Mgao wa DRFA shillingi milioni 12

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Wapenda michezo,

Mchezo wa juzi DRFA imeingiza 12m bila jasho.

Naomba kuuliza hawa DRFA wana responsibility gani kubwa ya kuwafanya wapate mgao mkubwa hivi? Je TFF inavitendea haki vyama vya michezo mikoa mingine kama Mwanza,Unguja,Singida nk kwanini huo mgao usigawanywe kwa vyama vyote vya mikoa? Au kwanini Taifa Stars isicheze uwanja wa Gombani Pemba au Kambarage Shinyanga? Najua hamna haki bila wajibu je wajibu wa DRFA kwa maendeleo ya mpira ni nini? Na je DRFA wanafanya huo wajibu wao?
 
Mkuu nakubaliana na wewe, huo uwanja ni wa Taifa, siyo mkoa. Umejengwa kwa fedha za Watanzania siyo watu wa Dar pekee hivyo mgawo unaotokana na mapato ya uwanja huo si sahihi yakabaki Dar peke yake, unatakiwa ufike mikoa yote ya Tanganyika na Zanzibar. TFF walitazame jambo hili kwa jicho la 3.
 
mkuu nakubaliana na wewe, huo uwanja ni wa taifa, siyo mkoa. Umejengwa kwa fedha za watanzania siyo watu wa dar pekee hivyo mgawo unaotokana na mapato ya uwanja huo si sahihi yakabaki dar peke yake, unatakiwa ufike mikoa yote ya tanganyika na zanzibar. Tff walitazame jambo hili kwa jicho la 3.
huo uwanja ni mali ya wajanja wachache ,ndio maana wananyonya uchumi wa uwanja wa taifa ohh sorre uwanja wa .............,kuleni nchi ......heri mkoloni arudi atutawale.
 
Back
Top Bottom