Naomba kujulishwa wanaJF kama mgawo umeanza au kuna tatizo gani maana huku ubungo (baadhi ya maeneo) umeme umekuwa adimu wiki ya pili hii. Mfano jana umekatwa saa kumi na mbili jioni umerudi leo saa 7 mchana. Ukawaka hadi saa 9 ukakatika. Ukarudi saa 10 jioni. Saa 12 umekatika na haijulikani utarudi saa ngapi. Nijuzeni wapendwa huenda tangazo la mgawo limetolewa mie limenipita.