Mfumo wa kuchagua comb kidato cha kwanza

sameer0220

Member
Joined
Nov 10, 2024
Posts
21
Reaction score
37
Nina ndugu yangu yuko kidato cha kwanza shule ya private ila leo karudi na barua toka shule kwamba kachuguliwa kusoma HKL kwa maana ya masomo ya ART na ni yuko kidato cha kwanza je huu ni mtaala mpya wa kulazimishwa kusoma combinations fulani bila mwanafunzi kuchagua?

Na hata bado hajafika Kidato cha tatu?
 
Inawezekanaje hili?
Em waja mkuje mtoe ufafanuzi, maana hata 4m 3 huchagui comb, ila unachagua masomo ya kusoma.

Hii ya kuchagua comb ni mpyaa kabisaa. Lol
 
Ni masomo ya kusoma amechaguliwa ART na sio sayansi anayoitaka
 
Kuna mikondo ya Sayansi,Sayansi ya jamaii, sports n.k (Mikondo ya Jumla)hapa ni wale wasio wa Amali.Huyo nduguyo kachaguliwa Sayansi ya Jamii. Wengine watakuja kuongezea.
 
Ahaa kwahiyo ni wanaanza toka form 1 kutosoma Physics, biology na Chemistry?
 
Ni masomo ya kusoma amechaguliwa ART na sio sayansi anayoitaka
Labda aseme ameambiwa asome Arts, kulingana na uwezo wake darasani, ila asiseme Comb tena HKL, em uliza shuleni kwake wakupe ufafanuzi zaidi.
 
Kuna mikondo ya Sayansi,Sayansi ya jamaii, sports n.k (Mikondo ya Jumla)hapa ni wale wasio wa Amali.Huyo nduguyo kachaguliwa Sayansi ya Jamii. Wengine watakuja kuongezea.
HKL ni sayansi ya jamii? Akati ni pure Arts.
Sayansi ya jamii, ni HGE, EGM, ECA, CBA,
pure sayansi, ni PCB, CBG, PCM, PGM, PMC
pure Arts, ni HKL, HGL, HGK
 
Iongeze HGL kwenye sayansi jamii.

Ila scenario aliyoileta mtoa mada nimekwisha ishuhudia mahali isipokuwa mwanafunzi atasoma Science ama Arts subjects ila "FULL BOOSTER" kwenye masomo yanayounda Combination
mfano Civics,Biology,HISTORY,GEOGRAPHY,KISWAHILI,Language,BA.Mathematics
 
HKL ni sayansi ya jamii? Akati ni pure Arts.
Sayansi ya jamii, ni HGE, EGM, ECA, CBA,
pure sayansi, ni PCB, CBG, PCM, PGM, PMC
pure Arts, ni HKL, HGL, HGK
Sayansi ya jamaii kwa mtaala mpya Kuna masomo sita ya Msingi yaani anasoma Geo, Business, Kiswahili, English,Historia ya Tanzania na Maadili na Basic Mathematics+History.Hapo yasizidi kumi,sasa mwanafunzi anaweza ongeza Labda Edk,divinity, Biology n.k.Hawa hawagusi kabisa Phys Wala Chem.Ila History ni lazima hapo kumbuka mikondo mingine kama Sayansi,Tehama, Sports n.k Hawa hawagusi History.
 
HKL ni sayansi ya jamii? Akati ni pure Arts.
Sayansi ya jamii, ni HGE, EGM, ECA, CBA,
pure sayansi, ni PCB, CBG, PCM, PGM, PMC
pure Arts, ni HKL, HGL, HGK
Mwanao akikuambia HKL ujue yupo Sayansi ya Jamii maana ndipo ilipo History.
 
HKL ni sayansi ya jamii? Akati ni pure Arts.
Sayansi ya jamii, ni HGE, EGM, ECA, CBA,
pure sayansi, ni PCB, CBG, PCM, PGM, PMC
pure Arts, ni HKL, HGL, HGK
Hapo nazungumzia mtoto wa Form one kwa mtaala mpya.Sio Advance.Kama mleta Mada alivyoshangaa.🙏🙏
 
Nina ndugu yangu yuko kidato cha kwanza shule ya private ila leo karudi na barua toka shule kwamba kachuguliwa kusoma HKL kwa maana ya masomo ya ART na ni yuko kidato cha kwanza je huu ni mtaala mpya wa kulazimishwa kusoma combinations fulani bila mwanafunzi kuchagua?

Na hata bado hajafika Kidato cha tatu?
Mtaala mpya unamtaka mtoto achague mwenyeww wap anataka kuelekea kutokana na ndoto zake huko mbeleni, hivyo basi amepewa nafasi ya kuchagua asome masomo ya sayansi au sanaa(masomo yasipungue 8 na yasizid 10), angalia nia ya mtoto au hata wewe unataka awe nani huko mbeleni halafu mchagulie cha kusoma kutokana na uelekeo wake
 
angalia nia ya mtoto au hata wewe unataka awe nani huko mbeleni halafu mchagulie cha kusoma kutokana na uelekeo wake
Siyo tu nia na uelekeo wa mtoto bali pia UWEZO wa mwanafunzi kumudu masomo mfano ya sayansi ni muhimu sana.

Mtoto anataka na wewe unataka awe na fani zenye sayansi, tatizo uwezo uwezo wake unaweza kua kikwazo
 
Back
Top Bottom