Mfumo wetu wa jua ulivyo jiumba hapo zamani za kale

THE SPIRIT THINKER

JF-Expert Member
Sep 9, 2019
392
555
FAHAMU SAYARI ZETU 8 ZILIVYOJIUNDA 🤔

Sayari zimeanza kujiunda mara baada tu ya mfumo wetu wa Jua ulivyomaliza kuundika kutokana na mawingu mazito yenye gesi na mavumbi mavumbi yatokayo huko interstellar space

Mawingu mazito yalipasuka kutokana na mvumo au twaweza kusema shockwave iliyotokea baada ya mojawapo ya Nyota kubwa ilivyolipuka kitaalamu tunaita " supernova 💥 " na kupelekea kuuna solar nebula au twaweza kusema swirling disk of material

Mzunguko wa mduara wa gases ndio kitu kilichoundwa ambapo kutokana na mzunguko huo ilipelekea kutokea kwa nguvu ya uvutano katikati ambayo ilipelekea kuvuta zile material gase katikati na kusababisha pressure kubwa katika kiini kilichopo katikati hatimaye hydrogen atoms ziliungana na kuunda helium na kusababisha kutokea kwa mlipuko mkubwa uliosababisha muwako

Mzunguko ule wa gases mbalimbali ulisababisha kuvuta maada zilizopokaribu na kuziunganisha kwa pamoja yaani mawe yaliungana kwa pamoja na pia vipande vya barafu na gases viliungana kwa pamoja na kutokana na mizunguko ya hizo maada basi kuna kulizaliwa nguvu ya uvutano na kuunda mduara wa maumbo

Baadhi ya mawe yalishindwa kushikana kwa pamoja na kuunda masayari matokeo yake yalipeleke kuunda asteroids belt na mengine yaliishia kuunda asteroids zile kubwa kubwa kabisa

Maada za mawe ziliunda sayari kama mercury , Venus , Earth na Mara huku Maada za Barafu na Gas ziliunda Gas Giant na Ice Giant - Jupiter , Saturn , Uranius na Neptune

Naishia Hapa kwa Leo
 
TUHUFAHAMU MFUMO WETU WA JUA

MFUMO WA JUA ( CHAPTER 1 ) 💥

UTANGULIZI

Mfumo wetu wa sayari (Dunia) ambapo tunapopaita nyumbani unapatikana kwenye upande wa spiral arm kwenye kundi kubwa la Nyota ambapo Nyota yetu ya Jua ndipo ilipo kundi hilo Linaitwa Milkyway Galaxy .

Mfumo wtu wa Jua umejumuisha Nyota yetu ambayo Ni Jua Tambua Hii ndio imebeba Jina la mfumo mzima ukiachilia mbali Nyota Jua na vyote vilivyomo ambavyo vimeshikiliwa thabiti na uwepo wa Nguvu ya uvutano iitwayo gravity vilivyomo ni kama Sayari ;

(1)Mercury
(2)Venus
(3)Earth
(4)Mars
(5)Jupiter
(6)Saturn
(7)Uranius
(8)Neptune

Bila kusahau uwepo wa Sayari kibete kama Pluto ; na Namba nyingi za Miezi (Moons) na Mamillion ya Mawe ( Asteroids , Comets na Meteoroids )

Tukienda mbali zaidi Nje kabisa na Mfumo wetu wa Jua kuna Masayari mengi zaidi na Namba nyingi za Nyota kwenye Anga letu kwa wakati wa Usiku , Hadi sasa tumeweza kufanya upembuzi yakinifu na kugundua Maelfu ya Sayari ambazo zinazozunguka nyota Nyengine kwenye ilivyo kwa sayari zinavyozunguka Jua Letu kuna Mifumo mingi ya Nyota inazaozungukwa na sayari kwenye Kundi Letu Nyota La Milkyway Galaxy ,

Ukiachilia mbali sayari zilizogunduliwa mpaka sasa Kwenye kati ya Mabillions ya Nyota yanakadiriwa kuwa na Syari zake zenyewe , Lakini huenda kwenye 100 galaxies ulimwenguni kote , Vilevile inahisiwa Sayari yetu Dunia Huenda ikawa inachembechembe za kutokea huko katika Cosmic .

Kuna Sayari Nyingi sana katika Ulimwengu wetu zinazofanana na sayari yetu ambazo zinazozunguka mifumo yake iliyonayo na Nyota

Mfumo wetu wa sayari umeitwa " Solar system " kwasababu Jua letu lilipewa Jina la Sol , ambalo lilikuja kubadilishwa na walatini na kuita Sun "solis" kwahiyo kitu chochote chenye kushabihiana na Jua tutahihita "solar "

UKUBWA WAKE ENEO

Mfumo wetu umesogea mbali sana tofuti na mawazo ya wengi wanavydhani umeishia tu kwenye sayari ya Mwisho Neptune Hapana , Mfumo wa Jua umeenda mbali na kujumuisha mkanda wa Kuipler Belts ambao upo kati ya Neptune orbit na Sayari kibete Pluto

Mkanda Huu umejawa na umetengeneza Mduara uliojawa na Maumbo yenye barafu amabyo kwakiasi fulani mengi yanaukubwa kama sayari kibete maarufu iitwayo Pluto

Tukiaenda mbali mbele zaidi ya Mkanda wa Kuipler belt kuna "Oort Cloud" Oort Shell ni Ganda kubwa wa Duara lililozunguka mfumo wetu wa Jua .

Kumbuka Ganda hili bado halijaonekana ni kwa jinsi gani lilivyo bali limetabiriwa kutokana na mathematics models and chambuzi mbalimbali (obsevation) za Kometi
ambazo zaidi hupatikana kwenye eneo hilo

The Oort cloud imeundawa na vipande vya mabarafu yaliyotokana na mabaki baada ya maumbo ya nyota na sayari - Mengine yanaukubwa
zaidi ya Mlima yanazunguka mfumo wetu wa Jua kwa umbali wa 1.6 Miaka ya Mwanga (Nuru)

Ganda hili lina matilio Manene yenye yenye kufika mbali kwa zaidi ya 5000 Astronomical Unit to 100,000 Astronomical unit " 1 Astronomical unit 1 ni sawa na umbali kutoka kwenye Jua mpaka duniani au ni zaidi ya 90 milions Miles au (150 million kilometers)

Ganda la Oort cloud ni mpaka wa nguvu ya uvutano wa Jua ambapo maumbo yote yanayozunguka Jua yakifika hapo hayawezi kuvuka
au kutoka nje zaidi ya hapo kiufupi hapo ndipo mwisho wa umiliki wa nyota yetu Jua .

Tabaka la Jua liitwalo Helisphere haliendelei mbali zaidi sana ya Hapo . Heliosphere ni Nini ? " Heliosphere ni maputo yanayozalishwa
na solar wind yaani mvumo unaotokana na uchakachuliwaji wa hewa za hydrogen na helium ili Jua iweze kuwaka au tuseme ni
Mikondo ya electrically charge gas ambayo hutemwa juu kila upande mwa Jua kwa mielekeo tofauti tofauti , eneo ambalo ni mipaka
ya hizi solar winds huitwa terminator , solar winds hupunguzwa kasi au husimamishwa kutokana na pressure kutoka kwenye gas zitokazo
huko interstellar space

Ni vyombo viwili tu vilivyotengenezwa na mwanadamu vimeweza kuvuka eneo hili la Terminator shock : Voyeger 1 minamo mwaka 2004
na Voyager 2 katika miaka ya 2007 , voyager 1 ilifanikiwa kufika katika anga za interstellar katika miaka ya 2007 na kufuatiwa
na voyager 2 katika miaka ya 2012 kumbuka vyombo vyote hivi vilirushwa kwenye miaka ya 1977 na vilirushwa na shirika la uchunguzi
wa anga za mbali Nasa .

MIEZI

Kuna zaidi ya Miezi 200 iliyokwisha tambulika baada ya tafiti mbalimbali za kisayansi kwenye Mfumo wetu wa solar system na baadhi bado inasubiria udhibitisho wa kiuchunguzi wa wataalamu , Katika sayari zote 8 Mercury na Venus pekee ndizo sayari zilizokuwa hazina Miezi lakini kwa sayari zote zilizobaki zinazungukwa na miezi yake yenyewe .

Sayari 2 kubwa ( Gas Giant ) ndizo zinazoongoza katika kumiliki miezi Mingi sana katika muonekano mwengine makundi ya miezi hii katika sayari hizi huonesha ni kwa jinsi gani ule mfanano wa solar system na sayari zake ulivyo kam sayari hizi zinavyozungukwa na miezi yake

Sayari kibete pluto ni ndogo zaidi ukifananisha na Mwezi wetu wa Duniani ila Sayari
kibete hii ina miezi yake 3 kwenye orbit yake ikijumuishwa Charon mwezi huu ni mkubwa sana unaopelekea sayari kibete hii kutetemeshwa
kwasababu ya mvutano mkali sana bina ya Pluto na Charon Moon ,
Fahamu hata Asteroid inaweza ikawa na Miezi yake wanasayansi wameshafanyia uchunguzi jambo hilo

UUNDWAJI

Mfumo wetu wa Jua umeundwa miaka 4.5 billions iliyopita kutokana na mawingu mazito za gesi na mavumbi zitokazo huko interstellar space
Mawingu yalipasuka pengine kunauwezekano yalipasuka kutokana na mvumo " shockwave " kutoka kwenye nyota ya karibu iliyopasuka
kitaalamu tunaita "Supernova "

Kipindi mawingu haya yakipasuka au kulipuka baadae huunda Solar nebula yaani kiini cha muwako -Yenye Material
yanayozunguka mfano wa sahani mduara

Katikati mwa sola nebula Hii nguvu ya uvutano inayavuta yale material kwenda ndani zaid Hatimaye Huzalisha Pressure kubwa kwenye kiini
inayopelekea Hydrogen atoms kuanzakujichanganya kwa nguvu na kuzalisha Helium

Ambayo baadae huzalisha kiasi kikubwa sana cha
Nishati na Kupelekea Kuwaka na Kutokea kuzaliwa kwa Jua Letu na hatimaye kukusanya 99% ya Maada zilizopo .

Maaada zilizokuwepo nje ya mzunguko huo zilikusanywa kwa pamoja , Zilijikusanya na kuvunjikavunjika moja baadala ya nyengine
na hatimaye kuunda maumbo makubwa makubwa , Maumbo mengine yalijijenga kwa pamoja na nguvu za uvutano za maumbo hayo zilijiunda
maumbo ya maduara kimionekano na kuwa sayari ,

sayari kibete , na Miezi mikubwa , vipande vya maumbo madogo madogo yaliyoshindwa kuungana
kwa pamoja na kutengeneza sayari wakati wa ule mzunguko wa "swirling disk"

Hatimaye yaliishia kutengeneza mduara wa ule Mkanda wa Asteroid Belt
Vipande vyengine vilijiunga kwa pamoja na kuwa vipande vikubwa ambavyo kwa sasa kitaalamu tunaviita Asteroids , Comets , Meteoroids , na Miezi yengine iliyokosa maumbo ya kimuonekano

MIPANGILIO

Mpangilio wa Sayari na maumbo mengine yanayolizunguka Mfumo wetu wa Jua yalitokea kipindi wakati mfumo wetu wa Jua ulivyokuwa ukijiunda
Karibu kabisa na Jua ni sayari Zenye miamba migumu ziizoweza kuhimili kiwango kikubwa cha Joto wakati mfumo wetu wa Jua ulivyokuwa
mdogo sana " early solar system " kwasababu hizi zilipelekea kuwepo kwa kwa sayari kama - Mercury , Venus , Earth , Mars , Hizi zote
ni sayari zenye ardhi ngumu " Terrestial Planets "

Wakati huohuo aina za matilio kama ice , liquid au gas zote zilijishikilia kwa pamoja mbali kidogo na mfumo wa jua wakati wa udogo

Nguvu ya uvutano uliyavuta matilio hayo kwa pamoja na kuunda sayari kama Jupiter , Saturn na Sayari zenye Mabarafu kama Uranius na Neptune

Mwendelezo utaendelea

Andiko La Moudy Swema💥
 
Back
Top Bottom