.
 
Salam za asubuhi wakuu.

Kwanza let me declare my interest kuwa simchukii baba yangu.

Bila kupoteza muda leo nimeona nilitoe tatizo langu hili wanasema mficha maradhi kifo humuumbua.

Mimi ni mtoto wa kiume kwenye familia ya watoto wanne, mimi ndio wa kwanza, watatu waliobaki ni wa kike. Basi katika ukuaji kulikua na tabia ya baba kuwa mkali sana endapo nikikosea jambo nitapigwa fimbo, ngumi za kutosha na maneno makali sana ya kila namna, ambayo yalikuwa yakiingia moyoni kabisa na kujeruhi hisia, nilijipa moyo kuwa huenda ni kwa sababu mimi ni wa kwanza natakiwa niwe mfano.

Ilifika siku baba ametoka safarini usiku, tulichelewa kwenda kumpokea mizigo, kwa maana wakati bodaboda inapiga honi hatukusikia, vile natoka tu kwenda kumpokea nilikutana nae akatua mizigo hapo hapo akaanza kunishushia kipigo hapo hapo, rungu kumbe alikuwa amekuja nazo, nilipigwa magoti mpaka nikashindwa kuamka, alipomaliza akahamishia kipigo kwa mama.

Basi mdogo wangu wa kike akamuandalia chakula akala, baada ya kula akaanza kutukana, alipomaliza kutukana akanitemea mate akaenda kulala[emoji26] .

Nikaendelea na shule hivyohivyo, hatimaye nikapata nafasi ya kujiunga chuo nikawa nimefanikiwa kutoka nyumbani bado mahusiano na baba yakiwa sio mazuri.

Nikipata likizo kwenda nyumbani, mambo ni yaleyale, mpaka ninapoandika sasa hivi nikiwa mtu mzima mzee wangu kauli ya kistaarabu kwangu hana nikikosea kidogo ananidhalilisha, nyumbani kwao yaani kwa bibi na babu ameshanisema sana kuwa mimi sio mtoto mzuri, wakati juhudi zangu zinaonekana kama ni elimu nimejitahidi sana kuipata, now ni msaada kwa wadogo zangu, lolote nitakalofanya kwa mzee ni baya.

Namheshimu sana mzee maana amenihangaikia sana mpaka hapa nilipo, nimejitahidi to make him proud in all means lakini kila ninalofanya inaonekana si lolote si chochote [emoji17] . Nimejitahidi sana kufanya jitihada za kuondoa kero yoyote kwa mzee, huenda ndiyo maana anakasirika Ila bado tu, uso wake unaonekana una chuki. Nikaamua nikae mbali tu maana jitihada zangu zimefail, yaani hata nyumbani huwa naenda akiwa hayupo!

Matukio ni mengi sana kama hayo , wakati mwingine kosa ni dogo tu maneno machafu kabisa nimejaribu kufupisha tu.

Basi waungwana wanasema "Time tells!" . Siku zimekwenda nimekuja kugundua kuwa mimi ni mtoto wa nje! Je nimegunduaje?

Baada ya kuwa mtu mzima na kuona kwamba hali hii si ya kawaida ikabidi nimuulize mama mbona hivi? Mbona mzee anaonesha upendeleo wazi wazi, chuki zisizoisha na maneno machafu? Mpaka leo hii ni salamu tu.

Basi mama akanikalisha chini, akanipa ukweli halisi wa mambo kuwa baba yako yupo mwingine hata yeye anajua kabisa, mama alinionesha na nikiri nilipomuona nilijua huyu ndiye baba yangu mzazi tumefanana sana, akaniambia wala usishangae na mambo yanayoendelea, kubali endelea na maisha mengine.

Let me declare my interest kuwa simchukii mzee wangu ila moyo wangu hauna upendo naye, naappreciate sana mchango wake kwenye maisha yangu.

I am trying my best level to make him proud of me hata kama ni mtoto wa nje, ila he do not appreciate chochote kutoka kwangu, ila ni makosa tu ndio huwa yanaonekana, moyo wangu umekuwa mzito sana kwake.

Imefika mpaka mahali najiona kuwa mimi ni kama mkimbizi fulani, nyumbani hapakaliki hata kwa siku moja, inaniumiza nikiona baba anaelewana na mwanae, ila mimi baba yangu ndio hivyo.

Wajuvi naombeni ushauri wenu niondokane vipi na hali hii, najua humu kuna watu wananizidi umri wameshaona mengi.

Shukrani.
Kijana hata kabla sijafika huko kujigundua kuwa umtoto wa nje nilikuwa nimeshajua kuwa wewe siyo shahawa ya huyo mzee na akikuona anakuchukia sana kikubwa ongea na baba yako mzazi uhamie kwake acha kumuumiza baba lez kwa kuendelea kuwepo hapo..
 
Kingine muombe sana Mungu huo mkosi husijetokea kwako na kwa mkeo hapo baadae. Mwenye makosa hapo ni mama yako na wala si baba yako. Mama yako alifanya kosa ambalo ni gumu sana kusameheka (ukikuwa utaelewa kwa nn baba yako aliwachukia wewe na mama yako). Kwa kukulea na kukusomesha mpk chuo kikuu nakwambia huyo baba amefanya jambo ambalo 90% ya wanaume hawawezi kulifanya. Hayo mapungufu mengine yapotezee ushakuwa mkubwa ni changamoto tu zilikutokea ila hii nakupa kama tip " alichomfanyia mama yako huyo mzee wako ukija kufanyiwa na wewe na mkeo ukija kuoa ndio utaelewa jinsi huyo mzee wako alivyona moyo wa kusamehe"
 
1) Katika maisha yako, don't ever try to make a human being proud! Make God proud and by doing so, he who knows God will be proud, he who doesn't know God did not deserve it in the first palce. Ishi maisha kama Mungu wako anavyotaka na utashangaa vile maisha yako yatakavyokua na maana.

2) Wengine tumechapwa sana na wazazi wetu. Ndo wazee wa Tanzania walivyo. Maadam aliweka paa juu ya kichwa chako, uliishi ukijua una baba, alikupa mavazi, chakula na mengine mengi. Heshima yake ya baba ibaki palepale, we samehe madhaifu yake but never doubt that he is your father (Ukifanya hivyo hata Mungu hatapenda).
Baba yako aliyekuzaa maadam hakukuclaim as a man should do. Mheshimu maana ndo geneology yako ila anayeumba binadamu ni Mungu so usimtelekeze aliyekulea.

3) Support your family ila tengeneza umbali na baba yako ili asikuumize. Just penda mama na dada zako waje kukutembelea na usiende kwenu often. Ukienda usimsumbue just msalimie mpe zawadi zake ondoka.
Asante sana kwa ushauri mzuri.
 
Achana naye, usimpe muda wa kuonana naye, msaidie chochote unachoweza kumsaidia ukiwa mbali.

Jenga uhusiano mzuri na wadogo zako na mama yako, ikibidi kaa na wadogo zako waeleze hilo swala ila wahakikishie kwamba undugu wenu ni mkubwa na baba hawezi kuutenganisha.

Kama amekusomesha na umeweza kujitegemea ni swala la kumshukuru Mungu, endelea kumpa heshima yake na usimwambie lolote juu ya wewe kujua kwa nini anakuchukia.

NOTE: Akili za kuambiwa changanya na zako pia.
 
Mzee wako inaonekana alikuwa anakuchukia Sana kwa sababu wewe Si mwanae bila wewe kujua. Kikubwa umeshaujua ukweli achana nae. Fanya maisha yako msaidie mama Na wasaidie wadogo zako kwa hali Na mali Ili kumproove wrong Hilo lizee. Na ikibidi msaidie Tu kwa hiari huyo baba ako wala isiwe lazima. Kwa ajili zangu Mimi iko siku ningemlia timing ningemchana live akijifanya bado msela ana nguvu namtandika mangumi.
Mkuu kwa nini Umeamua Kutumia neno ...Lizeeee
 
Heri ushamjua baba yako halisi shukuru, sio unahangaika kumtafta siku unampata mara paaaaap baba ni lemutuz na mnafanana ile mbaya, hahaaaaa my friend utajuta kudadisi
 
Hapo wakulaumiwa ni mama aliyechepuka (cause) hayo yanayokupata ni effect (matokeo ) tu ambayo huyo baba yako mlezi ni reactions zake kama binadamu wengine tu ambao amesingiziwa mtoto, kuanzia hapo solution ndio unaweza ukupata
 
Back
Top Bottom