Mfuko wa Jimbo kupingwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfuko wa Jimbo kupingwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Mar 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  Mfuko wa Jimbo kupingwa mahakamani


  Na Gladness Mboma

  MASHIRIKA sita yasiyo ya kiserikali yakiongozwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yanatarajia kufungua shauri la kikatiba mahakamani
  kupinga Sheria ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kwa madai kuwa inadhoofisha nguvu za wabunge kusimamia serikali.

  Sheria hiyo inadaiwa kwamba ikiendelea kutumika mbali na kudhoofisha nguvu ya wabunge inaendeleza ufisadi nchini.

  Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa Policy Forum, Bw. Israel Ilunde aliwaambia Waandishi wa Habari Dar es Salaan jana kuwa wanapeleka suala hilo mahakamani ili kuhoji uhalali wa kikatiba wa sheria hiyo ambayo ina athari ya kudhoofisha majukumu ya wabunge na kukinzana na dhana ya mgawanyo wa madaraka.

  Alisema kuwa mfuko wa jimbo unaweza kuonekana kama jambo zuri, lakini wamebaini kuwa utekelezaji na usimamizi wake utakuwa na kasoro nyingi na hasa nafasi wanayopewa wabunge kuwa wasimamizi wakuu wa mfuko huo.

  "Uamuzi wa bunge kutunga sheria ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo, Bunge lilikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na hasa ibara ya 63 na 64 ambazo zinabainisha kazi ya wabunge kuwa ni kusimamia na kuishauri serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.

  Alisema kuwa hali kadhalika sheria hiyo inakiuka ibara ya nne ya katiba ya nchi kuhusu mgawanyo wa madaraka.

  Bw. Ilunde alisema endapo wabunge watajiingiza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo wao wenyewe badala ya kuziachia serikali na halmashauri za wilaya watakuwa wamedhoofisha uhuru na nguvu yao ya kuohoji serikali kwenye masuala ya utekelezaji wa bajeti.

  "Wabunge kujiingiza katika kusimamia mfuko huo watakuwa wanakiuka mgawanyo wa madaraka, kwani kazi ya wabunge si kusimamia kutekeleza miradi ya maendeleo," alisema.

  Alisema kuwa kuna hatari ya mfuko huo kutumika kama takrima wakati wa kampeni za uchaguzi na hivyo kutotoa nafasi sawa kwa wagombea.

  Bw. Ilunde alisema kuwa mfuko wa maendeleo ya jimbo utachukua rasilimali fedha ambazo zingekwenda kuimarisha uwezo wa utendaji wa halmashauri hapa nchini.

  "Pamoja na kufungua shauri hili bado tunaishauri serikali iwawezeshe wabunge wetu kutekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha wana ofisi majimboni mwao ili wawe karibu zaidi na wananchi," alisema.

  Pia alishauri serikali kuboresha mfumo wa mawasiliano kati ya wabunge na wananchi majimboni ili kuwawezesha wabunge kupata taarifa sahihi za utekelezaji wa mipango ya serikali pamoja na kuwawakilisha wananchi.

  Bw. Ilunde alitoa wito kwa vyombo vinavyotoa haki kuangalia jambo hilo na itamke kuwa sheria ya mfuko wa maendeleo ya jimbo namba 16 ya 2009 ya mwaka 2009 ni batili kwa kuwa inapingana na katiba ya nchi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  Hii ni hoja nyeti sana...................mwingiliano kati ya Bunge na watendaji serikalini ni moja ya maeneo koleza ya ufisadi.................
   
 3. M

  Mtaalaamuna Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni ukweli usiopingika kuwa wabunge hutumia fedha hizi kama mali yao na kufanya wanavyo taka wao bila kuzingatia mahitaji halisi ya wapigakura wake. Pia inatoa mwanya kuwanyima wapigakura wa sehemu zile ambazo mbunge husika hakupata kura nyingi kuto fikiriwa kwenye miradi hio na kupendelea zaidi eneo analotoka mbunge husika.

  Nawapa hongera taasisi husika kwa kuona hilo. Big Up
   
 4. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Huu mfuko wa jimbo ni yale yale wanasiasa kutaka kujifanya watendaji. Wanasisa wetu wanajisahu sana na wanataka wawe mingu watu.
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi kuna wimbi wa wabunge (Moshi mjini, Arusha mjini, Monduli) kusafirisha wapiga kura wao kwenda kunywa dawa kule Loliondo, wanatumia fungu hili au zao za mfukoni?
   
 6. j

  joejou Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  kama wanashindwa kukabidhi hata samani za ofisi wanapomaliza kipindi chao, watalazimishwa na nani kuwasilisha mahesabu ya hizo hela zinavyotumika?
   
Loading...