Mfumo wa Rais Unatengeneza Kundi Jipya la Janjajanja na Wala Nchi kwa Mgongo wa Kuisaidia Serikali

mwanaapolo

JF-Expert Member
Mar 14, 2014
256
195
Unajua wakati raisi anaingia madarakani nilijua kuwa ndio wakati hakuna mtu yoyote atatia mkono kwenye bakuli la nyama la serikali na kujichotea minofu, hakuna mtu atapata "upendeleo" kutoka serikalini, hakuna mtu atafanya mambo kwa nyodo kwani serikali ya awamu ya 5 haina "undugu/ushkaji/urafiki"

Mweeeee kumbe sio bwana, watu walishachungulia mapungufu na kuchukua fursa hiyo. nimeona uzi nyingi humu juu ya GSM mwaka juzi ikijulikana kama Home Shopping Center. Mwishoni mwa mwaka 2015, Home Shopping walitangaza kufilisika na kufunga kampuni lao hilo, kisha mwanzoni mwa 2016 wakaja na kampuni jipya la GSM wakiambatanisha na Charity yao ya GSM Foundation ambayo ninakiri kwa kinywa changu kuwa inafanya kazi kubwa katika upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa nchi nzima, kazi nzuri sana.

Hawa GSM ndio wafadhili wa mabango ya kampeni ya kupanda miti Dar nzima, na kumbuka kampeni hii ilikuja na makonda baada ya upinzani kuamsha joto la UKUTA.

GSM ndio wafadhili wa ziara ya Paul Makonda juzi juzi kuzunguka Dar, kuna magari yalikuwa yana nembo ya GSM yalikuwa yanamsaidia Mkuu wa Mkoa kupunguza gharama za PA.

Hata ziara ya Makonda na mkwewe Marekani ninahisi GSM wamemsaidia kupunguza gharama za matumizi kidogo. Kwani nilipoona Makonda yupo New York, Los Angeles na Springfield Massachusetts kuna baadhi ya mameneja wa GSM wapo miji hiyohiyo, ikawa inanibidi nianze kuunganisha nukta zangu moja baada ya moja mpaka hapo walipo amua kupiga picha ya pamoja na kujiita Class sehemu moja.

Hata kuna tetesi za "vijiweni" kuwa kuna ndugu wa hao jamaa wa GSM aliswekwa kituo cha polisi kwa kosa la uvutaji shisha, akapiga simu moja tu, wakatolewa kituo kizima hata waliokuwa central kwa makosa tofauti wakapata msamaha wa ndugu wa jamaa wa GSM, mwishoni mwa mwaka 2016. Habari za vijiweni zinasema jamaa wa GSM wanapata kaupendeleo sana kwenye baadhi ya mambo kwani wanajitoa sana pia kwa serikali ya mkoa.

Swali kubwa ninalo jiuliza ni kuwa, Home Shopping/GSM wanatoa misaada kwa Tanzania, Dar es Salaam na ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kwa Mkuu wa Mkoa bure bila return yoyote? Wanarudisha kwa jamii pasipokuhitaji mrejesho wowote?

Kama Home Shopping ilifilisika, GSM wanapata wapi fedha za Charity na kuisadia Serikali ya mkoa na mkuu wa mkoa? Usiniambie ile stunt iliyofanywa na wasanii wa bongo fleva Diamond na Ali Kiba kumpa msaada mkurugenzi wa GSM kama mchango kuiwezesha GSM Foundation.

Ninahisi wakati "baadhi" ya mafisadi na wakiondolewa kwenye ulaji na mirija ya asali na maziwa kuna baadhi wanatumia mianya ya umasikini wa baadhi ya viongozi na taasisi kujipenyeza na kupenyeza rupia zao.

Ninajaribu kujiuliza ni makampuni mangapi janjajanja yanatumia speed ya Raisi kujipenyeza kama malaika ilhali waliyoyafanya nyuma wanayajua wao na baadhi ya viongozi.

Amini usiamani, kama Ayi Kwei Armah alivyo andika baada ya mapinduzi kufanyika Ghana, hata katika Ghana mpya hapakuwa na mazuri wala wazuri. Vivyo hivyo kwa Tanzania ya mapinduzi ya awamu ya 5, wazuri bado hawajazaliwa kwani mfumo bado unatoa fursa kwa daraja la wajanja wapya kuibuka na kufanikiwa. Vile vile kuna viongozi matajiri wapya wanaibuka kwenda kujiunga na ligi ya wakina Lowassa, Ridhiwani, Sumaye n.k kutokana na mfumo huu wa serikali hii kwani hawa wako jikoni wanatazama bakuli la nyama muda wote.

Mchaka mchaka wa raisi Utawaogopesha baadhi ya wajanjajanja wasio na muunganiko na serikali au walioiudhi serikali na utawanufaisha wajanjajanja wenye muunganiko na serikali au wenye kuifurahisha serikali na kuisaidia kupunguza gharama kweye baadhi ya miradi yake.

"Even in the new regime, The Beautiful Ones are Not Yet Born" - Ayi Kwei Armah
 
Attachments

naan ngik-kundie

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
1,771
2,000
Umenena vyema mkuu lakini huu mtandao ni mkubwa unahitaji mtu ambaye ana uzalendo kweli kweli ata tukimtazama sura yake kweli ionyeshe uzalendo wake. Lakini si mtu wa kusimama mbele yetu na kutuambia mimi ni mzalendo wa Kweli na mtetezi wa wanyonge wakati moyoni hana uzalendo wowote.
 
Lil G

Member
Dec 15, 2014
83
125
Watakukebehi sana humu kwa ajiri ya huu UZI....ila ulioyasema tutayaona tu.

Ukipata nafasi muda mwingine ebu connect dots za huyo jamaa kupewa hicho cheo na kuachwa mjini.
 
NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,536
2,000
Maskini hana jeuri, omunaku tatamwa, ukiwa fukara, punguza jaziba ili matajiri wakusaidie
 
aroro

Member
Jan 2, 2017
12
20

Upo deep sana mkuu
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,812
2,000
Nimependa ulivyoyaandika, ila ndio hivyo lazima qengi wanakula na nchi ni yao.
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,070
2,000
Bora yule DC wa Kinondoni aendelee kushika hiyo nafasi ingawa wanafanana at least ameonesha kutatua matatizo ya msingi ikiwemo hili la wanafunzi 18000 kukosa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza kwa kuwalazimisha Zantel kulipa fedha na kuzielekeza kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
7,718
2,000
Kwa hizo hoja uliyosema. Kama ni mechi CCM mmewapiga+chali. Hawana hoja za kutoka hapo na kama maisha na mwenyewe yamemgonga*rais anafanya kazi kubwa tumsaidie na yeye mpk Sasa kama ni ufisadi pia amejitahidi kusambaza*nao.. Ufisadi wa LUGUMI imetokea awamu Yake no actions
 
Ally Kanah

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
1,480
1,500
Umenena vyema mkuu lakini huu mtandao ni mkubwa unahitaji mtu ambaye ana uzalendo kweli kweli ata tukimtazama sura yake kweli ionyeshe uzalendo wake. Lakini si mtu wa kusimama mbele yetu na kutuambia mimi ni mzalendo wa Kweli na mtetezi wa wanyonge wakati moyoni hana uzalendo wowote.
Mkuu ni kweli kabisa tunahitaji mzalendo kama Lowassa vile maana Lowassa ni mzalendo haswa na mtetezi wa wanyonge na moyoni mwake sio jambazi/fisadi bali ni mzalendo haswa hata tunapomuangalia Lowassa usoni tunauona kabisa uzalendo wake
 
naan ngik-kundie

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
1,771
2,000
Mkuu ni kweli kabisa tunahitaji mzalendo kama Lowassa vile maana Lowassa ni mzalendo haswa na mtetezi wa wanyonge na moyoni mwake sio jambazi/fisadi bali ni mzalendo haswa hata tunapomuangalia Lowassa usoni tunauona kabisa uzalendo wake
Ni mtazamo wako pia na siwezi kukupinga maana una haki ya ku share mawazo/mitazamo yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom