Mfugaji

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Mfugaji amejiwa na mwaandishi wa magazeti ili kumuhoji kuhusiana na maisha ya shambani kwake.
Kwa bahati nzuri au mbaya Mfugaji hawapendi waandishi wa habari akaona bora amchoshe katika kujibu maswali...!
Na mambo yakawa hivi;


Mwandishi: Je ndugu wewe unawalisha ng'ombe wako chakula gani?

Mfugaji: Ng'ombe yupi unayemzungumzia...! Mweupe au Mwekundu?

Mwandishi: Ng'ombe mweupe!

Mfugaji: Ninamlisha nyasi na vigunzi vya mahindi.

Mwandishi: Na mwekundu?

Mfugaji: Mwekundi yupi

Mwandishi: Nina maana Ng'ombe wako mwekundu.

Mfugaji: vilevile nyasi na vigunzi vya mahindi.

Mwandishi: ahaa ok... sawa, Je unawalaza wapi?

Mfugaji: Ng'ombe yupi mweupe au mwekundu?

Mwandishi: Mweupeee!!!

Mfugaji: Mweupe ninamlaza bomani kulee..!

Mwandishi: Na mwekundu?

Mfugaji: vilevile ninamlaza na mwenziwe!!!!

Mwandishi: Hii sehemu ina majumba mengi, Na wakienda kulisha unafanyaje?

Mfugaji: Yupi mweupe au mwekundu?

Mwandishi: Woooteeee!!! ! (kwa hasira kidogo)

Mfugaji: Umekasirika!?

Mwandishi: La... Hapana sijakasirika! Naonekana nimekasirika?

Mfugaji: Naona umenitolea mimacho... kaa ng'ombe anazaa

Mwandishi: Aaah! Mzee utani huo...!

Mfugaji: Sitanii ni kweli!

Mwandishi: Tafadhali nifahamishe wakienda kulisha unafanyaje?

Mfugaji: Mweupe nina mfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha.

Mwandishi: na mwekundu vilevile?

Mfugaji: Mwekundu? Mwekundu ninamfunga kamba na kuzunguka nae kama mwenziwe!!!

Mwandishi: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe zako unaniuliza mweupe
au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa?

Mfugaji: Kwa sababu Ng'ombe mweupe ni wangu.

Mwandishi: Na mwekundu?

Mfugaji: Ni wangu vilevile!!

(Mwandishi presha juu)
 
Ha Ha Ha Ha Ha Ha Ha Ha ebwana hapo unajikuta unapayuka "aaaaaaggghhhh" afu unamalizia "pumbavu"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom