Mgogoro wa kisaikolojia na baba

Mgogoro wa kisaikolojia na baba

Salam za asubuhi wakuu.

Kwanza let me declare my interest kuwa simchukii baba yangu.

Bila kupoteza muda leo nimeona nilitoe tatizo langu hili wanasema mficha maradhi kifo humuumbua.

Mimi ni mtoto wa kiume kwenye familia ya watoto wanne, mimi ndio wa kwanza, watatu waliobaki ni wa kike. Basi katika ukuaji kulikua na tabia ya baba kuwa mkali sana endapo nikikosea jambo nitapigwa fimbo, ngumi za kutosha na maneno makali sana ya kila namna, ambayo yalikuwa yakiingia moyoni kabisa na kujeruhi hisia, nilijipa moyo kuwa huenda ni kwa sababu mimi ni wa kwanza natakiwa niwe mfano.

Ilifika siku baba ametoka safarini usiku, tulichelewa kwenda kumpokea mizigo, kwa maana wakati bodaboda inapiga honi hatukusikia, vile natoka tu kwenda kumpokea nilikutana nae akatua mizigo hapo hapo akaanza kunishushia kipigo hapo hapo, rungu kumbe alikuwa amekuja nazo, nilipigwa magoti mpaka nikashindwa kuamka, alipomaliza akahamishia kipigo kwa mama.

Basi mdogo wangu wa kike akamuandalia chakula akala, baada ya kula akaanza kutukana, alipomaliza kutukana akanitemea mate akaenda kulala[emoji26] .

Nikaendelea na shule hivyohivyo, hatimaye nikapata nafasi ya kujiunga chuo nikawa nimefanikiwa kutoka nyumbani bado mahusiano na baba yakiwa sio mazuri.

Nikipata likizo kwenda nyumbani, mambo ni yaleyale, mpaka ninapoandika sasa hivi nikiwa mtu mzima mzee wangu kauli ya kistaarabu kwangu hana nikikosea kidogo ananidhalilisha, nyumbani kwao yaani kwa bibi na babu ameshanisema sana kuwa mimi sio mtoto mzuri, wakati juhudi zangu zinaonekana kama ni elimu nimejitahidi sana kuipata, now ni msaada kwa wadogo zangu, lolote nitakalofanya kwa mzee ni baya.

Namheshimu sana mzee maana amenihangaikia sana mpaka hapa nilipo, nimejitahidi to make him proud in all means lakini kila ninalofanya inaonekana si lolote si chochote [emoji17] . Nimejitahidi sana kufanya jitihada za kuondoa kero yoyote kwa mzee, huenda ndiyo maana anakasirika Ila bado tu, uso wake unaonekana una chuki. Nikaamua nikae mbali tu maana jitihada zangu zimefail, yaani hata nyumbani huwa naenda akiwa hayupo!

Matukio ni mengi sana kama hayo , wakati mwingine kosa ni dogo tu maneno machafu kabisa nimejaribu kufupisha tu.

Basi waungwana wanasema "Time tells!" . Siku zimekwenda nimekuja kugundua kuwa mimi ni mtoto wa nje! Je nimegunduaje?

Baada ya kuwa mtu mzima na kuona kwamba hali hii si ya kawaida ikabidi nimuulize mama mbona hivi? Mbona mzee anaonesha upendeleo wazi wazi, chuki zisizoisha na maneno machafu? Mpaka leo hii ni salamu tu.

Basi mama akanikalisha chini, akanipa ukweli halisi wa mambo kuwa baba yako yupo mwingine hata yeye anajua kabisa, mama alinionesha na nikiri nilipomuona nilijua huyu ndiye baba yangu mzazi tumefanana sana, akaniambia wala usishangae na mambo yanayoendelea, kubali endelea na maisha mengine.

Let me declare my interest kuwa simchukii mzee wangu ila moyo wangu hauna upendo naye, naappreciate sana mchango wake kwenye maisha yangu.

I am trying my best level to make him proud of me hata kama ni mtoto wa nje, ila he do not appreciate chochote kutoka kwangu, ila ni makosa tu ndio huwa yanaonekana, moyo wangu umekuwa mzito sana kwake.

Imefika mpaka mahali najiona kuwa mimi ni kama mkimbizi fulani, nyumbani hapakaliki hata kwa siku moja, inaniumiza nikiona baba anaelewana na mwanae, ila mimi baba yangu ndio hivyo.

Wajuvi naombeni ushauri wenu niondokane vipi na hali hii, najua humu kuna watu wananizidi umri wameshaona mengi.

Shukrani.
kumbe ushapajua kwenu kwann unaenda kwa watu......cha kulipa hapo we wasaidie watoto wake ambao na ww pia ndugu zako basi.....ila uanze kujifunza kwenda kwa baba yako mzazi sisi waswahili huwa hatuadopt watoto ambao hatujawakojoa....
 
Saidia ndugu zako, ila huyo Mzee wako uloonyeshwa usimfatilie kwani hajakulea pia huna mapenzi nae,Fanya mambo yako maisha yatasonga, ukizidi kumfatilia huyo baba yako mzazi italeta mgogoro kati ya baba yako mlezi pia baba yako mzazi kwa upande Wa mke wake, hivyo wew jiweke mbali kwani tayali ilishatokea huna sababbu ya kuumiza kichwa
 
Njia bora ni kumwepuka huyu baba yako...mchunie!
Mwache hadi akutafute mwenyewe....
Akigundua anapoteza mtu wa kumsaidia uzeeni atarudi! Acha muda uamue!
Usijaribu kutaka kumfurahisha..
 
Pole sana ndugu usisononeke sana mshukuru Mungu kwa kila jambo, jitahidi kuchukulia kama mambo ya kawaida.
 
Kukimbia tatizo sio kusolve Tatizo... Ukisema ukae mbali nae au uende home pindi akiwa hayupo ndo unazidi kumwaminisha kuwa hana faida kwako na hakuwa wrong kukufanyia hvyo...
Solution :
Jitie ukauzu... Muite uongee nae faragha ukiwa Wewe na mama yako na yeye tu.. Kisha umwambie kuwa ushaijua sababu ya yeye kukufanyia hvyo na kukuchukia kwake hakubadilishi ukweli kuwa ww sio mwanae... Ila Kama uwepo wako mbele ya macho yake ni kero kwake Basi umuahidi kuwa huto-appear tena...
Umesema mama yako kakwambia kuwa baba yako anajua kuwa ww sio mwanae.. Hvyo hata ukisema umwambie hawatogombana...
Nadhan itasaidia... Na ataona aibu kuwa umejua kuwa anakuchukia Japo mwenye Kosa sio Wewe Bali ni mama yako
 
Hakuna haja ya kuendelea kuumiza kichwa,tafuta maisha yako tu,ww ni mwanaume
 
Back
Top Bottom