Hapo vip!!
Huku maeneo ya Ngulelo,Kimandolu sekei n.k umeme umekuwa unakatwa kuanzia saa 8 nane mchana mapaka siku inayofuatwa.
Kitu ambacho wananchi wenzangu wanalalamika ni kutopewa taarifa ili wapambane na hali ya hilisi kwasababu kuna watu wanategemea umeme kuingiza kipato.
Mfano wafanyabiashara wa samaki na nyama wanategemea umeme kuifadhi bidhaa zao zisiharibike.
Tunaomba TANESCO muache madharau..
Sema taarifa hazijakufikia, sio kimya kimya.
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KATIZO LA DHARURA-TANESCO MKOA WA ARUSHA
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Arusha,linawataarifu wateja wake kuwa,Kutakuwa na matengezo ya dharura katika kituo chetu kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme Njiro kama ifuatavyo:-
Tarehe: 24/02/2021
Siku: Jumatano
Muda: 19:00 Jioni- Saa 22:00 usiku
Feeder: Industrial 3,Themi 1,Sakina na M5
Sababu Matengenezo ya dharura katika katika kituo chetu kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme Njiro ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme
Maeneo yanayoathirika Moshono,chekereni, boma siara,suye,baraa, olorieni,kokoriko, baadhi ya maeneo ya kijenge,Njiro PPF, Sunflag factory, Ngaramtoni Seliani, Ngaramtoni NMB, stand ya zamani Ngaramtoni, sokoni Ngaramtoni, Kimynaki, visima vya maji,Olkokora,mbuga nyeupe, Njiro nane nane,Njiro SDA, Chuo cha Uhasibu, ESAMI, Njiro kwa Tondi, Double B, Kikwakwaru A, Sunflug quarters, Njiro complex, Kambini, world vision, TBC,FFU ,Sekei yote, Olgilai, Ngiresi,Bangata, Midawe, Engokareti, Kwa mbotela, Songota, Olgilai kimeo, na baadhi ya maeneo ya jirani .
Ungozi unaomba radhi sana kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Kwa taarifa yoyote ya dharura tafadhali wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo:
Tanesco Arusha dawati la dharura, 0272610120 na 0758174343
Call centre: 0768985100 & 022194400
Huduma kwa wateja Arusha: 0737 894000
Imetolewa na : Ofisi ya Uhusiano na Huduma kwa wateja
TANESCO- Arusha
24/02/2021