Kwa mfumo uliopo Mkuu wa Mkoa na Wilaya hakuna maendeleo wanaweza leta

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,517
8,760
Mfumo wa Utawala wa hii nchi ni Centralized kwa maana kwamba maamuzi yote yanafanyika juu then ndio yanaanza kushuka chini na hakuna maamuzi yanayo anzia chini kupanda juu.

Wakija wawekezaji vibari na kila kitu vinatolewa juu na sio chini, Mipango ya maendeleo inasukwa juu then inashuka chini, sasa tukiaminishwa kwamba wakuu wa wilaya na mikoa kuna maeneleo wanaweza leta ni kudanganyana tu.

Sana sana ni kupiga misele na magari na kwrnda kusweka wafanya kazi ndani au kuwatishia kuwaweka ndani, Sasa Mkataba wa mradi unasainiwa Dar es salaaam au Dodoma, Wakati mkataba wa mradi fulani unasainiwa hao wakuu wa mikoa na wilaya hawajahusishwa, sasa how come waanze kusimamia miradi ambayo wao hawajui hata mikataba inasemaje?

Wakuu wa wilaya zaidi ya kazi za kufungua waasha, semina na makongamano hawana kazi za kufanya wala hawana maamuzi ambayo yanaweza leta maendeleo.

Kwa katiba ya nchi kama Kenya wana kitu kinaitwa County,ambapo kwa sasa county zina ongozwa na Magavana walio chaguliwa na wananchi, zile county zina bajeti yao ya kikatiba sio ya hisani na kila Gavana anapanga jinsi ya kutumia pesa kwenye jimbo husika.

Huo mfumo tukiambiwa kwamba Gavana analeta maendeleo ni sawa kabisa ila sio huu mfumo wetu wa kijamaaa.

Mikoa haina bajeti zao za kikatiba ambazo ni za maendeleo kwba basi mkuu wa mkoa awe anakaaa ba wakuu wa wilaya wanapanga maendeleo ya mkoa husika.

Mipango inapangiwa kule Dodoma
 
NJE YA MADA:
Kuna mtaa nilipita uko Kasulu Mjini Mkoa wa Kigoma unaitwa MURUSI..
 
Back
Top Bottom