pumbatupu
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 256
- 82
Hivi haya maisha tunayapeleka wapi?...ndivyo tulivyoamua..haya ngoja twende tuone kama tutafika..
''Mgawo wa umeme wafikia saa 18 kwa siku
Monday, 25 July 2011 09:32
Daniel Mjema
MAKALI ya mgawo wa umeme, yanazidi kuitikisa nchi huku mgawo huo ukiongezeka kutoka saa nane hadi kufikia saa 18 kwa siku.
Wakati hayo yakitokea, habari zinasema mitambo ya kuzalisha umeme katika Bwawa la Mtera, huenda ikazimwa wakati wowote kuanzia sasa baada ya kina cha maji kufikia kiwango cha mwisho cha uzalishaji umeme.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa kwa baadhi ya maeneo ya nchi, umeme umekuwa ukiwaka kwa saa sita tu saa zingine 18 mikoa hiyo inabaki gizani yakiwa ni matokeo ya makali ya mgawo huo.
Habari kutoka katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, zilisema umeme umekuwa ukikatwa saa 6:00 usiku na kurejeshwa saa 12 jioni siku inayofuata huku baadhi ya maeneo yakiwa hana umeme ka siku nzima.
Habari kutoka mjini Tabora na Morogoro zilisema makali ya mgawo wa umeme yana unafuu ikilinganishwa na Mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam na Arusha.
Baadhi ya wananchi katika mikoa hiyo wamedai kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco, wanaohusika na kukataji na urejeshaji wa umeme, wanafanyakazi hiyo kwa upandeleo wa maeneo.
Ofisa mmoja mwandamizi wa Tanesco, aliliambia Mwananchi kuwa hali ya uzalishaji umeme nchini ni mbaya na kwamba kama hatua za haraka hazitachukuliwa, nchi itaingia gizani.
Tulikuwa tunaongea na wenzetu kule Mtera wanasema kama hali itaendelea kama ilivyo sasa, watakuwa hawana jinsi zaidi ya kuzima mitambo .kina cha maji kimefikia kiwango cha dharura,alisema.
Ohuyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema kwa hali ilivyo, mgawo wa umeme unafikia hadi saa 18 ingawa uongozi wa Tanesco, umeamua kulifanya kuwa ni jambo la siri kubwa.
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alikiri kuwa ratiba iliyotolewa awali na shirika hilo sasa haifuatwi na kwamba mgawo umekuwa ukiongezeka na kupungua.
Ile ratiba hatuwezi kuifuata tena kwa sababu wanaotuuzia umeme ndio wanatuambia leo punguzeni megawati kiasi fulani baada ya muda wanakuambia tena punguzeni, kwa hiyo tatizo liko hapo,alisema.
Hatuwezi kuwatangazia wananchi kila mara kwamba sasa mgawo utakuwa hivi au vile kwa sababu hilo linategemea Pan African mimi nafikiri itakuwa vizuri kama mtawauliza wao kwamba tatizo ni nini,alisisitiza.
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanabashiri uchumi wa Tanzania kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa kuwa kwa hali ilivyo, serikali haiwezi kuwadai kodi wafanyabiashara ambao kimsingi hawazalishi chochote.
Hivi karibuni Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mgawo wa umeme, unapungua kwa kiasi kikubwa ifikapo Desemba mwaka huu, watakapozalisha megawati 300.
Hata hivyo wabunge na wananchi wamekuwa wakiitupia lawama serikali kuwa haikuwa makini na suala la umeme tangu ilipoingia madarakani 2006 hata baada ya kuliona tatizo hilo.
Kufuatia mgao huo,wajasiriamali nchini wameziomba taasisi za fedha ambazo zimewapatia mikopo ya fedha kuwaongezea muda wa kurejesha mikopo hiyo kwa madai kutokana na mgao huo wameshindwa kuzalisha. ''
(Mwananchi)