Mfaransa Afutiwa Kesi Ili Kuimarisha Uhusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfaransa Afutiwa Kesi Ili Kuimarisha Uhusiano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gamba la Nyoka, Apr 26, 2008.

 1. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  HABARI KWA HISANI YA ippmedia

  Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar


  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Bw. Pandu Ameir Kificho, amesema raia wa Ufaransa, Jeane Francois Leon (47), alifutiwa mashitaka ya utapeli ili kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa kati ya nchi yake na Tanzania.

  Spika alieleza hayo wakati akitoa ushahidi katika kesi ya utapeli iliyokuwa ikimkabili Mfaransa huyo pamoja na Watanzania watatu ambao wanatuhumiwa kumtapeli, Spika huyo pamoja na kaka yake, Bw. Hassan Ameir Kificho.

  Akiwa katika kizimba cha mahakama ya Mkoa Vuga, Spika Kificho alisema Balozi wa Ufaransa baada ya kukamatwa kwa raia huyo na kushitakiwa alimfuata ofisini kwake na kuomba waimalize kesi hiyo nje ya mahakama, kwa vile raia wake amekaa muda mrefu rumande na hana mtu wa kumuwekea dhamana.

  Katika kesi hiyo, Mfaransa huyo na Watanzania Halfan Suleiman Shaibu (47) mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Ezakiel Andrew Mwaitekele (40), mkazi wa Sinza na Robert Sospeter (44) mkazi wa Sinza walishitakiwa kwa kosa la kutapeli Sh. milioni 11. 8 na dola za Marekani 2,475, baada ya kumuuzia lulu bandia kaka yake Spika Kificho.

  Spika Kificho alisema kwamba kwa kuzingatia suala hilo bado lipo mahakamani alimshauri balozi huyo kufuata taratibu za kisheria kwa vile jambo hilo lipo nje ya uwezo wake.

  Hata hivyo, alisema baadaye alitaarifiwa juu ya kutakiwa kufika mahakamani na baada ya kufika upande wa mashitaka uliwasilisha ombi la raia huyo kufutiwa mashtaka ili kuimarisha uhusinao wa kimataifa kati ya pande mbili ombi hilo liliwasilishwa mahakamani na upande wa mashtaka Desemba 21, mwaka 2004.

  Alisema kwamba ni kweli alilipwa na mzungu huyo shilingi milioni tano na baada ya kukiri kutenda kosa na kufutiwa mashtaka yake.

  Malezo hayo ya Spika yalikuja baada ya Wakili anayewatetea washitakiwa wengine katika kesi hiyo, Bw. Hamid Bwezeleni kuhoji kwa nini mshitakiwa mmoja ameachiwa katika kesi hiyo, wakati wote walikuwa wakabiliwa na mashitaka ya jinai.

  Hata hivyo, hakimu wa mahakama ya mkoa anayesikiliza kesi hiyo, Bw. George Joseph Kazi, alisema Spika hapaswi kuulizwa sababu za kuachiwa kwa raia huyo wa Ufaransa na badala yake ziulizwe taasisi husika.

  Hakimu huyo alisema kwamba kulingana na kumbukumbu za mahakama upande wa mashitaka ukiongozwa na Salima Khamis uliwasilisha ombi la kumfutia mashtaka Mfaransa huyo ili kuimarisha ushirikiano mwema baina ya Ufaransa na Tanzania.

  Alieleza kwamba uamuzi huo hauendani na hali halisi ya matukio kwa vile wapo Watanzania wanahusishwa na makosa kama hayo ya jinai nje ya nchi lakini hawafutiwi mashitaka kienyeji.

  Awali kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu, Abraham Mwampashi na uamuzi wa kuachiwa Mfaransa huyo ulitolewa na Mrajis wa Mahakma Kuu Zanzibar, Bw. Essaya Kayange.

  Katika maelezo yake ya ushahidi Spika Kificho, alisema kwamba washtakiwa hao walifika nyumbani kwake wakiwa na nia ya kukodi nyumba ya kupanga kwa ajili ya ofisi, wakiwa wameambatana na raia huyo wa kigeni.

  Alisema kwamba baadaye aliwatembeza katika nyumba yake ya ghorofa tatu iliyopo katika eneo la Mpendae kwa lengo la kuwapangisha na waliridhishwa na nyumba hiyo na ndipo taratibu za malipo zikaanza kuandaliwa.

  Hata hivyo, alisema kwamba akiwa safarini kikazi mkoani Morogoro alipokea simu kutoka kwa Bw. Ezekiel Andrew, kumtaka wakutane Aprili 9, mwaka 2004 ili waweze kuingia mkataba wa ukodishaji nyumba na ununuzi wa madini ya lulu.

  Spika huyo alisema kwamba suala la kuingia katika biashara ya lulu hakufanya yeye, bali kaka yake aliyeingia katika biashara hiyo baada ya kuombwa na watuhumiwa hao waliokuwa wakimsaidia mzungu huyo kupata nyumba ya kukodi.

  Hakimu George Kazi ameiahirisha kesi hiyo ili kutoa nafasi kwa upande wa mashitaka ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka Muumin Khamis ili kuita mashahidi wengine wane katika kesi hiyo.

  SOURCE: Nipashe

  My take:
  Kwa nini wananchi wenzetu waliohusika na wizi uliomshirikisha mfaransa waendelee kusakamwa wakati mhusika mmojawapo(mfaransa) aachiwe huru. je sheria si ni msumeno?.
  kweli haki itatendeka hapo?
   
 2. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kuimarisha uhusiano na matapeli.........Afana leki kweli tuna kazi, yaani wakiona ngozi nyeupe basi mkojo kwenye chupi.
   
 3. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Wa kumuuliza ni huyo aliyekubali Sh Milion 5.
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Acheni ujinga nyie
  Ngozi nyeupe zinawazuzua sana, sijui mna matatizo gani? ni watanzania wangapi wanakamatwa huko ufaransa na nchi zingine? Je kesi zinafutwa ili kuimalisha uhusianao??
  na kama hata raia wa nchi husika ana makosa, basi mtamuachia tu kwa vile mnataka kupewa vijimisaada sio?

  Hiyo sio akili bali ni matope
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,744
  Likes Received: 82,685
  Trophy Points: 280
  Sheria zetu za bongo hizo!!. Mzungu anaachiwa kwa sababu ya ngozi yake lakini walioshirikiana naye katika utapeli watapata kibano.
   
 6. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu wazawa nao wamestrike deal au ndio hivyo tena mkono mtupu haulambwi?
   
 7. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kibaya zaidi hata wadhungu wameshajua kuwa tukiona ngozi nyeupe tunatetemeka.
   
 8. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wazungu wengi wanaokuja hapa Tanzania wana kazi mbili tofauti. Kwa hiyo inawezekana kazi yake ilikua ni ya Kijasusi. Ili kupata taarifa anazozihitaji ilibidi ajiingize kwenye biashara haramu kama hizo. Maana haiingi akilini Balozi kuingilia kesi kama hiyo na hata kukiri wazi inaweza kuharibu mahusiano na Ufaransa
   
 9. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ndani ya maneno mna maneno manene
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  .


  [​IMG]
   
Loading...