Elections 2010 Mgaya wa TUCTA kugombea Muheza?

Kwa akili ya watanzania nitakubaliana na wewe lakini katika nchi nyingi mgomo ni haki ya mfanyakazi uwe unamsukumo wa kisiasa, upinzani au chochote kile, kinachotafutwa ni maslahi mazuri ya mfanyakazi haijalishi yameletwa na nani. Hata TANU ilitumia vyama vya wafanyakazi kufanikisha matakwa yake kama TAA, NUTA nk. Mimi nafikiri wafanyakazi hawana akili ndogo kiasi hicho kudhani kwa vile madai yao yanamsukumo wa siasa za upinzani basi wasidai tena au ndiyo sababu ya kumpa kura JK.

Luteni,

Labda kama unaongea kiushabiki lakini hili jambo linatendeka dunia nzima na wala sio kwa akili ya Watanzania tu.

Nikupe mfano mmoja, UK kuna general alikuwa mkuu wa majeshi anaitwa general Sir Richard Dannat, jamaa alikuwa mtetezi mzuri sana wa maslahi ya wanajeshi na aliibana kweli serikali kuhusu vifaa jeshini. Opposition party wakati huo ni hao Tories walikuwa mara nyingi wanatumia comments zake ambazo zilikuwa genuine kuilima serikali ya Labour. Alipomaliza muda wake tu wa kazi akaamua kuwa mshauri wa Tories. Ilileta kasheshe kubwa na mambo yake yote mazuri aliyokuwa anafanya kwa niaba ya wanajeshi ikaonekana yalikuwa politically motivated.

Hata wanajeshi wengi wakaanza kumkana maana hawakutaka kwa njia yoyote ile jeshi litumike kufikisha ambitions za watu kisiasa.

Hili halina tofauti na la Mgaya. Kama ingelikuwa ni kweli basi ingelikuwa ni move mbaya sana kwake na kwa wafanyakazi. Ingebidi wafanyakazi wamkane. Hakuna kitu kibaya kwenye madai ya wafanyakazi kama kuonekana kuna siasa ndani yake. Serikali yoyote ikiona hivyo inakumaliza.

Thather alivimaliza vyama vya wafanyakazi UK kwasababu hiyo hiyo, vilikuwa vinatumiwa na Labour kwenye malengo ya kisiasa. Wananchi walipoona hivyo wakawa upande wa Thatcher alipoamua kula sahani moja na hivyo vyama na ndio ukawa mwisho wa vyama vya wafanyakazi vyenye nguvu kwa hapa UK.
 
Mgaya wa TUCTA ahusishwa na siasa
Imeandikwa na Na Waandishi Wetu, Dar, Muheza; Habarileo





KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya, amehusishwa na siasa, akitajwa kuwa ‘lulu' ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ubunge katika Jimbo la Muheza mkoani Tanga.

Mgaya ametajwa kuwa mtu jasiri, shupavu na mtetezi wa haki katika vipeperushi vilivyotawanywa juzi katika mji wa Muheza; alikozaliwa kiongozi huyo wa wafanyakazi ambaye katika siku za karibuni, jina lake limetawala vyombo vya habari.

Hata hivyo, Mgaya licha ya kukiri kufahamu kuhusu kusambazwa kwa vipeperushi hivyo mjini humo siku chache tangu afike kwa mapumziko ya mwishoni mwa wiki iliyopita, ameviruka na kueleza kwamba hana mpango na siasa kwa sasa.

Kipeperushi hicho kina maneno yanayosomeka: "Nicholaus Mgaya: Mbunge aliyesubiriwa, nuru mpya ya Muheza…Mgaya ni jasiri, Mgaya ni shupavu, Mgaya ni mtetezi wa haki, Mgaya ni mwanamageuzi, Mgaya ni mwana maendeleo, Mgaya ni lulu ya Chadema, mpatie kura yako Oktoba,"

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Mgaya alikiri kuwa juzi alasiri alipigiwa simu na mmoja wa jamaa zake wa Muheza na kufahamishwa kuwa kuna vipeperushi vimesambazwa vikiwa na jina lake na kumtaja kuhusishwa na ubunge.

"Ni kweli hata mimi nimesikia habari hizo…nilipigiwa simu na jamaa yangu (anamtaja jina) na akanieleza kuhusu vipeperushi hivyo. Nikamwomba anitumie kwa fax (nukushi) na kweli saa 9.40 jana (juzi), akanitumia…

"Kwa kweli sivijui vipeperushi hivyo, na kwanza sihusiki navyo kwa sababu mimi si Nicholaus, mimi ni Nicholas Mgaya," alisema Mgaya na kuongeza: "Lakini hata hivyo, ukiacha hayo, mimi pia si mwanachama wa Chadema, hivyo ubunge kupitia Chadema utatoka wapi? Lakini pia nina sababu tatu za msingi za kupuuza vipeperushi hivyo."

Alijitambulisha kuwa mwanachama wa CCM tawi la Mchafukoge katika kata ya Mchafukoge, wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Mzaliwa huyo wa kijiji cha Magila kilometa chache kutoka Muheza Mjini, alizitaja sababu hizo kuwa ni kutokuwa mwanachama wa Chadema; kutoamua kujitumbukiza katika siasa na kwamba hawezi kumpinga mbunge wa sasa wa Muheza, Herbert Mntangi kwa kuwa ni ndugu yake.

"Sababu hizo tatu zinanifanya nisihusike na vipeperushi hivyo. Ni kweli nilikuwa Tanga mwishoni mwa wiki. Nilikwenda Jumamosi, nikalala Tanga Mjini, Jumapili nikaenda kijijini, jioni nikapanda basi kurudi Dar," alisema Mgaya jana na kueleza kuwa anaamini vipeperushi hivyo vilisambazwa baada ya kuondoka mjini humo.

Alisema kwa sasa hakusudii kuingia kwenye siasa wala kuwania ubunge si Muheza tu, bali katika jimbo lolote nchini, kwa sababu malengo yake ni kuendelea kuwa mtetezi wa wafanyakazi na kwamba ana kazi ambazo amezianza Tucta na angependa kuona zinakamilika katika uongozi wake.

"Mpango wa siasa mimi sina … nina malengo ya kuendelea kuwatumikia wafanyakazi, sina wazo kabisa la siasa. Ninataka kuendelea kuwatumikia wafanyakazi na kukamilisha kazi mbalimbali ambazo nimezianza," alisema Mgaya anayekaimu nafasi ya Katibu Mkuu baada ya kusimamishwa kwa aliyekuwa akiishikilia, Nestory Ngulla.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Tucta amekuwa akivuma katika vyombo vya habari tangu mwezi uliopita, baada ya shirikisho hilo kutangaza kusudio la mgomo wa wafanyakazi nchi nzima Mei 5, mwaka huu; lakini ulishindwa kufanyika.

Baada ya kusudio hilo umekuwapo mvutano mkubwa kati ya Tucta na Serikali; kiasi cha kumlazimu Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati na kutoa hotuba kali akieleza kuwa madai ya Tucta hayatekelezeki na kuwaonya wafanyakazi wasigome.

Aidha, alisema hajui Mgaya ana ajenda gani kwa sababu yamekuwapo mazungumzo na Serikali, lakini mara kadhaa viongozi wa Tucta wamekuwa wakieleza tofauti na yanayokubaliwa katika vikao; hivyo kuwadanganya wafanyakazi.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, hakupatikana, lakini Mkurugenzi wa Vijana wa Taifa wa chama hicho, John Mnyika, alielekeza atafutwe Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Tanga, Benson Mramba, ambaye alisema:

"Tumeshtushwa na hiyo taarifa, kwa sababu hatuna mawasiliano naye ya aina yoyote… mimi nilipigiwa simu na viongozi wa Chadema wa wilaya ya Muheza, wakidhani huyu jamaa amepitia mkoani hapa moja kwa moja.

"Tukapata mshituko na kutaka kuthibitisha na makao makuu nao wakasema hawana taarifa wala mawasiliano naye, lakini kama Mtanzania na mwananchi wa kawaida, anakaribishwa (Chadema) kama atafuata taratibu kwani ni haki yake ya msingi na ya kikatiba."

Lakini juhudi za HABARILEO za kumpata mbunge wa sasa wa Muheza, Mntangi hazikuzaa matunda licha ya kumtafuta kupitia simu zake mbili za mkononi.

Naye Oscar Mbuza, anaripoti kuwa Tucta imesema iko mbioni kumfikisha Mahakama ya Kazi, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, kwa madai ya kukiuka sheria alipotangaza kima cha chini cha mishahara ya sekta binafsi Aprili 30 mwaka huu.

Mgaya alisema Dar es Salaam jana, kuwa Waziri Kapuya hakufuata taratibu za kisheria alipotangaza mishahara hiyo kupitia Notisi ya Serikali (GN) namba 172, iliyofuta GN 223 ya mwaka 2007.

Alisema kima cha chini kilichotangazwa na Waziri Kapuya na ambacho kimepelekwa kwenye Baraza la Uchumi, Ajira na Ushauri (LESCO), hakikutokana na mapendekezo ya Bodi za Mishahara za Kisekta kama ilivyoelezwa, kwani bodi hizo hazijakaa tangu mwaka 2007.

Alisema taarifa iliyopelekwa Lesco ni ya mapendekezo ya Mtafiti Mwelekezi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuyapeleka Lesco ni kinyume cha Sheria namba 7 ya mwaka 2004.

Alisema upungufu uliojitokeza katika tangazo hilo la Waziri Kapuya ni kushushwa kwa viwango vya mishahara vya kima cha chini ambavyo viliwekwa na GN 223 bila kuzingatia mfumuko wa bei, kuanguka kwa thamani ya sarafu na uwezo wa mfanyakazi kuishi.

Aliongeza kuwa badala ya kupandisha kima cha chini cha mshahara, GN 172 imeshusha viwango hivyo ambavyo awali vilikuwa vimepandishwa kupitia tangazo la GN 223 la Waziri John Chiligati akiwa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana wakati huo.
 
Agombee uraisi sisi wafanyakazi tutampa kura zetu! Ubunge ni nafasi ndogo sana kwake huyu mpiganaji
 
Mgaya wa TUCTA ahusishwa na siasa
Imeandikwa na Na Waandishi Wetu, Dar, Muheza; Habarileo





KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya, amehusishwa na siasa, akitajwa kuwa ‘lulu' ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ubunge katika Jimbo la Muheza mkoani Tanga.

Mgaya ametajwa kuwa mtu jasiri, shupavu na mtetezi wa haki katika vipeperushi vilivyotawanywa juzi katika mji wa Muheza; alikozaliwa kiongozi huyo wa wafanyakazi ambaye katika siku za karibuni, jina lake limetawala vyombo vya habari.


Underlined hii habari ya kupikwa
 
"Kwa kweli sivijui vipeperushi hivyo, na kwanza sihusiki navyo kwa sababu mimi si Nicholaus, mimi ni Nicholas Mgaya," alisema Mgaya.

Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Tanga, Benson Mramba, ambaye alisema:

"Tumeshtushwa na hiyo taarifa, kwa sababu hatuna mawasiliano naye ya aina yoyote… mimi nilipigiwa simu na viongozi wa Chadema wa wilaya ya Muheza, wakidhani huyu jamaa amepitia mkoani hapa moja kwa moja.

"Tukapata mshituko na kutaka kuthibitisha na makao makuu nao wakasema hawana taarifa wala mawasiliano naye, lakini kama Mtanzania na mwananchi wa kawaida, anakaribishwa (Chadema) kama atafuata taratibu kwani ni haki yake ya msingi na ya kikatiba."

Naona huu ni mpango wa CCM ili ionekane kuwa jamaa aliitisha mgomo kutafuta mtaji wa kisiasa, na pengine maneno ya mkuu wa kaya yapate back up...lakini wamechemsha Watanzania sio wajinga tena..!! Hatudanganyikii...!
 
Mwanakiji.......tuweke sawa kidogo hapa: Yusuph Mgaya na Nicholous Mgaya ni mtu mmoja??????????????????
 
Yusuph Mgaya na Nicholas P Mgaya ni watu tofauti kabisa.
Mimi ninamfahamu nd. Mgaya ni mtu mwenye msimamo thabiti na vigumu kutumiwa na mtu au chama chcchote cha siasa.
Kama alivyosema mwenyewe siasa kwa sasa haipo kabisa kwenye malengo yake.
 
Kule Muheza mmojawapo wa watu wenye kutaka kugombea kule ni Balozi Andrew Daraja na Mbunge wa sasa Herbert Mntangi. Lakini siku chache zilizopita (kuanzia hii tarehe 19 Mei) kuna tetesi kuwa Katibu wa TUCTA Yusuph Mgaya ambaye alijiwa juu na Rais Kikwete anampango wa kupeleka mapambano yake ya wafanyakazi ndani ya Bunge kwa kugombea huko Muheza kwa tiketi ya Chadema. Kuna vipeperushi inadaiwa vimeenezwa vikimwaga sifa zake huko na wenye nchi yao wanashtuka.

Hata hivyo, kwa sasa Bw. Mgaya hajakiri moja kwa moja kuwa kweli anataka kugombea zaidi ya watu wengine kuwa na wasiwasi huo kwa sababu tu alienda kusalimia nyumbani kwao na kuondoka mapema na hivyo tetesi hizi kuanza.

Stay tuned.

Mwanakijiji huyu underlined ndo Nicholas Mgaya naomba utuweke sawa
 
"Kwa kweli sivijui vipeperushi hivyo, na kwanza sihusiki navyo kwa sababu mimi si Nicholaus, mimi ni Nicholas Mgaya," Mgaya

Hapa inaonekana kuna watu watatu:-

1. Kuna huyu Yusuph Mgaya - kwa mujibu wa Mwanakijiji.
2. Kuna Nicholaus Mgaya - kwa mujibu wa vipeperushi.
3. Kuna Nicholas Mgaya - wa TUCTA
.

Sa sijui yupi ni yupi..?
 
Maeneo tofauti
Sio kilakitu kina apply, hizi fikra zako pia nafikiri ndo zinaturudisha nyuma
Mi nadhani fikra zako ndizo zinaturudisha nyuma. Jamaa kakujibu kwa reference sasa nani ana fikra zinazopiga reverse?
 
Si kweli amekanusha,kwa cha chake ni ccm nasio chadema tena ni mlipa ada mzuri pale mchafukoge tawini
 
Back
Top Bottom