Mfumo wa Majimbo(Counties) vs Mikoa na Wilaya, upi wenye gharama kubwa katika kuendesha Serikali?

Very well said.... Tumeambiwa kwenye Kuraani.... Itafuteni elimu hata ikibidi kwenda mpaka China, kwa hakika mola wetu ni mjuzi wa kila kitu....
 
Itakua unatatizo la uelewa alichokushauri jamaa ni kua tafuta nauli utembee upate exposure ya jinsi hayo majimbo yalivyo na tawala zake hajakwambia kwamba uende sehemu ingine ukahamie ili uwe mjanja yawezekana unatatizo la kuelewa vitu naona
 
Mkuu kwenye mfumo wa central government, kwanza kikundi cha watu wachache ndo wana dictate kila kitu , watu wenye vision na strategies nzuri hawana nafasi... Maana wakipewa nafasi watawafunika hao wanaojifanya wajuaji..
 
Hatuna tatizo la ukabila kitaifa mkuu!.. Tuna hilo tatizo kwenye ngazi za chini na litakuwa kubwa tukitenga hizo county!..
Kuna kipindi Magembe alishutumiwa kupeleka Bajeti yote ya maji kama 30 bln wilayani kwake. Tumeona miradi ya maendeleo ikipelekwa kikanda. Kwa hiyo hata kama tatizo la ukabila kitaifa ni dogo lakini ndilo lenye impact kubwa sana katika kugawana pesa za maendeleo. Hili la ukabila kwa ngazi za chini ni kweli upo lakini impact yake ni ndogo, maana hata leo si upo. Tukiweka sheria ndogondogo tunaweza kuudhibiti ila hauna nguvu ya kutuzuia kuvuna faida za decentralization.

Kusema mikoa mingine itakuwa nyuma, hata sasa mikoa kama Singida na Lindi ipo nyuma. Ugatuzi utasababisha magavana hao kuchangamka kutafuta njia mpya za kukuza uchumi kitu ambacho wakuu wa wilaya na mikoa hubweteka. Pia mfano kenya kwenye utaratibu wao wa kugawana pato la taifa kuna kipengele kuwa unaongezewa kiasi fulani kama kiwango chako cha umaskini kipo juu sana. Pia kama kuna watu wana potential ya kwenda mbali ni hasara kuwazuia kwa kigezo cha kuleta usawa.
 
Unapoamua kutoa elimu jifunze kuonyesha faida na hasara au madhala ikiwezekana kwa mifano. Halafu unatoa mapendekezo au unawaachia unaowafundisha wajadiri na kukuliza kama wana cha kukuliza.
Yeye ametimiza wajibu wake kwa kuweka faida anazozijua za mfumo wa Majimbo. Wewe weka hasara Kama wazijua....
 
Nigeria,Afrika ya kati,Sudan hadi wakatengana kukawa na Sudan mbili,Kongo DR
Ambacho huelewi mkuu ni kuwa nchi nyingi kama Nigeria huingia kwenye mfumo wa majimbo ili kuzuia kutengana. Iko hivi mfumo huu huzuia kutengana na si kuleta utengano. Nchi kama Mynamar inafikiria kuwa kuweka mfumo wa majimbo sababu ya machafuko yaliyosababishwa na centralized system.
 
Unapoint mkuu. Ila sidhani kama hilo la county ya Kenya ni kweli maana ni kinyume na sheria za nchi. Pia sida ya hizi halmashauri zetu wateuliwa ambao ni MaDC na Wakurugenzi hawawajibiki kwa wananchi bali kwa Rais. Hao ndiyo wanapanga na kusimamia shughuli za maendeleo hasa halmashauri ikiwa chini ya upinzani, madiwani huwa kama vikaragosi tu. Ndiyo maana halmashauri ya ujiji ilipopata hati chafu aliwajibishwa Mkurugenzi.
 
Acheni mawazo ya kijima na ulaghai wa watawala.... Eti Lindi na Mtwara wataachwa!!! Gesi iliyogunduliwa iko wapi? Zamani hata multi party mlidanganywa italeta vurugu Kama Rwanda... Nyerere akawapinga
 
Acheni mawazo ya kijima na ulaghai wa watawala.... Eti Lindi na Mtwara wataachwa!!! Gesi iliyogunduliwa iko wapi? Zamani hata multi party mlidanganywa italeta vurugu Kama Rwanda... Nyerere akawapinga
Hao jamaa ni matajiri sana. Uchumi wa gesi na korosho ni utajiri mkubwa. Nchi kama Rwanda ni ndogo kuliko mkoa wa Mbeya na una rasilimali chache kuliko Mbeya japo ina watu wengi. ila Rwanda ina GDP kubwa karibu mara kumi ya Mbeya. Tatizo hapo ni kuwa rasilimali za Rwanda ziko Managed kwa efficiency kubwa sana. Ndiyo ilivyo mfumo wa county/majimbo huongeza ufanisi kwenye usimamizi wa rasilimali. Unaweza kuta kwenye huo mfumo Lindi na Singida zikawa na uchumi mkubwa kuliko mikoa inayoonekana imejaliwa.
 
Acheni mawazo ya kijima na ulaghai wa watawala.... Eti Lindi na Mtwara wataachwa!!! Gesi iliyogunduliwa iko wapi? Zamani hata multi party mlidanganywa italeta vurugu Kama Rwanda... Nyerere akawapinga
Nilitaka kukupinga lakini nilipogundua nipo Jukwaa la Siasa, ulichoandika kinafaa humu!..
Ukipata fact rudi nitagg!.
 
utapigana ili ukapore kwenye jimbo la wenzio au? toa na mifano hai wapi wana utawala wa majimbo then wengine wameenda kupambana kwenye jimbo jirani!

Je huoni kama mfumo uliopo ndio utapelekea kupotea kwa amani? kama sehemu zenye viongozi zinapewa attentions na zisizo na viongozi zinapuuzwa Pomona na kuwa na resources? Hebu toka nje ya karai sail in the see!
 

Please usilete ya Kenya katika nchi yetu! Angalia Kenya wamegawa kwa majimbo(counties) ukabila mtupu, makabila 44 kila kabila na county yake,labda tuweke kwa kanda(zone) five zones to avoid tribal issues.
 
Hasara za huu mfumo ni kuwa gharama za uendeshaji huwa ni kubwa na unaweza chochea ukabila usipoangaliwa vizuri.

Unahisi mfumo kama huu unaweza kutufaa Tanzania?

cc Malcom Lumumba zitto junior Palantir MSEZA MKULU

Mkuu Giant,
Kubwa zaidi ni kwamba kabla ya kuiga kitu hata kama kiwe ni kizuri kiasi gani na kinapendeza macho, hebu tujaribu kupima kwa mapana ili kuona jinsi gani huu mfumo umewaletea Kenya faida na changamoto zipi wamezipata. Mambo ya Kenya yanaweza kufanana na Tanzania lakini yasiwe sawa (SIMILAR BUT NOT EQUAL) . Inapaswa tujiulize swali (Empirical Question)la msingi kabisa kwamba WILL IT WORK WITH US ??? Umezungumzia changamoto kubwa mbili kwenye huo mfumo wa Kenya ambazo ni kuchochea Ukabila na Gharama za uendeshaji. Je, Tanzania na sisi tutakuwa na changamoto hizi mbili tu au kwetu zitaongezeka mara dufu ??? Hili swali ndiyo juzi nimezungumza na ndugu yangu zitto junior , hapa inabidi tufanya EMPIRICAL STUDY kwa kuchambua taarifa zetu ili tuangalia kama huu mfumo utakuwa na faida au hasara kwetu.

Mosi,
Hilo suala la Ukabila niseme tu kwamba kwasasa lipo lakini siyo changamoto kubwa sana kiutawala hapa nchini kwetu kama ambavyo lipo nchini Kenya. Lilikuwa ni kipaumbele cha Serikali ya Mzee Nyerere kwa zaidi ya miaka 23 na nikiri tu kwamba alifanikiwa kwa Asilimia 85% katika kupambana nalo. Muhimu kabisa siyo kwa mtu kutoajiri mtu wa kabila lake lakini ni ile hali ya kujijengea akili ya kutambagua mtu yeyote aitwae Mtanzania akiwa mbele yako. Leo hii mimi nimefanya kazi katika Ofisi ilikuwa imejaa Wachagga lakini zaidi ya kuwatania tu, sikuwahi kujihisi kama mimi ni mpweke ndani ya ile ofisi kwasababu walikuwa wananijali kama ndugu yao wa damu kuliko hata ambavyo watu wa kabila langu wangenipenda. Tanzania tumejengewa huo utamaduni wa kutomhukumu mtu katika minajili ya Ukabila wake,ndiyo maana hata leo hii Mkuu Giant mimi wewe sina haja ya kulijua hata kabila lako lakini ninachojua ni kwamba mimi na wewe tumekuwa marafiki ambao ni kama ndugu.

Nchini Kenya Ukabila ni sehemu ya falsafa ya kitaifa ambayo ilijengwa tangia awamu za Mzee Jomo Kenyatta na Mzee Moi. kibaya zaidi ni kwamba wakenya wenyewe walikubaliana kabisa na huo mfumo kwamba kuna nafasi maalum za Wajaluo na nafasi maalum za Wakikuyu: Hili limeenda hadi kufikia sehemu kwamba nchi inashindwa kuwa na umoja wa kitaifa kwasababu ya huu Ubaguzi. Angalia vita vyao vya mwaka 2007-2008 vilikuwa ni vya kikabila, imefikia hadi kipindi vyama vya kisiasa vinakuwa katika mwamvuli wa Kabila (Hii ni hatari sana kwa taifa changa kama Kenya). Lakini kinachotia moyo ni kwamba hiki kizazi kipya cha wasomi wa Kenya waliona hilo tatizo la Ukabila na wakaanza kukataa ndiyo kupelekea hayo mabadiliko ya Kikatiba. Hivyo naweza kusema kwamba One of the push factor for Constitutional change in Kenya is a need to address the challenge of tribalism.

Haya turudi kwenye swali letu la msingi,
Je, Ukabila ni tatizo kubwa sana nchini Tanzania kama ambavyo ni tatizo la kimfumo (Systematic Problem) nchini Kenya ? Kama jawabu ni Ndiyo basi nashauri tuendelee kubaki na huu mfumo wetu wa sasa kwasababu umefanikiwa kudumisha Amani, Umoja na Upendo hapa nchini tokea tumepata Uhuru. Lakini kama jawabu ni Hapana basi nauliza kwanini tufanye siasa za woga kwa kujitengenezea vichwani mwetu matatizo ambayo hayapo ? Mtazamo wa haraka watanzania tumeingiliana sana na kizazi cha kwanza na cha pili kinapotea kinabaki kizazi cha tati (SISI) ambao hatuhusudu kabisa Ukabila na Ukanda. Hivyo kama huu mfumo wa majimbo unaweza kuleta faida kubwa za kiuchumi kuliko hasara kwanini tuogope kuutumia hapa nchini kwetu ? Kubwa ni kwamba Ukabila utakuwa na nafasi ndogo sana kwasababu majimbo hayawezi kujiamulia tu kama yanavyotaka na isitoshe tutaweka mfumo madhubuti kabisa kwamba wafanyakazi wasiochaguliwa wa hizi Halmashauri watalipwa na Serikali kuu.

Hapa sioni kama kuna jimbo litajaribu kusumbua kwasababu yatakuwa Semi-Autonomous na kama yanataka kupitisha mradi mkubwa basi ni lazima mradi huo uangaliwe na Serikali kuu sambamba na kuangalia kama una maslahi mapana kwa taifa letu. AU Serikali kuu inaweza ikaamua kugawana majukumu na hizi Serikali za Majimbo ambapo yenyewe inaweza ikabaki na kazi kubwa kama Ulipaji wa mishahara, Ukusanyaji wa Kodi, Uwekezaji,n.k lakini mambo mengine kama miradi ya barabara, usimamizi wa elimu,kilimo, usimamizi wa afya n.k yakaachiwa majimbo yafanye yenyewe na kujiendesha yenyewe.

Pili,
Suala la gharama katika uendeshaji wa shughuli za kiserikali naomba nisema tu haya yafuatayo: Hii ni changamoto lakini tunaweza kuizuia kama tu nchi itatambua vipaumbele vyake, kubana matumizi na kuongeza nguvu ya ulazishaji kuanzia ngazi ya chini. Kifupi nakubaliana na msemo kwamba Serikali isianze na wafanyakazi wengi na mishahara mikubwa kabla ya nguvu ya uzalishaji kuongezeka katika hayo majimbo. Hivyo hakutakuwa na gharama za uendeshaji wa Serikali kama kuna uwiano wenye afya baina ya nguvu ya uzalishaji wa Serikali hizo na ukubwa wa serikali hizo. Tusipojibebesha mzigo mkubwa hatuwezi kukutana na mambo kama Retrenchment of Workers and Heavy Taxation. Hivyo tujiulize kwamba tuna vyanzo vya kutosha kuwezesha serikali ya kila jimbo kujiendesha vizuri na kutimiza majukumu yake kwa kiwango kikubwa na kinachostahili kama ilivyo sasa ???

Tatu,
Changamoto kubwa ambazo Tanzania inabidi tuziogope kutokana na huu mfumo wa majimbo ni Rushwa, Utakatishaji wa fedha, Matumizi mabovu yasiyo na tija ndani ya Serikali na Usimamizi mbovu wa rasilimali za nchi. Haya ndiyo matatizo makubwa ambayo serikali ya Tanzania inapambana nayo tokea tumepata Uhuru mpaka leo hii. Hadi kufikia mwaka 2014 zaidi ya Asilimia 30% ya Pato la Taifa ilikuwa inapotelea kwenye Rushwa. Hebu tujiulize kama kukiwa na majimbo yanayojitegemea hili tatizo litakuwa kubwa kiasi gani hapa nchini ??? Tutalikabilije sisi ??? Haya ya matumizi mabovu yasiyo na tija na Usimamizi mbovu wa rasilimali za Ummah hayani haja kuelezewa sana kwasababu mifano iko wazi kabisa. Trilioni 1.5 inapelekwa kwenye matumizi mengine bila ruhusa ya Bunge na wala hakuna anayejali kabisa, hili ni changamoto kubwa sana. Mikataba mibovu isiyo na tija kwa taifa ndiyo mingi usiseme: Je, tukianzisha huu mfumo wa majimbo unadhani hata matatizo yatakuwa yamepungua au yameongezeka zaidi ??? Inabidi tujiangalie kama Taifa jinsi gani tunaweza kuzikabili changmoto zetu.

NB 1: Hivyo basi nasema kwa Tanzania Changamoto zetu kuu zitakuwa ni:
1. Rushwa na Ufisadi uliokithiri
2. Utakatishaji wa fedha
3. Matumizi mabaya ya mali za Ummah (V8 hadi kwa kila kiongozi)
4. Usimamizi mbovu wa mali za Ummah (Mikataba mibovu, Usimamizi mbovu wa mifumo ya elimu na afya)
5. Kuchanganya Siasa na Utaalamu (UCCM, UCHADEMA na UCUF kwenye utendaji wa kitaifa)
6. Ukabila na Ukanda (Haya yapo lakini siyo makubwa kivile kwa Tanzania yetu ya sasa japo kuna watu wanataka kuleta)
7. Gharama kubwa za uendeshaji wa serikali.

NB 2: Wenzetu wa Kenya tatizo la Ukabila ndiyo litakuwa la kwanza Kabisa juu ya hayo matatizo ambayo nimeyataja.
Hivyo basi The EMPIRICAL QUESTION: WILL THIS WORK ??? litajibiwa zaidi kwa kukusanya taarifa nyingi kuhusu mfumo wa Tanzania huku tukizichambua kuona ni jinsi gani mfumo huo wa Kenya unaweza kufanya kazi nchini Tanzania.

CC: Palantir , chige , Consigliere , James Comey , TUJITEGEMEE , Nalendwa , SirChief , Graph Theory , Richard
 
Mkuu Malcom Lumumba,

Huu mjadala ni nyeti sana na unahitaji uchambuzi wa kutosha kama ulivyofanya.

Binafsi nitarudi baadae kuongea kwa kirefu lakini kwa sasa nitaongea kifupi sana.

Linapokuja suala la majimbo; binafsi naunga mkono!

Hata hivyo, binafsi sipo interested KABISA na Administrative Zones per se bali ningependa tuwe na Economic Zones!

Aidha, if possible, criteria ya ku-point zone husika isiwe geographical location bali physical characteristics!

Kwa maana nyingine, I don't mind kama Kilimanjaro na Lindi zinakuwa zone moja provided zina-share major physical features.

BRB...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…