Mfumo wa utumishi wa umma umevurugwa na umevurugika hakuna sheria tena bali ni utashi wa mwenye mamlaka juu yako

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Kama kichwa kisemavyo hapo juu utumishi wa uma kwa sasa haueleweki

Maamuzi mengi yanategemea kauli ya aliye juu yako na si sheria tena inayo zingatiwa

Utumishi umekuwa wa mashaka kila siku maana huyu anapandishwa leo kesho kashushwa bila sababu , atapandishwa huyu yule ataondolewa bila sababu , huyu ata mtukana yule ili mradi tuu yuko juu yake ., utumishi hauna heshima tena na amani ya kazi imetoweka

Imefika hatua hata mwenye kiti wa chama kata anaweza kumtusi DMO hadharani huku akishangiliwa

Utumishi umevamiwa na wahuni hakuna tija uwepo wa sheria za utumishi maana kila mara ni vitisho na mikwara kwa watumishi

Nini kifanyike kurudisha heshima kwa watumishi waheshimiwe na watekeleze majukumu yao kwa umakini?
 
Siyo Utumishi tu.... Tazama bajeti za Wizara zinavyodhalilishwa...Hapa Kazi tu
 
hahahaaaaa yaaan kuna kitu mimekishuhudia na kimenisikitisha sana hadi napost uzi huu yaani mtu kwenda kuuliza kwanini nimeshushwa cheo bila kuitwa wala kuelezwa chochote anaambiwa ukiendelea kujifanya unajua sheria mshahara wako utasitishwa haaaaa!! kweli bora uishi kuzimu kuliko kuishi nchi isiyo heshimu sheria ilizo jiwekea yenyewe.
 
Kama kaweza kulipoka madaraka Bunge, sembuse watumishi was umma?

Kiasi kikubwa mahakama ni hivyo hivyo. Wamebaki mahakimu na majaji wachache weye uwezo wa kusimamia uhuru wa mahakama.

Kuna sehemu atakwama tu.
 
Umenitonesha kidonda kwani Mimi ni mfuasi wa uongozi unaojenga mifumo imara au taasisi imara na si MTU (individua)imara

Uongozi wa sasa unavunja mifumo imara ya kuendesha nchi.Mfano bunge limekuwa dhaifu,mahakama zimegeuka kuhukumu kulingana na upepo wa kisiasa,Jeshi lililovaa koti la chama, Katiba mbovu na sheria ndogondogo hasa za kijamii na kiutumishi kwa sasa ziko likizo, wizara hazina sauti juu ya mambo yaliyochini yao.

Ubaya wa kuharibu mifumo ni kuwa nchi inakuwa inamtegemea kiongozi mmoja imara au kikundi kidogo imara.Lakini siku kiongozi huyo imara akiondoka madarakani kwa kumaliza mhula wake au kwa kufariki nchi inaharibika na kukosa uelekeo.

Faida ya kujenga mifumo na taasisi imara ni kwamba hata akiingia kiongozi dhaifu mifumo inamuongoza na kumwelekeza namba bora ya kuendesha nchi, kama inavyotokea kwa nchi ya Marekani.
Uongozi usiopenda kujenga mifumo imara ni uongozi usiopenda maendeleo endelevu. Pia ni uongozi usiojali vizazi vijavyo.
 
Kabisaa leo walimu wamehamishwa kutoka sekondary kwenda msingi hawajalipwa mnakomaa na mkurugenzi anaanza kuomba msahaha ilikuwa order toka juu tukashindwa kujiandaa hela hatuna rudini secondary miezi mitatu wapo mtaani tu huu upotevu kabisa wa rasilimali watu...think tank ya awamu ya tano sijui ni nan???
 
Kama kaweza kulipoka madaraka Bunge, sembuse watumishi was umma?

Kiasi kikubwa mahakama ni hivyo hivyo. Wamebaki mahakimu na majaji wachache weye uwezo wa kusimamia uhuru wa mahakama.

Kuna sehemu atakwama tu.
naiona gharama kubwa sana ya kuirejesha mifumo iliyo kuwepo awali tena gharama kubwa kabisa baada ya jiwe na vibaraka wake kutoka madarakani maana hata mawaziri husika sijui wana kazi gani matatizo ni yale yale na tena yamezid
 
Jana nimesikia wanamkaanga Dr. Mpango. Wanasahau kwamba de facto Finance Minister ni Magufuli mwenyewe.
Mawaziri wamekosa ujasiri wa kuachia ngazi maana hawana kazi kabisa.
 
Standing Orders zimesiginwa hauelweki tena. Utawala wa awamu yA sita utapata Shida Sana
Awamu ya sita itahitaji muda wa kutosha kuirudisha nchi kwenye reli.
Kuna kuanza kuheshimu katiba na sheria za nchi.
Bunge kuja kutimiza wajibu wake.
Mahakama kuja kuwa mhimili huru.
 
Mie sihitaji kupandishwa mshahara,nachotaka Ni daraja langu sitahiki Na wakati sitahiki maana Ni haki yangu ya msingi ya kiutumishi.
Hata ukipandishwa hulipwi kama alivyotamka bali utasubiri hadi apende napo hutolipwa bali itatolewa orodha ya watu wachache nawe utapewa matumaini kuwa utalipwa awamu ijayo! Unakumbuka aliagiza kuwa upatapo barua ya daraja na mshahara wako wa mwezi huo unabadilika mwezi huohuo? Imekuwa kinyume kwani waliopandiahwa April mosi hadi leo mishahara yao ni ileile ya kabla ya daraja! Hakuna maelezo wala mshahara mpya zaidi ya kuambiwa usubirie arrears ambazo hazijulikani zitatolewa lini na huenda May mosi nyingine labda! Wafanyakazi jiongezeni kwani maisha haya siyo!
 
Kama kichwa kisemavyo hapo juu utumishi wa uma kwa sasa haueleweki

Maamuzi mengi yanategemea kauli ya aliye juu yako na si sheria tena inayo zingatiwa

Utumishi umekuwa wa mashaka kila siku maana huyu anapandishwa leo kesho kashushwa bila sababu , atapandishwa huyu yule ataondolewa bila sababu , huyu ata mtukana yule ili mradi tuu yuko juu yake ., utumishi hauna heshima tena na amani ya kazi imetoweka

Imefika hatua hata mwenye kiti wa chama kata anaweza kumtusi DMO hadharani huku akishangiliwa

Utumishi umevamiwa na wahuni hakuna tija uwepo wa sheria za utumishi maana kila mara ni vitisho na mikwara kwa watumishi

Nini kifanyike kurudisha heshima kwa watumishi waheshimiwe na watekeleze majukumu yao kwa umakini?
tapatalk_1527267431402.jpeg

Bila kuliondoa jinamizi hili tuateseka sana.
 
Leo tunapoongea kuna intake 3 hazijapandishwa Madaraja kuanzia 2016/2017, 2017/2018 na 2018/2019 Sijui siku akisema anapandisha Daraja atawapandisha kundi lipi maana jumla ya wanaotakiwa kupandishwa Madaraja imefikia watumishi 150,000. Nakumbuka Nape Nnauye alisema kama serikali itafanya Miradi mikubwa kwa Fedha za Ndani Kundi LA Utumishi Wa Umma ndilo litakaloathirika ndo Maana hadi Leo hakuna cha Kupandisha Mishahara wala Kupanda Madaraja kwa Watumishi Wa Umma. Hata watumishi Wa Umma waliopanda ni Wale Wa mwaka 2015/2016 ilikuwa bajeti ya Mzee Kikwete kabla ya kuondoka na si bajeti ya huyu jamaa. Mbaya zaidi hata hao waliopandishwa kwa bajeti ya mwaka 2015/2016 mishahara yao haijabadilika tangu wapewe barua nyingine Novemba 2017, sanasana kilichofanyika no kuagiza barua hizo zifutwe na kuandikwa upya.
 
Back
Top Bottom