bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,565
- 2,966
Ndugu zangu tuzinduke kwenye huu usingizi mzito, tumeshalala kwa kipindi kirefu sana sasa ni muda sahihi wa kuvuta shuka na kutupilia mbali Fikra na Tamaduni zote zilizotokana na Wazungu. Tuanze mwanzo kila kitu kiwe chetu. Kitu cha kwanza kuking'oa kiwe mfumo wetu wa Utawala huu mfumo wa Democracy ni dhahiri hautufai hata kidogo.
Jambo linalofanya huu mfumo usikidhi ni kutokana na uwepo wa makabila tofauti ndani ya mipaka ya nchi za Africa tofauti na Ulaya ambapo hamna makabila. Kwa sababu hiyo viongozi ulaya wanachukulia raia wote kama ndugu zao Huku Africa hali inakuwa tofauti kwa sababu kiongozi kutoka kabila fulani haoni na hana hisia za umiliki wa pomoja wa mali ya umma. Ndio maana ataiba ili akajenge kwao kwa ndugu zake au avutie upande wake keki ya taifa. Hapa hakuna kulaumu mtu haya ni matokeo ya kanuni za kisayansi zinazohusu utawala na ukabila.
Eti tunakalisha makalio Secondary school tunafundishwa juu ya Democracy! ubatili mtupu, kwa nini tusijiongeze tukajifunza jinsi watalawa wetu wa kimila walivyoendesha jamii zao. embu vuta picha tawala za kijadi kama kina Mangi wangeachwa waendelee na tawala zao au Machief kwenye makabila mengine hivi ni kweli wangekubali kuona watu wao wakiteseka! vijana wao wakiranda randa kutafuta ajira! Ukitazama kwa undani Matatizo mengi yanayotukabili Africa hayana uhalisia hata kidogo na chimbuko lake ni kunakili mifumo ta watu kuja kuendesha nchi yako.
Eti wasomi wetu enzi hizo Warioba na wenzake wakaenda ufaransa na nchi nyingine Ulaya kujifunza na kunakili katiba ya nchi hizo kisha kuja kuchapisha kama katiba yetu hivi hata Utashi tu wa kawaida mtu huwezi kuona hili ni zuri hili ni baya.
nitaendeleea kesho...