Mfumo wa Rais Unatengeneza Kundi Jipya la Janjajanja na Wala Nchi kwa Mgongo wa Kuisaidia Serikali

Unajua wakati raisi anaingia madarakani nilijua kuwa ndio wakati hakuna mtu yoyote atatia mkono kwenye bakuli la nyama la serikali na kujichotea minofu, hakuna mtu atapata "upendeleo" kutoka serikalini, hakuna mtu atafanya mambo kwa nyodo kwani serikali ya awamu ya 5 haina "undugu/ushkaji/urafiki"

Mweeeee kumbe sio bwana, watu walishachungulia mapungufu na kuchukua fursa hiyo. nimeona uzi nyingi humu juu ya GSM mwaka juzi ikijulikana kama Home Shopping Center. Mwishoni mwa mwaka 2015, Home Shopping walitangaza kufilisika na kufunga kampuni lao hilo, kisha mwanzoni mwa 2016 wakaja na kampuni jipya la GSM wakiambatanisha na Charity yao ya GSM Foundation ambayo ninakiri kwa kinywa changu kuwa inafanya kazi kubwa katika upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa nchi nzima, kazi nzuri sana.

Hawa GSM ndio wafadhili wa mabango ya kampeni ya kupanda miti Dar nzima, na kumbuka kampeni hii ilikuja na makonda baada ya upinzani kuamsha joto la UKUTA.

GSM ndio wafadhili wa ziara ya Paul Makonda juzi juzi kuzunguka Dar, kuna magari yalikuwa yana nembo ya GSM yalikuwa yanamsaidia Mkuu wa Mkoa kupunguza gharama za PA.

Hata ziara ya Makonda na mkwewe Marekani ninahisi GSM wamemsaidia kupunguza gharama za matumizi kidogo. Kwani nilipoona Makonda yupo New York, Los Angeles na Springfield Massachusetts kuna baadhi ya mameneja wa GSM wapo miji hiyohiyo, ikawa inanibidi nianze kuunganisha nukta zangu moja baada ya moja mpaka hapo walipo amua kupiga picha ya pamoja na kujiita Class sehemu moja.

Hata kuna tetesi za "vijiweni" kuwa kuna ndugu wa hao jamaa wa GSM aliswekwa kituo cha polisi kwa kosa la uvutaji shisha, akapiga simu moja tu, wakatolewa kituo kizima hata waliokuwa central kwa makosa tofauti wakapata msamaha wa ndugu wa jamaa wa GSM, mwishoni mwa mwaka 2016. Habari za vijiweni zinasema jamaa wa GSM wanapata kaupendeleo sana kwenye baadhi ya mambo kwani wanajitoa sana pia kwa serikali ya mkoa.

Swali kubwa ninalo jiuliza ni kuwa, Home Shopping/GSM wanatoa misaada kwa Tanzania, Dar es Salaam na ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kwa Mkuu wa Mkoa bure bila return yoyote? Wanarudisha kwa jamii pasipokuhitaji mrejesho wowote?

Kama Home Shopping ilifilisika, GSM wanapata wapi fedha za Charity na kuisadia Serikali ya mkoa na mkuu wa mkoa? Usiniambie ile stunt iliyofanywa na wasanii wa bongo fleva Diamond na Ali Kiba kumpa msaada mkurugenzi wa GSM kama mchango kuiwezesha GSM Foundation.

Ninahisi wakati "baadhi" ya mafisadi na wakiondolewa kwenye ulaji na mirija ya asali na maziwa kuna baadhi wanatumia mianya ya umasikini wa baadhi ya viongozi na taasisi kujipenyeza na kupenyeza rupia zao.

Ninajaribu kujiuliza ni makampuni mangapi janjajanja yanatumia speed ya Raisi kujipenyeza kama malaika ilhali waliyoyafanya nyuma wanayajua wao na baadhi ya viongozi.

Amini usiamani, kama Ayi Kwei Armah alivyo andika baada ya mapinduzi kufanyika Ghana, hata katika Ghana mpya hapakuwa na mazuri wala wazuri. Vivyo hivyo kwa Tanzania ya mapinduzi ya awamu ya 5, wazuri bado hawajazaliwa kwani mfumo bado unatoa fursa kwa daraja la wajanja wapya kuibuka na kufanikiwa. Vile vile kuna viongozi matajiri wapya wanaibuka kwenda kujiunga na ligi ya wakina Lowassa, Ridhiwani, Sumaye n.k kutokana na mfumo huu wa serikali hii kwani hawa wako jikoni wanatazama bakuli la nyama muda wote.

Mchaka mchaka wa raisi Utawaogopesha baadhi ya wajanjajanja wasio na muunganiko na serikali au walioiudhi serikali na utawanufaisha wajanjajanja wenye muunganiko na serikali au wenye kuifurahisha serikali na kuisaidia kupunguza gharama kweye baadhi ya miradi yake.

"Even in the new regime, The Beautiful Ones are Not Yet Born" - Ayi Kwei Armah
Umeandika kile nilicho taka kuandika
46c14899bc689df125b71a9060b6a3b8.jpg
 
Hawa jamaa GSM...labda waingie kwa mlango mwingine wakitokea Congo lakini hii janja janja yao IPO kwenye radar kitambo mbona!
Acha warudishe sehemu ya kumi ya zile walizochuma kwa hila ili wapate thawabu zao.
 
Mkuu watanzania wana kipaji,
Ulimwengu unajua,
Tu wajanja mno na tena twajua kula na kipofu.
Hebu jiulize.
Nchi hii lini tuliwahi kupata neema?
Tunalalamika kila siku lakini maisha yanasonga...mtu hana kazi lakini kila siku yupo njwiiii na ana simu ya gharama.
 
Mmesahau uuzwaji wa nyumba za serikali? Pogba alifanya nn? Tulishawaambia kuwa ccm sio mtu bali mfumo.
Hakuna mzalendo ndani ya ccm. Huoni kinachoendelea bungeni wanavopitusha miswada ya kuwakandamiza watz na ione miccm inavoshabikia na kuunga mkono uchafu wote. Mpaka wanapewa rushwa na Ikulu ili kupitisha mambo......
Ccm hawajawahi kuwa na nia nzuri na watz
 
Mke wa RC huwa anaomekana sana Dom na gari 1 d/cabin mpyaaa, aliyopewa na GSM, mke wa jamaa huwa anakwenda sana kwa uwekezaji wa maeneo. mojawapo ni kule maeneo ya UDOM na NALA.
 
Mmesahau uuzwaji wa nyumba za serikali? Pogba alifanya nn? Tulishawaambia kuwa ccm sio mtu bali mfumo.
Hakuna mzalendo ndani ya ccm. Huoni kinachoendelea bungeni wanavopitusha miswada ya kuwakandamiza watz na ione miccm inavoshabikia na kuunga mkono uchafu wote. Mpaka wanapewa rushwa na Ikulu ili kupitisha mambo......
Ccm hawajawahi kuwa na nia nzuri na watz
Siasa za hawa jamaa nahisi zina msaada mkubwa sana wa shetwani! kwani mambo mengine kwa roho ya kawaida ya binadamu haiwezekani hadi upate 'msaada wa shetwani aisee!
 
Mupe....Muruke..
Yule Mupe Wine.. Yule Mupe Bia. ..Yule Mupe Soda...Yule Muruke....Yule Mupe Maji...Yule Mupe Kiroba

Yule Usimupe Maana Amezamia
 
Sasa hivi ni zamu ya wengine...mengine yote ni mbwembwe/maigizo tuu za siasa....tena sasa hivi wenye zamu wanatumia amri tuu!....ukileta ubishi unafitiniwa tuu kisha unatumbuliwa
 
Unajua wakati raisi anaingia madarakani nilijua kuwa ndio wakati hakuna mtu yoyote atatia mkono kwenye bakuli la nyama la serikali na kujichotea minofu, hakuna mtu atapata "upendeleo" kutoka serikalini, hakuna mtu atafanya mambo kwa nyodo kwani serikali ya awamu ya 5 haina "undugu/ushkaji/urafiki"

Mweeeee kumbe sio bwana, watu walishachungulia mapungufu na kuchukua fursa hiyo. nimeona uzi nyingi humu juu ya GSM mwaka juzi ikijulikana kama Home Shopping Center. Mwishoni mwa mwaka 2015, Home Shopping walitangaza kufilisika na kufunga kampuni lao hilo, kisha mwanzoni mwa 2016 wakaja na kampuni jipya la GSM wakiambatanisha na Charity yao ya GSM Foundation ambayo ninakiri kwa kinywa changu kuwa inafanya kazi kubwa katika upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa nchi nzima, kazi nzuri sana.

Hawa GSM ndio wafadhili wa mabango ya kampeni ya kupanda miti Dar nzima, na kumbuka kampeni hii ilikuja na makonda baada ya upinzani kuamsha joto la UKUTA.

GSM ndio wafadhili wa ziara ya Paul Makonda juzi juzi kuzunguka Dar, kuna magari yalikuwa yana nembo ya GSM yalikuwa yanamsaidia Mkuu wa Mkoa kupunguza gharama za PA.

Hata ziara ya Makonda na mkwewe Marekani ninahisi GSM wamemsaidia kupunguza gharama za matumizi kidogo. Kwani nilipoona Makonda yupo New York, Los Angeles na Springfield Massachusetts kuna baadhi ya mameneja wa GSM wapo miji hiyohiyo, ikawa inanibidi nianze kuunganisha nukta zangu moja baada ya moja mpaka hapo walipo amua kupiga picha ya pamoja na kujiita Class sehemu moja.

Hata kuna tetesi za "vijiweni" kuwa kuna ndugu wa hao jamaa wa GSM aliswekwa kituo cha polisi kwa kosa la uvutaji shisha, akapiga simu moja tu, wakatolewa kituo kizima hata waliokuwa central kwa makosa tofauti wakapata msamaha wa ndugu wa jamaa wa GSM, mwishoni mwa mwaka 2016. Habari za vijiweni zinasema jamaa wa GSM wanapata kaupendeleo sana kwenye baadhi ya mambo kwani wanajitoa sana pia kwa serikali ya mkoa.

Swali kubwa ninalo jiuliza ni kuwa, Home Shopping/GSM wanatoa misaada kwa Tanzania, Dar es Salaam na ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kwa Mkuu wa Mkoa bure bila return yoyote? Wanarudisha kwa jamii pasipokuhitaji mrejesho wowote?

Kama Home Shopping ilifilisika, GSM wanapata wapi fedha za Charity na kuisadia Serikali ya mkoa na mkuu wa mkoa? Usiniambie ile stunt iliyofanywa na wasanii wa bongo fleva Diamond na Ali Kiba kumpa msaada mkurugenzi wa GSM kama mchango kuiwezesha GSM Foundation.

Ninahisi wakati "baadhi" ya mafisadi na wakiondolewa kwenye ulaji na mirija ya asali na maziwa kuna baadhi wanatumia mianya ya umasikini wa baadhi ya viongozi na taasisi kujipenyeza na kupenyeza rupia zao.

Ninajaribu kujiuliza ni makampuni mangapi janjajanja yanatumia speed ya Raisi kujipenyeza kama malaika ilhali waliyoyafanya nyuma wanayajua wao na baadhi ya viongozi.

Amini usiamani, kama Ayi Kwei Armah alivyo andika baada ya mapinduzi kufanyika Ghana, hata katika Ghana mpya hapakuwa na mazuri wala wazuri. Vivyo hivyo kwa Tanzania ya mapinduzi ya awamu ya 5, wazuri bado hawajazaliwa kwani mfumo bado unatoa fursa kwa daraja la wajanja wapya kuibuka na kufanikiwa. Vile vile kuna viongozi matajiri wapya wanaibuka kwenda kujiunga na ligi ya wakina Lowassa, Ridhiwani, Sumaye n.k kutokana na mfumo huu wa serikali hii kwani hawa wako jikoni wanatazama bakuli la nyama muda wote.

Mchaka mchaka wa raisi Utawaogopesha baadhi ya wajanjajanja wasio na muunganiko na serikali au walioiudhi serikali na utawanufaisha wajanjajanja wenye muunganiko na serikali au wenye kuifurahisha serikali na kuisaidia kupunguza gharama kweye baadhi ya miradi yake.

"Even in the new regime, The Beautiful Ones are Not Yet Born" - Ayi Kwei Armah
Usijisumbue kuleta vitu ambavyo washajua muda mrefu. Binafsi simuoni RC akimaliza miaka mitano bila kutumbuliwa.
 
Back
Top Bottom