Mgao wa umeme: San Flag yapunguza wafanyakazi 3,000

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Tanzania tumepata pigo baada ya kiwanda cha san flag cha mjini Arusha kuamua kupunguza wafanyakazi 3,000, hii ni baada ya kuwa wanapata umeme saa 6 kwa siku huku wao wakidai mitambo yao huanza kufanyakazi ipasavyo baada ya saa 3-4 baada ya umeme kuwaka hivyo unapo wapa umeme saa sita inamaana wafanyakazi watakuwa wanafanya kazi saa 2 -3.....
View attachment 33885

wito wangu:
...Ngereja boss wako jana kaonyesha njia chondechode ifate usisubiri tukuondoe kwa nguvu

...CHADEMA maandamano lini tumngoe ngereja tunateseka watanzania
 
Oooo,maskin weee,waliopunguzwa ni elf 3,watakaoathrika ni zaid ya hao......Ngeleja hawez kujiuzuru maana alomteau mwenyewe anaifurahia hii hali
Tanzania tumepata pigo baada ya kiwanda cha san flag cha mjini Arusha kuamua kupunguza wafanyakazi 3,000, hii ni baada ya kuwa wanapata umeme saa 6 kwa siku huku wao wakidai mitambo yao huanza kufanyakazi ipasavyo baada ya saa 3-4 baada ya umeme kuwaka hivyo unapo wapa umeme saa sita inamaana wafanyakazi watakuwa wanafanya kazi saa 2 -3.....wito wangu:...Ngereja boss wako jana kaonyesha njia chondechode ifate usisubiri tukuondoe kwa nguvu...CHADEMA maandamano lini tumngoe ngereja tunateseka watanzania
 
Nilishauri kwenye uzi mwingine kuwa lile fungu nono la vitambulisho lielekezwe kwenye kutatua tatizo la umeme kwani madhara ya kutokuwa na vitambulisho vya Taifa si makubwa kama kukosekana kwa umeme. Unapozungumzia watu 3000, ukijumlisha na wategemezi wao kuna watu 18,000 watakuwa hawana uhakika wa maisha
 
Anzeni kwanza na viongozi wa Tannesco waliotoa bahasha zimejaa hela ili kuwahonga wabunge, baada ya hapo ndipo seleka lihamie kwa ngeleja.
 
Dah! Sanflag walikuwa wanaajiri vijana wengi wa Arusha, sipati picha watu watakavyotaabika na jinsi maisha yalivyomagumu. poleni wana arusha
 
Tanzania tumepata pigo baada ya kiwanda cha san flag cha mjini Arusha kuamua kupunguza wafanyakazi 3,000, hii ni baada ya kuwa wanapata umeme saa 6 kwa siku huku wao wakidai mitambo yao huanza kufanyakazi ipasavyo baada ya saa 3-4 baada ya umeme kuwaka hivyo unapo wapa umeme saa sita inamaana wafanyakazi watakuwa wanafanya kazi saa 2 -3.....

wito wangu:
...Ngereja boss wako jana kaonyesha njia chondechode ifate usisubiri tukuondoe kwa nguvu

...CHADEMA maandamano lini tumngoe ngereja tunateseka watanzania

Halafu yule Mkulo wa Hazina na Ndulu wa BoT watakwambia pamoja na matatizo makubwa sana ya umeme nchini lakini bado uchumi wetu unakuwa kwa kasi kubwa sana kati ya 6% yo 7.5% kwa mwaka!!!....sijui huwa wanazungumzia uchumi upi hasa!!! labda uchumi unaowahusu mafisadi.
 
Timua Ngeleja hivi hii nchi gani watu hamuwezi kuwawajibisha wazembe?!
 
Dah! Sanflag walikuwa wanaajiri vijana wengi wa Arusha, sipati picha watu watakavyotaabika na jinsi maisha yalivyomagumu. poleni wana arusha
siyo tu waliopunguzwa fikiria hawa watu wakiiengia mitaani kutakalika kweli...?
 
Halafu yule Mkulo wa Hazina na Ndulu wa BoT watakwambia pamoja na matatizo makubwa sana ya umeme nchini lakini bado uchumi wetu unakuwa kwa kasi kubwa sana kati ya 6% yo 7.5% kwa mwaka!!!....sijui huwa wanazungumzia uchumi upi hasa!!! labda uchumi unaowahusu mafisadi.
Sijui haya mahesabu huwa wanayapigaje...hali ni ngumu sana kwa watanzania au ni hapa Arusha tu...
 
Sunflag pamoja na A to Z wanachukua vijana wengi sana ingawa kwa kipato kidogo wanachotoa lakini inasaidia kupunguza matukio mabaya.........hali itakuwa mbaya sana Arusha vijana wakikosa ajira tutegemee ongezeko la vibaka/changudoa.......halafu huku tunakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye giza
 
Sijui haya mahesabu huwa wanayapigaje...hali ni ngumu sana kwa watanzania au ni hapa Arusha tu...

Ni Tanzania yote Mkuu lakini wasanii hawa kamwe hawatasema ukweli wa hali halisi ya uchumi wetu, wao miaka yote uchumi wetu unakuwa kati ya ya asilimia 5 mpaka 7.5% pamoja na Watanzania wengi kuelemewa kwa kiasi kikubwa na gharama kubwa za maisha na ajira kuzidi kupungua.
 
kwani aliyempatia madaraka ngeleja si alisema ngeleja asilaumiwe? Sasa sijui hizo familia za watu 3,000 zitaishije, maana hao wanategemewa na watu wengi, hebu hili swala la umeme lipatiwe ufumbuzi haraka maana sasa hivi utasikia na wengine maelfu wamepunguzwa ndio mwanzo wa kuongeza vitendo viovu.
 
Mimi navishauri vyama vyote vya upinzani kwa hili waungane kuwashinikiza hawa magamba kutatua tatizo hili la kitaifa..
 
Sunflag pamoja na A to Z wanachukua vijana wengi sana ingawa kwa kipato kidogo wanachotoa lakini inasaidia kupunguza matukio mabaya.........hali itakuwa mbaya sana Arusha vijana wakikosa ajira tutegemee ongezeko la vibaka/changudoa.......halafu huku tunakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye giza
tunachokifanya ni ujinga mtupu...nchi iko gizani kuna sehemu hapa arusha hawapati umeme saa 24 halafu siku inayofata wanakuletea umeme kwaa saa 6, huku ukiwa hauna nguvu ya kutosha kwa wale mafundi wa kuchomelea...
 
kwani aliyempatia madaraka ngeleja si alisema ngeleja asilaumiwe? Sasa sijui hizo familia za watu 3,000 zitaishije, maana hao wanategemewa na watu wengi, hebu hili swala la umeme lipatiwe ufumbuzi haraka maana sasa hivi utasikia na wengine maelfu wamepunguzwa ndio mwanzo wa kuongeza vitendo viovu.
Mkuu kuna dada zetu na kaka zetu wana saloon nao kazi haziendi na wenyewe kimsingi hawana kazi pia..yaani hali ngumu mno na mwezi mtukufuku utaanza karibuni sijui maisha yatakuwaje...
 
Timua Ngeleja hivi hii nchi gani watu hamuwezi kuwawajibisha wazembe?!
wanamsubiri ang'atuke mwenyewe siku akipenda....jamaa tangu aingie wizara hiyo hakuna cha maana alichokifanya...
 
Anzeni kwanza na viongozi wa Tannesco waliotoa bahasha zimejaa hela ili kuwahonga wabunge, baada ya hapo ndipo seleka lihamie kwa ngeleja.
Siku zote huwajibika mkuu na kwa issue ya tanesco ni waziri, kama kuna rushwa tanesco thibitisha hapa lakini kilichosikika ni rushwa wizara ya nishati, kwahiyo tyunasema Ngeleja MUST RESIGN
 
tunachokifanya ni ujinga mtupu...nchi iko gizani kuna sehemu hapa arusha hawapati umeme saa 24 halafu siku inayofata wanakuletea umeme kwaa saa 6, huku ukiwa hauna nguvu ya kutosha kwa wale mafundi wa kuchomelea...

Kinauma zaidi ni pale waziri anapodanganya mgao ni
masaa kumi mchana na usiku sita lakini sehemu nyingi ni siku nzima.
Hata rais hotuba ya mwezi wa kwanza alidanganya ikifika july tatizo litaisha..............labda limeisha kwake
 
Kwa hali hii machangu na vibaka lazima waogezeke. Hebu fikiri\: ikiwa tu kila mmoja wa hao 3000 atakuwa na wategemezi watatu wa karibu bila kuhesabu extended family memebers!

Nafikiri serikali inaangukia pua hapa kwenye huu mgao wa kijinga. Mpaka lini watanzania tutakuwa tunategemea mvua ili tupate umeme?

Someone has to take responsibility for this situation!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom