Mfumo wa vyama vingi ufutwe

mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
842
512
Ndugu wana JF,
Nadhani ni muda muafaka sasa wa kufuta mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Sababu;
1. Maisha enzi za chama kushika hatamu yalikuwa ya upendo, umoja, amani na heshima. Tofauti na sasa ambapo hakuna tena upendo, tazama post zinazohusu majeshi, waziri mkuu n.k.
Kila mtu ni msemaji, tumekuwa familia ya kambare!
2. Mfumo huu ulikubaliwa na asilimia ndogo tu ya Watanzania.

Ndugu wana JF, kurudi nyuma (retreat) ni mbinu pia ya ushindi.

Naomba kuwasilisha. Zidumu fikra sahihi za watanzania. Mungu ibariki Tanzania.
 
Naona mmeishiwa hoja, si ajabu kesho mkaja na wimbo wa mfumo wa dini nyingi ufutwe, mfumo wa madhehebu mengi ufutwe,mfumo wa familia moja kuwa waumini wa imani tofauti ufutwe na kadhalika.Upendo, amani na umoja misingi yake mikubwa siyo kulazimisha kuamini katika itikadi moja bali katika usawa na uhuru wa kuamua suala unaloamini na ndiyo maana Mwl.Nyerere alisema kupanga ni kuchagua!
 
Unakuwa kama unajipiga risasi mwenyewe.

Kwani hufahamu kuwa na television wakati huo ilikuwa ni dhambi katika macho ya Mwl. Nyerere achilia mbali kuweza kutumia viganja, screen na internet kurusha maneno yako wakati wowote na mahali popote kwa yeyote yule atakaye yasoma.

Hujui kipindi cha utawala wake kuwa na pasi ya kusafiria ilikuwa ni DILI na UJIKO achilia mbali kusafiri nje ya nchi.

Hujui kama Mwl. Nyerere alitunyima maendeleo kutokana na mlengo wa siasa zake za nadharia za ujamaa na kujitegemea.

Hujui kama Mwl. Nyerere 'alichanja mbuga' za uongozi kwa kutumia lugha ya 'kung'atuka' baada ya gari la maendeleo alilokuwa analiendesha nchini kumshinda.

Alifikiri ataonekana mwanamme akikataa kula matapishi yake bila kujua kuwa KURUDI NYUMA (RETREAT) NI MBINU PIA YA USHINDI!.

Kila kizuri kina ubaya wake lakini mabaya ya utawala wa Mwl. Nyerere kwa maendeleo ya binadamu yalikuwa ni mengi zaidi ya mazuri. Kurudi huko ni kutaka kuwa na mabaya mengi zaidi ya mazuri.

We have moved.
 
Tatizo lililopo ni kuwa watawala hawajui maana ya nchi kuwa na vyama vingi. Hiyo ni kukua kwa demokrasia na kila mtu ana uhuru wa kufuata itikadi anayoona inafaa. Ni haki ya kila mtu ya kikatiba. Tatizo la watawala wanaona mtu anayependa chama ambacho hakiko madarakani wanamwona ni adui kitu ambacho si sawa.

Watawala hawajaelewa umuhimu wa kuwa na vyama vingi ndiyo maana hata bungeni wabunge wa upinzani wakitoa mapendekezo yanayosaidia nchi na wananchi wabunge wa CCM wanapinga eti tu kwa sababu jambo hilo limetolewa na mbunge toka upinzani.

Hata vurugu zinazotokea ni matokeo ya kutokuelewa kuwa vyama vyote vinatakiwa kuwa treated sawa. Kama ni haki ya kufanya mikutano vyama vyote vipewe nafasi sawa. Siyo chama tawala kinaruhusiwa lakini vingine vinafanyiwa mizengwe. Tatizo hata vyombo vya dola bado either havielewi au vinafanya makusudi kupendelea chama tawala.
 
Sisi wakati huo tulilazimika kuchukua kadi za uanachama wa TANU Youth League, KABLA ya kufikiriwa kustahili kupata hati ya kusafiria (Passport).

Tehe tehe tehe! Hata sijui iko wapi kadi yangu. Kumbe mimi bado "chipukizi"?
 
Haki ya mungu ccm ikiacha mbinu chafu kwa upinzan aman itakuwa zaidi kwan kila mwovu ataibuliwa na kushtakiwa! Maendeleo yatakwepo kwan kila pungufu litakicost chama kitakachokuwa madarakan hivyo wananchi kuamua nani aongoze, tutaokoa fedha nying kwan ccm inatumia fedha nying kujihakikishia wanabak madarakan. Ni mimi nimesema.
 
Hata na mimi naunga mkono hoja hii kuwa Mfumo wa Vyama vingi ufutwe na ubakishe mfumo wa Chama kimoja tu na kiwe CHADEMA maana ndicho chenye mwelekeo hapa TZ
 
Sisi wakati huo tulilazimika kuchukua kadi za uanachama wa TANU Youth League, KABLA ya kufikiriwa kustahili kupata hati ya kusafiria (Passport).

Tehe tehe tehe! Hata sijui iko wapi kadi yangu. Kumbe mimi bado "chipukizi"?
Mkuu, mimi huwa ninawashangaa sana watu wanaojaribu kulinganisha mazingira ya kipindi cha utawala wa Mwl. Nyerere na mazingira ya utawala wa sasa na kuona ya Mwl. Nyerere yalikuwa bora kuliko ya sasa.

Kweli kila binadamu ana fikra na mtazamo wake pamoja na kwamba ukweli unabakia kuwa ni ukweli.
 
Tuna chama kimoja tu, chenye historia ya nchi hii. Unakijua hata wewe!

The recent black history of this country does not help Tanzanians of this generation. Tanzania's history must be rebuild and forget the past! Hatuhitaji tena chama chenye historia ya ufisadi na uonevu Tanzania.
 
Kwa mfano tukisema tunarudisha chama kimoja, we ungependa chama gani kishike hatamu!
 
Kama vyama vyote vitafutwa kisha tuanze upya kabsa hapo naweza nikakuelewa kidogo sana ! Mie ningependekeza vibaki vyama viwili tu pamoja na mgombea Binafsi twende na Mfumo wa USA kwani utitiri wa Vyama Kama Congo DRC hukusaidii zaidi ya kuzidisha mgawanyo wa kura na kupata viongozi waliochaguliwa na watu wachache sana !
 
Back
Top Bottom