Mfumo wa Elimu utakuaje kama serikali itaongeza siku za likizo

Endapo hali itakuwa tata baada ya hizo siku 30 za matazamio hakuna namna mkuu, ratiba itakuwa adjusted. Likizo hii iliyotokea ghafla itafidiwa mwezi june (shule zisifungwe) ili kufidia kipindi hiki cha mpito.

Kwa madarasa yenye mitihani pia ratiba ya mitihani itabadilika....4m 6 badala ya kuhitimu mwezi May wahitimu mwezi July.

Wahitimu wa chuo pia ngoma isogee mwezi Nov.
Ili ratiba ya elimu ya 2019/2020 isiathiri ratiba ya 2020/2021.

Endapo mambo yatakuwa magumu zaidi katika kipindi cha makadirio kwa namna moja ama nyingine lazima ratiba ivurugike.
 
Kwa mtazamo wangu huu mwaka umeanza na nuksi kwa team ya LIVERPOOL isee wanachukuaje ubingwa wa EPL mwaka huu.

Kulingana na hili gonjwa la corona ambalo limekuwa kitendawili kwenye mataifa makubwa yenye uchumi mkubwa na maendeleo makubwa, ambayo yameshindwa kugundua dawa thabiti ya kuzuia huu ugonjwa moja kwa moja...ni dalili kuwa huu mwaka kwenye sector ya elimu lazima kutakuwa na mengi ya kushangaza sana.

Mfano form 6 mwezi ujao walitakiwa kuingia kwenye mtihani wa Taifa lakini mpaka dakika hii ni dhahiri kuwa hawatafanya mitihani kwa huo muda, lini itafanyika ni kitendawili na hata ikitokea watafanya mwezi 6 au 7 basi Yale mafunzo ya JKT kwa mwaka huu inabidi wayafute kwa kuwa wanafunzi wakianza mafunzo mwezi wa nane itabidi yaishe MWezi wa 11 na mwezi wa 10 kuna uchaguzi lakini pia mwezi wa 11 masomo kwa ngazi ya shahada ya kwanza yatatarajiwa kuanza.

Ukija kufuatilia zaidi kwenye sector ya elimu kwa hapa nchini itakuwa majanga sana cha msingi wanafunzi wajiandae kisaikolojia mapema kuwa kuna kusoma kwa mwendo wa 5G hapo mbeleni au kutakuwa na hati hati ya kurudia mwaka ila nawaza kwa wale wanafunzi wa chuoni ambao wanategemea pesa za mkopo itakuwaje na pesa umeshakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini pia sio sector ya elimu tu ndo itaathirika kuna makampuni ya kubeti sasa hivi wanahaha pamoja na sisi RAIA ambao tulikuwa tunategemea maisha ya kubeti kukidhi mahitaji madogo madogo....eee Mungu tunaomba utuepushe na hili janga...Amen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si Watapause tuu Mwaka huu wataendelea Mwakani
Mfano Mwaka huu Ulikua Form Five Mwakani unaendelea pale pale na form five yako Mpk chuo hvyo hvyo
Kama vile umepause mziki kwa Dk 5 Alaf baadae ukaendelea kusikiliza tena ulipoishia
 
vp kuhusu school fees?
Kuna wale waliolipa yote

Si Watapause tuu Mwaka huu wataendelea Mwakani
Mfano Mwaka huu Ulikua Form Five Mwakani unaendelea pale pale na form five yako Mpk chuo hvyo hvyo
Kama vile umepause mziki kwa Dk 5 Alaf baadae ukaendelea kusikiliza tena ulipoishia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endapo hali itakuwa tata baada ya hizo siku 30 za matazamio hakuna namna mkuu, ratiba itakuwa adjusted. Likizo hii iliyotokea ghafla itafidiwa mwezi june (shule zisifungwe) ili kufidia kipindi hiki cha mpito.

Kwa madarasa yenye mitihani pia ratiba ya mitihani itabadilika....4m 6 badala ya kuhitimu mwezi May wahitimu mwezi July.

Wahitimu wa chuo pia ngoma isogee mwezi Nov.
Ili ratiba ya elimu ya 2019/2020 isiathiri ratiba ya 2020/2021.

Endapo mambo yatakuwa magumu zaidi katika kipindi cha makadirio kwa namna moja ama nyingine lazima ratiba ivurugike.

Sasa what if hali itazidi kuwa mbaya hadi kufikia Julai, Septemba hadi Disemba huko ? Mfumo wa elimu si uta collapse ?
 
Si Watapause tuu Mwaka huu wataendelea Mwakani
Mfano Mwaka huu Ulikua Form Five Mwakani unaendelea pale pale na form five yako Mpk chuo hvyo hvyo
Kama vile umepause mziki kwa Dk 5 Alaf baadae ukaendelea kusikiliza tena ulipoishia

Kuna mdau hapo juu ameuliza kwamba je hiyo Corona ikidumu kwa miaka 10 au 15 je mfumo wa elimu utasimama kwa kipindi chote hicho ?
 
Ndio kwaanza hosteli za UDSM almaarufu Kama hosteli za Magufuli zimefanywa kuwa kituo cha kupokea wanaoingia na nchini kwaajili ya karantini.
 
Sasa what if hali itazidi kuwa mbaya hadi kufikia Julai, Septemba hadi Disemba huko ? Mfumo wa elimu si uta collapse ?
Kutakuwa hakuna namna mkuu, huu mwaka utakuwa ni mwaka wa mpito..Itakuwa ni changamoto kwenye mfumo mzima wa elimu.. Mungu asimame katika hili hali iwe shwari.
 
Ngoja tusikilizie maana hii hali imekuwa tishio, kama UDOM wametenga baadhi ya vyumba kwa ajili ya karantini,, pia UDSM tumesikia hivyo sasa hapo navuta picha itakuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ngumu kumeza mimi nachoona wangewarudisha tu wanafunzi maana kama hawajafanya prevention Juu ya mikusanyiko kama makanisa. Mskitin shulen sasa sijaona haja ya kuendelea kubakiza wanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa walilofanya ni kuwatoa wanafunzi waliokuwa boarding maana walikuwa hawana muingiliano na watu wa nje xaxa wako mitaani wakirudi shule mambo yatakuwa moto sana ila kama inawezekana kila shule iwe na quarantine yao ili kuepusha maambukizi kingine ni kuwapima wanafunzi kabla hawajarudi shule hamna namna wasiposoma wasomi wanapungua kuna wengine wanastaafu wengine wanakufa hamna shule ziendelee tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom