SoC03 Mfumo wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili-KIDGUS

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
996
1,511
UTANGULIZI
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la vitendo viovu vya kulawiti, ama kuwabaka watoto wadogo, na vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na watu wa karibu walioaminiwa na kupewa dhamana ya kuwahudumia watoto hao kama walimu na walezi wao katika mazingira ya shule zao ama makazi yao, na mara nyingine ndani ya vyombo vya usafiri wa shule.

Mpaka sasa hakuna njia mbadala iliyoweza kuhakikisha kwamba watoto watakuwa salama, bali kwa kudra za mwenye enzi. Kwa karne ya leo Teknolojia ina uwezo wa kujibu maswali mengi na kuleta suluhu ya changamoto mbalimbali.

Hili ni wazo la kiteknolojia ambalo litahakikisha watoto wengi wanakuwa salama wawapo katika mazingira ambayo yanahitaji uangalizi.

MUUNDO WA MFUMO
Mfumo huu utahusisha;

Simu janja ajili ya App ambayo itatumika kukamilisa mawasiliano kati ya mzazi au mlezi na saa janja atakayovalishwa mtoto.

Mfumo wa kompyuta utakuwa na sehemu muhimu mbili ambazo ni “Main controllerambayo itatumiwa na kitengo maalumu cha jeshi la polisi chenye dhamana ya kusimamia masuala husika kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii “Main controller” ndio atakuwa msimamizi wa mifumo yote katika taasisi ambazo itasimamiwa na “Sub-controlers” sehemu hizi zitapatikana ndani ya kitufe kiitwacho “Monitor”.

Kitufe cha “Sub-controllers” kitatumiwa na waongoza mfumo katika taasisi zinazohusika na malezi kama vile shule, vituo vya watoto yatima, mfumo utazuiwa kwa pasi kodi ambazo itakuwa ni lazima zithibitishwe kwa kupitia msimbo ambao utatumwa katika simu ya muongozaji kipindi anapoingia, lengo ni kuzuia taarifa kufutwa kwa lengo la kupoteza ushahidi.

Kamera yenye kutumia mtamdao wa intaneti itakayotumia laini ya kielektroniki kwa ajili ya kuwezesha intaneti, zitafungwa ndani ya magari yote ya shule, madarasani, na mabwenini na itarekodi matukio yote sehemu husika, kamera ya kwenye gari za shule itatumia umeme wa gari.

Saa janja itakuwa na kamera ambayo haitaweza kuonekana na itakuwa inarekodi matukio yote wakati wote, itatumia laini ya kielektroniki kwa ajili ya kuwezesha mtandao, itakuwa na uwezo wa kuzuia vimiminika kuiathiri, zitakuwepo za aina mbili, zile zinazotumia mfumo wa Android na IOS, zitaweza kufanya kazi katika simu yoyote ile inayoendana na mfumo wake.

App itakuwa na uwezo wa kuhifadhi video, picha na sauti ambazo zimerekodiwa na saa itapatikana katika mifumo yote ya Android na IOS.

UTENDAJI KAZI.
Saa janja
itarekodi matukio yote yanayoendelea katika mazingira aliyopo mtoto, itagundua matukio yote hatarishi kwa mtoto ama yale yanayoonekana si ya kiungwana kwa mtoto kisha kutuma taarifa kwenye simu ya mlezi kupitia App maalumu, simu ya muhusika itaita kwa mlio maalum ambao yeye atautambua kwa lengo la kumpatia taarifa, atakapotazama kupitia app ya simu yake ataona kila kinachoendelea hivyo inakuwa rahisi kufanya maamuzi, pia itataunganishwa na mfumo wa kompyuta

App itakuwa na kitufe maalumu kinachoitwa “Report” kitakachotumika kuripoti tukio linaloonekana, kikiguswa yatatokea machaguo mawili ambayo ni “School” na “Police” uchaguzi utafanywa kulingana na wapi unataka kuripoti tukio.

Saa janja Kila inapofunguliwa ili ivuliwe mkononi, simu ya mlezi itakuwa ikipiga kelele mfululizo na katika mfumo wa kompyuta watapata taarifa kwa sababu kuondolewa kwa saa mkononi kutasomeka kama ni hatari inatokea kwa mtoto, itavuliwa baada ya mzazi kusitisha mawasiliano kati ya saa janja na App ya simu kwamba anaweza kusimamiwa kawaida, na kwa upande wa shule itavuliwa wakati maalum tu utakaotengwa kwa shughuli maalumu kama kuoga.

Kamera za kwenye gari ya shule, madarasa na mabweni zitakuwa zikirekodi matukio yote ya ndani ya gari, na matukio yote yatatumwa katika mfumo wa kompyuta na kuhifadhiwa, pia zitakuwa na uwezo wa kupiga picha katika matukio yote ambayo sio sahihi kufanyika kwa mtoto, upigaji huo utakuwa ukifanyika na kamera yenyewe pasipo kuamuliwa kwa kushirikiana na mfumo, muongoza mfumo hataweza kuizuia kamera isichukue matukio ila anaweza kuifanyia mpangilio ili kuboresha utendaji kazi.

Waongoza mfumo kazi yao itakuwa ni kuangalia kama kuna taarifa ya dharura iliyoingia kutoka pande zote saa janja ya mtoto na kamera katika gari za shule, madarasa na mabwenini.

Kupitia mfumo watoto watatambuliwa kupitia saa zao ambazo zitakuwa zimesajiliwa katika mfumo huo kwa kuhusisha nambari tambuzi ya saa, na kwenye mfumo taarifa ikiingia itaonesha jina la mtoto.

Kwenye mfumo wa kompyuta kutakuwa na sehemu inayoitwa “Monitor” katika hii ukifungua utaona vitufe viwili ambavyo “Main Controller” na “Sub-controllers”, ambapo ukifungua Sub-controller utaona vitufe viwili ambavyo ni “School/Centre” na “vans”, ukifungua “School/Centre” itakuletea machaguo ambayo ni “School” na “Centre” hapo utachagua kulingana na uhitaji wako, ukifungua chochote utakutana na vitufe viwili ambavyo ni “Classes “ na “Hostels”

Katika “Classses” kuna orodha ya madarasa yote na kwa kila darasa utaweza kuona shughuli inayoendelea kupitia video iliyopo pembezoni mwa darasa husika, kumfuatilia mtoto mmoja mmoja basi utabonyeza kitufe cha darasa husika kisha yatakuja majina ya watoto wote wa darasa husika na picha zao, ukigusa jina ama picha ya mtoto husika utamuona mubashara nini anafanya, na yupo wapi, na utaweza kumtambua yeyote aliyepo jirani yake, mtoto anapokuwa darasani kutakuwa na mawasiliano kati ya saa yake na kamera za shule pale tu utakapoanza kumfuatilia mtoto hapa kamera ya darasani italazimishwa na mfumo kumtafuta mtoto alipo kwa kuunganisha mawasiliano na saa ya mtoto.

Katika “Hostels” kuna vitufe “Male” na “Female”, ukifungua kimoja wapo itakupeleka kwenye hostel husika ambapo utapata majina ya ya mabweni, katika kila jina la bweni ukifungu utakuna na majina ya wanafunzi wote na namba ya kitanda wanavyotumia, ukifungua kitanda husika kamera ya ndani ya bweni itaitafuta saa ya mtoto husika na kuunganisha mawasiliano na hapo itaanza kuonesha video, mfumo utakuwa na uwezo wa kutambua kama mwanafunzi amejisitiri au la, na kama hajajisitiiri wenyewe utazificha sehemu zote ambazo hazipaswi kuonekana wazi kulinda utu wa mtu na hakuna mtu ataweza kuondo kimvuli kilichoficha sehemu husika.

Katika “Vans” kutakuwa na vitufe viwili ambavyo ni “Live stream” ambacho kitaonesha matukio ndani ya gari mubashara na “Gallery” ambacho kitaonesha matukio ya picha na video yaliyo rekodiwa

'Main controller
" kitatumiwa na jeshi la polisi ama ustawi wa jamii tu, ambapo muongozaji ataona majina ya taasisi zote ambazo zimeunganishwa na mfumo huo, na ataona alama katika sehemu ya taasisi husika ikiashiria uwepo wa taarifa flani ambayo anaweza kuipata kwa kugusa jina la taasisi husika na kumpeleka kwenye “Gallery” ambako taarifa inakuwa imeifadhiwa ikionesha jina la muhusika na tukio zima.

Katika kila mbele ya jina la taasisi kutakuwa na kitufe kimeandikwa “Evaluate” ambacho kikibonyezwa na kufunguka mfumo utaonesha vitufe viwili ambavyo ni “Minor” na “Major” ambapo katika“Minor” kuna majina ya watoto wote na ripoti zao za kiusalama, na “Major “ kuna ripoti kamili ya mwenendo wa mfumo, na matukio yote ya kiusalama katika taasisi husika.
 
Back
Top Bottom