TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Kwa siku kadhaa ndani ya mitandao ya kijamii wamachama wa chama cha mapinduzi (CCM) wamekuwa wakilitumia jina langu kwamba eti wamenishawishi kujiunga na chama chao na kuwa siku ya jumapili tarehe 23/08/2015 nitajiunga na chama chao, katika uzinduzi wa kampeni zao
WALIYOYAFANYA.
1. Ni kweli na dhahiri kwamba CCM wamenishawishi kwa fedha na vyeo ili nijiunge na chama chao.
2. Wamewatuma wazee wengi sana kuja kunishawishi akiwemo katibu mkuu wao, mkuu wa usalama wa taifa, wazee wa chama chao nk.
MASWALI YA KUJIULIZA.
1. Kwa nini CCM wananifuata wakati huu na sio wakati mwingine?
2. Je, mbona mwaka 1995 walinitusi sana nilipoamua kuhama CCM, hali kadhalika mwaka 2010?
3. Je, sio kwamba CCM maji ya shingo yamewafikia?
4. Je, kwa nini wananiahidi vyeo vikubwa na mapesa mengi wakati huu na sio wakati mwingine kama wao walitambua kwamba nilistahili kuyapata hayo miaka iliyopita?
TAHADHARI.
1. Kwa hatua hiyo ni kwamba CCM wanatambua kwamba wamepoteza mvuto kwa wananchi hivyo hatuna budi kuyatafuta mabadiliko nje ya CCM.
2. Sina mpango wala sifikirii kukihama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) chini ya mwavuli wa UKAWA.
3. Baada ya CCM kuyaona mafuriko ya ukawa sasa wamegundua kwamba kuelekea uzinduzi wa kampeni zao walitumie jina langu ili angalau wapate watu wengi kwa sababu wanaelewa fika kwamba wamepoteza mvuto (MSIDANGANYIKE).
4. Siwezi kuyasaliti matumaini ya watanzania kwa maslahi yangu binafsi.
5. Hilo ndio goli la mkono wanalolisubiri kwa miujiza (Yesu atakapokuja kwa mara ya pili).
MWISHO.
Nawatakia kila la kheri katika kuyatafuta mabadiliko nje ya CCM, daima tusife moyo tupo pamoja na tutashinda kwa nguvu ya umma.
Wenu katika ukombozi,
Dr. Wilbrod Slaa,
KATIBU MKUU, CHADEMA.