Mgao wa umeme umeanza kimya kimya Arusha

Mgao wa umeme umeanza kimya kimya Arusha

Sema taarifa hazijakufikia, sio kimya kimya.
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KATIZO LA DHARURA-TANESCO MKOA WA ARUSHA


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Arusha,linawataarifu wateja wake kuwa,Kutakuwa na matengezo ya dharura katika kituo chetu kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme Njiro kama ifuatavyo:-

Tarehe: 24/02/2021
Siku: Jumatano
Muda: 19:00 Jioni- Saa 22:00 usiku
Feeder: Industrial 3,Themi 1,Sakina na M5

Sababu Matengenezo ya dharura katika katika kituo chetu kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme Njiro ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme


Maeneo yanayoathirika Moshono,chekereni, boma siara,suye,baraa, olorieni,kokoriko, baadhi ya maeneo ya kijenge,Njiro PPF, Sunflag factory, Ngaramtoni Seliani, Ngaramtoni NMB, stand ya zamani Ngaramtoni, sokoni Ngaramtoni, Kimynaki, visima vya maji,Olkokora,mbuga nyeupe, Njiro nane nane,Njiro SDA, Chuo cha Uhasibu, ESAMI, Njiro kwa Tondi, Double B, Kikwakwaru A, Sunflug quarters, Njiro complex, Kambini, world vision, TBC,FFU ,Sekei yote, Olgilai, Ngiresi,Bangata, Midawe, Engokareti, Kwa mbotela, Songota, Olgilai kimeo, na baadhi ya maeneo ya jirani .


Ungozi unaomba radhi sana kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Kwa taarifa yoyote ya dharura tafadhali wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo:

Tanesco Arusha dawati la dharura, 0272610120 na 0758174343

Call centre: 0768985100 & 022194400

Huduma kwa wateja Arusha: 0737 894000


Imetolewa na : Ofisi ya Uhusiano na Huduma kwa wateja
TANESCO- Arusha
24/02/2021
Wangewaambia utakatika kwa siku 5 mana wadau wa arusha wanasema umekatika tarehe 24, 25, 26, 27, 28 na pengine unaweza kuendelea kukatika tu na pia kusema ni masaa mawili au moja ni UONGO ..umeme unakatika zaidi ya MASAA 12

TANESCO
 
Tafuteni taarifa, kwa tabia hii ndio nyie mkiitwa kwenye vikao vya watoto shule hamuhudhurii mpaka jumba bovu limwangukie mwanao.

As long as upo connected na Tanesco hakikisha una namba za huduma kwa wateja.
Hivi wewe unayeandika hivi upo TZ?kweli?kama upo tz na bado umeandika hivi pole!!yaani kwa tatizo la kukatika umeme TZ, uwe unapiga simu tanesco kuulizia kulikoni??utaonekana chizi!!ki ufupi kwasasa kuna tatizo la usambazaji umeme nchini!!kila sehemu ni tabu tu, halafu wao wanakwambia tuna ziada ya megawati zaidi ya 400!!
 
Back
Top Bottom