Mgao wa umeme wa kufa mtu watangazwa, Juni 2011 na kuendelea

Leo asubuhi kwenye kipindi cha tuongee tbc wahandisi kutoka tanesco wameutangazia umma kuwa mgao utaendelea mpaka mwisho wa mwaka na ni mgao mkubwa kuanzia saa kumi na mbili mpaka saa ishirini nanne

Wameeleza huo mgao unasababishwa na nini?
 
... Tunasisitiza tena Maisha bora kwa Kila Mtanzania. Labda turudi mezani tujiulize 'Mtanzania' ni nani? Ni wazi kuna Watanzania, na Wananchi.
Kwa hili la Umeme
Mtanzania ni muuza Jenereta. Kwa mafuta ya taa Mtanzania ni Mchakachuaji, etc.

Mtanzania ni mtu mwenye passport ya Tanzania, ambaye ana: (1) uwezo wa kung'amua 'FURSA' (2) uwezo wa kuzitumia fursa na rasilimali zilizopo (3) uwezo wa kunufaika na fursa na rasilimali hizo. ...sio mjuzi saaaana wa 'mwananchi', don't ask me.
 
Wanadai eti tatizo na kupungua kwa kani cha maji kwenye mabwawa ya uzalishaji ila tatizo ni kubwa kwani tanesco wanaonesha kukata tamaa hata zile lugha zao zenye matumaini leo hazikuepo kwani walipo ulizwa na Raheli mhando walijibu ......msema kweli mpenzi wa MUNGU mgao utaenda mpaka mwishoni mwa mwaka
 
kwa hili la Umeme Mtanzania ni muuza Jenereta. Kwa mafuta ya taa Mtanzania ni Mchakachuaji, etc.
 
kabla ya uchaguzi tulishasema huyu mtu akirudi madarakani basi...nchi itapotea.hata mwka mmoa hajamaliza
 
Hiyo ndiyo tanzania niliyoikimbia,wananchi wengi ni kama kondoo, hawatambui hata haki zao za msingi. kama ingekuwa mambo haya yanatokea huku nilipo ilitakiwa tangu 2006 rais awe ameshajiuzulu mwenyewe na waziri wake mkuu pia,cha ajabu tz bado anakula kuku na ataendelea kula kuku.kinachowafanya wananchi wote wa tanzania wasiandamane kuishinikiza serikali ijiuzulu ni kitu gani?. kuna sababu gani za kwenda bungeni wakati umeme hamna? mimi nilifikiri ktk mambo yote yanayozungumzwa bungeni hakuna lenye umuhimu kama umeme!!!!!!
 
Hii nchi inabidi tupunguzane from 40m populataion to 30M pop ndo watawala wapya watapata akili ya mtanzania mpya!!!vinginevyo hakuna kiongozi mwenye uzalendo,vitani kwanza wakuu...
 
Naona wameshindwa hata kuheshimu ratiba waliyoitoa wao wenyewe. Nilitakiwa kuwa na umeme hadi jioni ya leo lakini wamekata saa 4.45 asubuhi. Nimewapigia simu naambiwa kuna agizo toka kwa wakubwa wao kuwa wakate na hawajui itakuwa kwa muda gani.
 
Leo asubuhi kwenye kipindi cha tuongee tbc wahandisi kutoka tanesco wameutangazia umma kuwa mgao utaendelea mpaka mwisho wa mwaka na ni mgao mkubwa kuanzia saa kumi na mbili mpaka saa ishirini nanne

na mabosi wao, wa shirika, na wa wizara, wamefanya Press conference huko Dodoma asubuhi hii bna kuahidi kuwa mgawo utapungua mwezi wa nane... kweli tumeweka matapeli kuendesha mashirika yetu nyeti
 
Mkuu sidhani maana wapiga kura wengi sana hawajui hata umeme nini. Wengine hawajawahi kuona hata nguzo ya umeme.
unamaanisha kuwa ccm waliwekwa pale na jamii ambayo haijawahi kuona hata nguzo ya umeme? vipi wabunge waliotoka dsm? na majiji mengine?
 
[h=3]Mgawo wa kizembe wa umeme; serikali iwajibike[/h]

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja anapaswa kuwajibika na kutoa kauli kwa umma na bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 49 ya Bunge kuhusu mgawo mkubwa wa umeme uliotangazwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuwa utaikumbuka mikoa 18 inayopata umeme kupitia Gridi ya Taifa.

Aidha kabla ya kusubiria kutoa kauli bungeni Waziri Mkuu anapaswa kuingilia kati kwa haraka kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na TANESCO ili kuharakisha maamuzi ya kupunguza muda wa mgawo unaoendelea hivi sasa.

Hii ni kwa sababu pamoja na kupungua kwa vina vya maji katika baadhi ya mabwawa zinazoelezwa; kwa sehemu kubwa mgawo wa umeme unaoendelea hivi sasa umechangiwa na sababu za kibinadamu za kutowajibika ipasavyo kisera, kimaamuzi, kiusimamizi na kiutendaji kwa viongozi wa kiserikali kuanzia Rais, Waziri Mkuu, Waziri mwenye dhamana na watendaji wengine na hivyo kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi na kuathiri uchumi wa nchi.

Maelezo ya kwamba mgawo huu umesababishwa na mitambo ya IPTL kuzalisha MW 10 badala ya MW 100 kutokana na upungufu wa mafuta mazito (HFO) yanatosha kwa serikali kuwajibika kutokana uzembe wenye kulitia hasara taifa kwa sababu suala hili lilikuwa likijulikana kwa miezi mingi bila hatua stahili kuchukuliwa.

Mara kadhaa tumetahadharisha kwenye vikao na hadharani mara kwa mara kuhusu suala hilo lakini inaelekea kuna ombwe na kiuongozi na kimaamuzi katika serikali ambalo linaambatana na hali mbaya ya kifedha ndani ya serikali inayoongozwa na CCM kutokana na fedha nyingi za umma kutumiwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Ikumbukwe kwamba katika mkutano wa pili wa Bunge kikao cha sita tarehe 15 Februari mara baada ya kauli za Mawaziri ambapo Waziri wa Nishati na Madini alitoa kauli ya serikali kuhusu hali ya umeme nchini na utekelezaji wa miradi ya umeme katika kipindi kifupi na cha kati nilitoa hoja ya dharura kwa mujibu wa kanuni 55 (3) (e) na kanuni ya 47 ili bunge lijadili jambo la dharura la mgawo wa umeme unaolikumba taifa.

Katika ya hatua za dharura ambazo zingejadiliwa kwa kina ni ufanisi katika matumizi ya mitambo ya IPTL ikiwemo kuboresha taratibu za upatikanaji wa mafuta mazito, kuharakisha mchakato wa kupata mitambo ya MW 260; kuharakisha kukamilisha mitambo ya MW 100 Ubungo, MW 60 Mwanza, kuwezesha upatikanaji wa gesi asilia kwa ajili ya mitambo na hatua nyingine za dharura; iwapo hoja hiyo ingejadiliwa wakati huo bunge lingepitisha maazimio ya kuwezesha hatua za mapema kuchukuliwa kudhibiti mgawo mkubwa uliolikumba taifa mwezi Mei na unaoendelea kulikabili nchi hivi sasa.
Pamoja na bunge kutojadili suala hilo baadhi ya ushauri wa kurekebisha kasoro zilizoendelea ulitolewa kwa serikali kupitia kamati ya nishati na madini mwezi Februari 2011 hata hivyo kuna mwelekeo wa kutokuwa na uongozi thabiti katika serikali wa kukabiliana na tatizo la mgawo mkubwa wa umeme.

Tarehe 2 Aprili 2011 nilitoa kauli ya kuitaka serikali ieleze maandalizi ambayo yamekwishafanyika mpaka hivi sasa kukabiliana na tatizo la upatikanaji, usafirishaji na uhifadhi wa mafuta mazito (HFO) ambayo yatahitajika kwa kiwango kikubwa katika kuendesha mitambo ya kufua umeme wa dharura ikiwemo IPTL na ya MW 260 kufuatia hotuba ya Rais Kikwete ya Aprili Mosi 2011 akilihutubia taifa ambayo haikuonyesha namna ambavyo serikali imejiandaa ipasavyo kukabiliana na mgawo wa umeme unaolikumba taifa.

Tarehe 22 Mei 2011 wakati taifa likikumbwa na mgawo mkubwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukarabati wa visima vya gesi asilia inayotumika kuendeshea mitambo ya umeme nilitahadharisha kwamba mgawo mwingine mkubwa zaidi unaweza kutokea iwapo hatua zaidi na za haraka hazitachukuliwa kuhusu upatikanaji wa mafuta mazito, gesi asilia na uharakishwaji wa mchakato wa kupata mitambo ya dharura ya MW 260.

Kauli zilizotolewa na Serikali baada ya kumalizika kwa ukarabati wa visima vya gesi kwamba mgawo ulikuwa umemalizika bila ya serikali kuchukua hatua za haraka kuzirekebisha kasoro tulizozieleza ililenga kutoa matumaini hewa kwa wananchi ili kuvuta muda kwa ajili ya kutoa visingizio vingine mwezi Juni kwa matatizo ambayo yalifahamika mapema.

Aidha kutokana na udhaifu wa kiutekelezaji Waziri Mkuu Pinda amekwepa katika Hotuba yake ya Bajeti ya tarehe 24 Juni 2011 kuzungumzia tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea hivi sasa badala yake ameeleza tu kwamba nishati ya uhakika itapatikana miaka michache ijayo. Hii ni kwa sababu Waziri Mkuu Pinda ameshindwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa MW 100 Ubungo na MW 60 Mwanza ambayo aliiahidi kupitia hotuba yake ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2010/2011 na mradi wa MW 200 Kiwira ambayo kama ingetekelezwa kwa wakati kuanzia ilipowekwa kwenye mipango ya serikali mwaka 2009 ingekuwa imekamilika mwanzoni mwa mwaka 2011 na hivyo taifa lisingekuwa na mgawo mkubwa wa umeme na kuingia gharama kubwa za mitambo ya kukodi kama ilivyo sasa.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kutoa majibu wakati wa majumuisho ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo kueleza kwa watanzania yeye kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni sababu za serikali kutokutekeleza kwa wakati mipango ya kulinusuru taifa kutokana upungufu wa umeme unaochangiwa na ukame hali ambayo aliifahamu tangu mwaka 2008 alipoingia madarakani. Ikumbukwe kwamba Waziri Mkuu Pinda aliingia madarakani wakati huo baada ya Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa kujiuzulu kufuatia maamuzi ya kifisadi yaliyofanywa na serikali wakati wa mgawo wa umeme kati ya mwaka 2006 mpaka 2007.

Kupitia kauli bungeni serikali ieleze ukweli kuhusu sababu za mgawo mkubwa wa umeme uliotokea mwezi Mei na unaoendelea hivi sasa na hatua ambazo serikali imechukua kwa waliosababisha hali hiyo. Aidha Serikali ieleze ukweli kwamba Waziri Ngeleja alitoa kauli potofu bungeni tarehe 15 Februari na Rais Kikwete alitoa ahadi hewa kupitia Hotuba yake kwa Taifa tarehe 1 Aprili 2011 kuhusu ukodishwaji wa mitambo ya MW 260 kwa ajili ya umeme wa dharura kuanzia mwezi Julai mwaka 2011. Serikali iwaeleze watanzania ukweli kuwa imeshindwa kutekeleza mpango huo na kueleza hatua mbadala za kurekebisha hali hiyo ili kuepusha mgawo huu ulioanza mwezi Juni kuendelea mpaka mwezi Disemba mwaka 2011 hali ambayo itakuwa ni janga kwa taifa.

Aidha serikali ieleze mikakati mahususi ya muda mfupi ya kushirikiana na sekta binafsi iweke mazingira wezeshi ya kisheria, kikanuni na kibajeti ya kuweka msingi wa utekelezaji wa miradi ya Somangafungu (MW 230), Mnazi Bay (MW 300), Kinyerezi (MW 240), maporomoko ya Ruhudji (MW 358) ili ikamilike kwa haraka zaidi kuliko ilivyopangwa hivi sasa.

Katika kauli hiyo serikali iwaeleze watanzania kupitia bunge mkakati mahususi wa kuwekeza katika kuongeza upatikanaji wa gesi asilia kwa ajili ya kuendesha mitambo hiyo ya umeme na pia kama sehemu ya mpango wa nishati mbadala yenye kupunguza gharama za maisha zinazochangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na mzigo mkubwa wa kodi ambao utaendelea hata baada ya serikali kutangaza punguzo dogo la kodi na tozo.

Kwa uchumi na usalama wa nchi serikali ya Tanzania inapaswa kufanya maamuzi mazito na kuwasilisha maombi bungeni ya kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 131 ambacho kinahitajika kama sehemu ya kuchangia asilimia 15 ya mkopo kwa ajili ya mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es salaam na baadaye hadi Tanga. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 ambayo imepitishwa serikali haijatenga kiasi hicho cha fedha hali ambayo itakwamisha utekelezaji wa mradi huo unaohitaji kati ya mwaka mmoja na miaka miwili kuweza kukamilika. Mradi huo usipotekelezwa kwa wakati ipo hatari ya baadaye ya kuwa na mitambo ya umeme ya gesi lakini ikakosekana gesi asilia ya kuiendesha na pia taifa litashindwa kutumia vizuri fursa ya kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kwa kutumia nishati mbadala ambayo inapatikana hapa nchini.

Hatua hizi zinahitaji sera sahihi, uongozi makini na taasisi thabiti zenye kuelewa kwamba sekta ya nishati ni roho ya taifa letu kwa sasa na kuchukua hatua kali dhidi ya ufisadi uliofanyika katika sekta husika, kufanya mapitio ya mikataba, kuharakisha utekelezaji wa mipango kwa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi na kwa ujumla KUWAJIBIKA. Kupungua kwa uzalishaji na kuishi gizani miaka 50 baada ya uhuru ndio mafanikio ambayo serikali inayoongozwa na CCM inataka tujivunie! Poleni wananchi, serikali inapaswa kutuomba radhi! Kambi rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA, kupitia kwa Msemaji wake Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini itaendelea kupitia Mkutano wa Nne wa Bunge kuifuatilia Serikali iliyoko madarakani kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa maslahi ya umma wa watanzania.

Wenu katika utumishi wa umma;

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
Bungeni, Dodoma-25 Juni 2011
 
tuingieni mtaani tuitoe serikali

DAWA ni kuhujumu magenereta kwenye nyumba zao binafsi tu level wao wanalipiwa mafuta na serikali kuwa na umeme wa genereta sisi tunasota na giza huku biashara zetu zikifa.

wapuuzi sana hawa usije kuta wanakula dili na wauza genereza na sasa unaweza kuta kotena limeingea
 
Mkuu sidhani maana wapiga kura wengi sana hawajui hata umeme nini. Wengine hawajawahi kuona hata nguzo ya umeme.
Ndio maana ya matabaka!!! Kuna mtabaka mengine madai yao kwa serikali yao ni more of basic needs maana umeme hawajawahi hata kuuona?
 
Back
Top Bottom