Mganda kinara mgomo UDSM ni wa UVCCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganda kinara mgomo UDSM ni wa UVCCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fidel80, Nov 22, 2008.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  UDSM ni wa UVCCM

  Na Rehema Mwakasese

  JESHI la Polisi nchini limesema mwanafunzi raia wa Uganda, Bw. Odong Kefa Odwar anayetuhumiwa kuwa kinara wa migomo mingi kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ni mwanachama hai wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) baada ya upekuzi aliofanyiwa kubaini kuwa na kadi ya umoja huo.

  Kutokana na hali hiyo jeshi hilo linafanya uchunguzi aidi kubaini mtu aliyempatia mgeni huyo kadi hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Makosa dhidi ya Binadamu, Bw. Peter Kivuyo alisema kuwa mwanafunzi huyo alipatiwa kadi hiyo katika tawi la Chuo Kikuu mwaka 2006.

  Bw. Kivuyo alisema kuwa namba ya kadi hiyo ni 711818 ambayo inaonesha kuwa ilitolewa Oktoba 25 huku pia upekuzi huo uliofanyika kwenye nyumba alikokuwa akiishi Mikocheni, Dar es Salaam, ukionesha kuwa Bw. Odwar alipatikana na daftari ambalo limeandikwa maneno yanayoashiria alikuwa anajihusisha na masuala ya kisiasa hapa nchini.

  Bw. Kivuyo alisema katika uchunguzi walioufanya wamegundua kuwa mwanafunzi huyo alikuwa kinara wa kushawishi migomo ambayo ilikuwa imetokea katika vyuo vya hapa nchini.

  Aidha alisema jeshi la polisi liliamua kumrudisha nchini kwao Uganda lakini Ofisi ya Uhamiaji ya Uganda imemzuia katika uwanja wa ndege wa nchini humo kwa sababu wanasubiri taarifa zaidi kutoka Tanzania ili hatua za kisheria zichukuliwe mkondo wake.

  Naye Kaimu Kamishina wa Uhamiaji, Uthibiti, Huduma za Mipaka na Ukaguzi, Bw. Philo Nombo alisema kuwa walimpatia, Bw. Odwar kibali cha kuishi nchini kama mwanafunzi na akapatiwa taratibu zote zinazohusu kuishi nchini lakini kwa sababu amevunja sheria hana tena ruhusa ya kuishi nchini.

  "Tulipata maelekezo kutoka Serikalini kuwa Bw. Odwar ameondolewa nchini mara moja kwa sababu amevunja taratibu za kuishi nchini nasi tulitekeleza agizo hilo," alidai Bw. Nombo.


  My take;
  Huyu jamaa angepatikana na card ya CHADEMA sijui wangemfanyaje maanake huo moto wake sijui!maana walikuwa wanasema CHADEMA wanahusika na migomo inayotokea sasa.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndio inawezekana wanahusika chadema kwa kumbambikiza hiyo cadi ya ccm kwani inashindikana ? Mbona hao polisi hawajasema hiyo kadi kama kweli ni yake na mtu ambaye alimkabidhi hakujua kwamba yeye sio raia wa tanzania ?
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Halafu inapaswa hiyo heading ubadilishe unadhalilisha uvccm kwa kweli hiyo sio haki
   
 4. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  I know the guy well, and I sometimes advised him on the nature of our Tz politics..Tatizo, to be frankly and honest,alkuwa more than opportunist, he was ready to advance anything just for the sake of his future fame..ishu ya kadi ya UVCCM sishangai,kuna vijana walikua wanamjaza ujinga na kumtumia kwa maslahi yao pia,waliwahi kumpeleka hata kwa KINGUNGE wakati anagombea urais last semesta, ili aonekane mtu wao-CCM-,lakini ajenda ilikuwa tofauti..very sorry for him coz nasikia hata Uganda mzee wa kofia ana matatizo nae.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  this kind of reasoning...
   
 6. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  sidhani kama CCM inadhalilishwa mkuu SHY,kwani in mafisadi wangapi wenye kadi na wengine ni viongozi kabisa?
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kivuyo aache usanii. Polisi ni mabingwa wa kubambikiza kesi. Wapo watu kibao waliobambikiziwa kesi za mauaji na kusota rumande miaka kibao huku majambazi yakitesa mtaani. Kujua kadi ilitolewa na nani wakati tawi ilipotolewa linajulikana ni kitu cha kufanyia uchunguzi? Hiyo kadi walimbambikizia kijana ili wapate uhalali wa kumfukuza nchini. Shame on you Kivuyo.
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ibadilishwe vp?Wakati tunaambiwa tena kuwa zengwe la migomo nchini ni mkakati kabambe wa watu wanao wania uongozi 2010.Yawezekana yeye alienda na akapewa kwa ridhaa yake.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hapo sasa sijui kijana wa watu ataweka wapi uso wake na huyo mzee wa mapama akikuchukia utakoma ubishi....bora amfuate Joseph Konn vichakani tu.
   
 10. Mr. Politician

  Mr. Politician Member

  #10
  Nov 22, 2008
  Joined: May 16, 2008
  Messages: 74
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  here we go again!
  Odong vs Mlowe mpaka jamii forums sio kihivyo kaka
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  here we go again mr.politician,siasa za DARUSO sio mahali pake humu,just mwaga facts zinazoendana na mada...
   
 12. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  hapo ndipo utakapotambua ama kwa upinzani au kwa chama tawala siasa za
  DARUSO zimeingiliwa!
   
 13. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Its an obvious fact!!
   
 14. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  tatizo kubwa tunatawaliwa na serikali ilyokosa mwelekeo na uhalali wa kuwepo, inatafuta mchawi kwa kila jambo, badala ya kushuhulika matatizo ya mkopo ambayo ndo chimbuko la migomo yote hii ya wanafunzi wanakimbilia kumfukuza mganda wa watu, badala ya kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu wanakimbilia kwenye mhimili mwingine yaani judiciary kuzuia wasigome. hatujawahi kuwa na serikali dhaifu namna hii.

  kikwete alipaswa aidha aidhinishe mikopo inayolalamilikiwa na wanafunzi au kama hana uwezo nayo aende pale mlimani azungumze na wale vijana, ataweza? akienda pale anaogopa ukuulizwa kuhusu kagoda, manji, nk

  ninamliia NYERERE mtu pekee aliyeweza kuzungumza bila woga kwa kuw hakuwa fisadi
   
 15. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  umegusa kiini-tete mkuu!! you can't believe. as a president hajawahi kwenda 'kuzungumza' na na hao vijana!! very pathetic..
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwikimbi big up sana unajua hata mimi nashindwa kuelewa the link between UVCCM, mgomo na huyo Odong na nini serikali inataka watanzania waamini. Na vilevile polisi wanaingiaje kushughulikia mgomo wa wanafunzi?????? Do they have the solution or at least the understanding au ni kufuata tu walichoambiwa na mabwana zao??
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sioni kosa la CCM kwa mgeni kukutwa na kadi ya uanachama kwa sababu unapo declare uzawa kwenye fomu za maombi sidhani CCM inategemewa iwasiliane na uhamiaji kupekua mafaili ya uzawa wako.

  Wabongo kibao wamempigia kura Obama, na sidhani karani wa voter registration alisumbuka kupiga simu Homeland Security kuthibitisha taarifa za uraia ulizojaza kwenye fomu ya uchaguzi.

  But all the same, huyu Mganda angekuwa CHADEMA mbona ingekuwa mbinde. Kijana Julius Mtatiro, Mtanzania, kakutwa na business card ya mtu wa upinzani political police wamemsweka kizuizini wakamuuliza maswali mia nne usiku kucha kichwa kidogo kimpasuke kabla ya kumuwahisha hospitali.
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Polisi wa Nchi hii wamekosa mwelekeo kabisa na nadhani wanazidi kujidhalilisha .Nimeshangaa na bado siamini kwamba watanzania wanaweza kuamini kwamba vijana wakotulivu ila Mganda ndiye alikuwa analeta tatizo .Wacha tuone baada ya Mganda kuondoka nini kinafuata .
   
 19. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kuwa na kadi ya CCM au kutokuwa nayo haimaananishi kwamba wewe siyo mfuasi wa upinzani. Hizo huwa zinatolewa tu muda wowote ukihitaji na bila kitambulisho. Fidel80 lazima utambue kuwa nchi hakuna vitambulisho vya uraia kwa hiyo kila aliyemo ni lazima athibitishe kuwa siyo raia, not otherwise! Inanikumbusha enzi za jeshi, kulikuwa watu kibao kibao ambao nilikja kugundua kuwa siyo baada ya serikali ya Kigali kupinduliwa 1994 na ya kitusi ikawekwa madarakani! Wote walirudi Kigali na kupata vyeo. Mpaka leo nashangaa! Kwa kifupi, Huyu jamaa ni hatari kabisa na nadhani ilikuwa muda muafaka kumtimua. Wako wengi, watani zetu hapo, wanajifanya raia wa nchi. Wako wengi sana. Nina hakia hata vitambulisho vya uraia vikitoka watapewa pia!

  Pia, watu wengine lazima mfikirie. Rais hawezi kuwa anakuja kushughulikia issue ndogo kama za kuongea na wanafunzi wa vyuo vikuu! Viko vingapi nchini!? Kuna kazi nyingi sana za Rais na si kuja kuongea kila mmoja anayelalamika. Kuna mawaziri watatu vizara hiyo na mmoja wa makatibu wakuu makini kabisa nchini. Sasa nyinyi kidogo tu, ati aje ongee na student!? Very stupid idea.

  Kuhusu mikopo, in fact ni kundi dogo tu, tena sana kwa kila chuo lilikuwa lina-instigate hii migono. nakumbuka hata enzi zetu, injias wakiamua kule FOEs baso unakuwa mgomo wa chuo chote, wether you like or not. Kukuthibitishia hili, wewe subiri one month, students watapewa mashrti na wote watarudi. Uje uniambie sasa kama kweli ulikuwa mgomo au upuuzi!
   
 20. k

  kela72 Senior Member

  #20
  Nov 22, 2008
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bw. Peter Kivuyo alivyokuwa aneleza utafikiri kafanya jambo moja kuuuubwaa! kama kuwafunglia mashtaka Kagoda?! Sasa tutaona kama migomo itakoma si mchochezi hayupo? Serikali hii inaona kila mgogoro unachochewa na wanaotaka kuingia Ikulu 2010, na hii inatokana na mbinu hii (pamoja na kuchafuana) kutumiwa sana na wana mtandao walipokuwa wanaisaka Ikulu. Hivyo wanaona haiwezekani haya mambo yakatokea tu.. lazima kuna mkono wa mtu.
   
Loading...