Mgao wa maji Dar, upungufu kina cha maji mto Ruvu na Wami

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Kuna taarifa nimesoma mahali juu ya upatikanaji wa maji. Mwaka huu mvua za Vuli hazijanyesha kabisa imeathiri sana upatikanaji wa maji katika mikoa ya pwani na Dar es saalam.

Tatizo lililopo si suala la kiufundi ndiyo maana Mhe. Rais anaharakisha ujenzi wa bwawa la kidunda liwe mbadala wa upatikanaji wa maji na solution ya kudumu kwa Jiji la Dar es salaam.

Taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa iliyotoka hivi karibuni inaonyesha mvua kwa mwaka huu zitanyesha chini ya wastani au zinaweza kuchelewa.

Maji tuliyonayo majumbani tuyatumie kitaalam, waambieni jamani dada wa kazi na mashamba boy katika matumizi ya maji.

Mabadiliko ya tabia ya nchi hichi kitu ni balaa.
 
Kuna kipindi ilitokea South Africa kukawa na mgao wa maji wa kupimiana kwenye ndoo.....hadi kwenye nyumba za wageni nilishuhudia tangazo kuhimiza uoge mara moja kwa siku na ufungue maji chini ya dakika mbili kutokana na uhaba mkali wa maji uliokuwa umesababishwa na ukame wa muda mrefu.
 
Haya mambo ya Mara ukame, Sjui njaa n.k.

Haya ni mambo mtambuka, ila pia Kwa sehemu nyingine, kiimani tunaita, Kibali cha Mungu Kwa watawala wetu, hakikipo,

Tuombeeni Taifa na viongozi wetu
 
Africa ni kama tume laaniwa kweli maji nao yawe shida wakati tuna ziwa kuu la 3 duniani kua na fresh water, Israel ili pata maji kutoka misiri karibu 1200km, na wakatalipia, wemehamisha undogo wa rutuba kutoka Jordan na Syria ili kufanya kilimo cha bogamboga, sisi kila kitu tunacho, maji safi kwa wakazi wa dar wasio zidi 4m tatatizo ni nini?
 
Kuna vitu hua vinanishangaza sn kwenye nchi yetu hii iliojaaliwa kila rasilimali kona zote za nchi.
Mikoa yote inayokaribiana na bahari kusingetakiwa kua nauhaba wa maji kabisa.mfano Dar ndio mji unaoongoza kwa kua naviwanda vingi nawasomi wengi sana serikali or hata wenye mtaji mkubwa wangetumia maji ya bahari kuilisha Dar ikawa inawauzia dawasco nakuweza ongeza kipato...uchujaji huu ungesaidia kupata chumvi na maji yakuilisha Dar nzima. ..kuna wasomi wengi sn wa kemia ambao wangeweza saidia taifa/jiji kuondokana nautegemezi wa mito...government needs to work up.
 
Back
Top Bottom