warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,213
- 18,455
Dah nimesikiliza mkasa wa huyu binti mdogo aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini Indonesia Mwaka 2017 na kuhukumiwa miaka 18 jela, story yake inasikitisha sana na kuhuzunisha
Kitu ambacho anakijutia zaidi ni kukamatwa wakati akiwa bado hajatimiza ndoto yake ya kumjengea nyumba Mama yake , anadai kama angetimiza ndoto yake hiyo , hiko kifungo kisingemuuma sana Kwani angejua Mama yake yupo sehemu salama ila sio sasa hivi ambapo hajui hata anakula nini na anaishi vipi na hajui kama akitoka atamkuta mama yake yupo hai au yeye mwenyewe kufia jela.
Kilichonivutia zaidi ni ujasiri aliokuwa nao wa kusimulia mkasa huo wa kuogopesha na kutisha bila kuwa na uoga wowote au huzuni.
Mungu amsaidie aweze kutumikia kifungo chake salama na kurudi uraiani
Sent from my iPhone using JamiiForums