Mfanyakazi wa bunge auwawa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyakazi wa bunge auwawa!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Adharusi, Jan 23, 2012.

 1. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,630
  Likes Received: 3,014
  Trophy Points: 280
  Chanzo gazet la mwananchi
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sasa wewe mwenzetu umesoma si ungetudadavulia japo jina tu sie ambao tunasubiri mpaka Bosi amalize kuyasoma!?
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Heading na chanzo tu! Kwanini usingeenda in detail kidogo kwa faida ya wengi...maswali ya nani kauawa na nani na kwasababu gani auawe yataumiza watu vichwa kabla ya kupata gazeti hilo!
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ata-edit mwali. Alikuwa anawahi kuileta, subiri kidogo. Mzima wewe?
   
 5. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  la lini?
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  gazeti la mwananch ndo lililoanzisha thread hapa jf?
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kukurupuka kwingine hakufai. usiaanzishe mada ukitegemea wanajamvi ndo wakupe full detail. umesikia magazetini, wengine wamesikia wengine bado. ni bora usubiri, ulipate gazeti husika ndo uje hapa sio kuwapa watu nusu nusu.

  Lakini sio kosa lako, ni ugeni jamvini hivyo bado hujajua nini ni nini.

  Join Date : 22nd January 2012
  Posts : 7
  Rep Power : 30
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  could you provide more details? Naona kama umeacha vitu vingi viko hewani hewani
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anataka mkalinunue, mkishajua kilichotokea in details, ni nani atanunua Gazeti hilo.................Hebu acheni ubahili....Ebo!
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Hawa Mwananchi walisema Dr Slaa hasalimianai na JK

  [​IMG]
   
 11. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Waandishi Wetu

  WAKATI Bunge likiendelea kuomboleza vifo vya wabunge wake wawili, Regia Mtema (Viti Maalumu Chadema) na Jeremiah Sumari Arumeru Mashariki CCM), limepata pigo jingine baada ya mfanyakazi wake, Nicolaus Luther Senge kufariki dunia kwa kupigwa risasi na askari polisi katika tukio ambalo lilisababisha vifo vya watu watatu.Hata hivyo, kumekuwa na taarifa za kutatanisha na zenye kupingana kati ya polisi na Bunge kuhusu jina halisi la mfanyakazi huyo na mahali ambako mwili wake umehifadhiwa.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Senge (49) alifariki dunia usiku wa kuamkia jana katika mauaji yaliyofanyika kwenye kikao cha wanafamilia Kibaha mkoani Pwani.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu amethibitisha kifo hicho lakini akamtaja mtumishi huyo wa Bunge kuwa ni Nkolo Senge.
  Kamanda Mangu alisema katika tukio hilo lililotokea nyumbani kwa Pendael Senge ambaye ni Mratibu wa Tasaf Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, wengine waliofariki dunia ni Andrew Nkolo (30) na askari polisi Nicodemus Senge ambaye ndiye anayetuhumiwa kuwaua wenzake.

  Alisema siku ya tukio, watu hao walifika nyumbani kwa Pendael ambaye ni baba yao mdogo kwa ajili ya kupatanishwa juu ya ugomvi wa urithi wa ekari mbili za ardhi zilizoko kijijini kwao Singida.

  "Ugomvi huo ulianzia Singida ambako walishtakiana lakini hakimu akawataka waumalize kiukoo. Ndipo Pendaheli ambaye ni baba yao mdogo akaamua kuwaita nyumbani kwake ili wazungumzie suala hilo," alisema Kamanda Mangu na kuendelea:

  "Wakiwa kweye kikao hicho kabla ya kufikia mwafaka, Nicodemus ambaye ni askari polisi wa Kituo cha Usalama Magomeni, Dar es Salaam alichomoa bastola yake na kuwamiminia risasi ndugu zake hao kisha kujimaliza mwenyewe."

  Kwa mujibu wa Kamanda Mangu, miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha na hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

  Kauli ya Ofisi ya Bunge

  Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amethibitisha kutokea kwa kifo cha mfanyakazi huyo wa Bunge na kueleza kuwa hadi jana mchana, lakini akasema maiti yake ilikuwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Ndugai alisema Ofisi ya Bunge imesikitishwa na kifo hicho kilichotokea usiku wa kuamkia jana, siku chache baada ya taasisi hiyo ya kutunga sheria kupoteza wabunge wawili.

  "Kwa sasa nipo Arusha lakini taarifa za kifo cha Senge nilizipata jana. Bado sina taarifa zaidi kuhusu kifo hicho kwa sababu kimetokea kwa njia ambayo lazima ihusishe uchunguzi wa kipolisi," alisema Ndugai.

  Hilo ni pigo jingine kwa taasisi hiyo katika kipindi cha juma moja baada ya Mtema kufariki dunia Januari 14, kwa ajali ya gari iliyotokea Ruvu, Kibaha na Sumari alifariki dunia Januari 17, mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mrefu saratani ya ubongo.

  Kauli ya familia


  Baba mdogo wa marehemu hao Pendael Senge naye alithibitisha mauaji hayo na kueleza kuwa yalitokana na ugomvi wa shamba.
  Pendael alisema askari huyo aliwaua ndugu yake Nicolaus Senge ambaye alikuwa mtumishi wa Ofisi ya Bunge, pamoja na binamu yake Andrew Nkolo (mtoto wa shangazi yake).

  Akisimulia tukio hilo Pendael alisema kabla ya mauaji hayo, ndugu hao walifika nyumbani kwake Kongowe Kibaha kwa ajili ya kikao cha usuluhishi kuhusiana na ugomvi huo wa shamba. Hata hivyo, alisema usuluhishi huo ulishindikana na badala yake ukazuka ugomvi baina ya ndugu hao uliwafanya wapigane ngumi kabla ya wanandugu kuwaamulia.

  Alisema muda mfupi baada ya ndugu kuwaamulia, askari huyo aliwapiga risasi ndugu zake kisha naye kujimaliza.
  Alisema chanzo cha ugomvi huo ni shamba la ekari mbili lililoko katika Kijiji cha Ilunda Wilaya ya Iramba, Singida... "Shamba hilo ni la mpwa wangu
  Andrew ambalo alirithishwa na mama yake aliyefariki dunia takriban miaka 15 iliyopita," alisema Pendael na kuongeza:

  "Lakini kwa kuwa Andrew anafanya shughuli zake za Steshenari Dar es Salaam, basi binamu yake Nicodemus Senge akajenga nyumba katika kiwanja hicho."

  Alisema baada ya Nicodemus kujenga katika kiwanja cha Andrew, walishtakiana katika baraza la ardhi kijijini hapo ambalo liliwaagiza wazungumze wenyewe kwanza ili kuona kama wanaweza kufikia mwafaka.

  "Kwa kuwa wote wako hapa Dar es Salaam ndipo jana wakaamua kuja kwangu kwa ajili ya kufanya kikao cha usuluhishi. Wao walifika saa 10 na baada ya ndugu wengine kufika saa 12 jioni ndipo tukaanza mazungumzo:

  "Niliwasihi kuwa nikiwa baba yao mdogo ningefurahi kuona jambo hilo linamalizika kindugu," alisema Pendaeli
  Hata hivyo, alisema wakati wa mazungumzo hayo Nicodemus akamshutumu ndugu yake Nicodemus (wa Bunge) kuwa ndiye anayempa msaada binamu yake wa kifedha na kiushauri.

  "Alikuja juu (polisi) na kuongea kwa hasira sana. Mimi baada ya kuona kuwa hakuna uelewano tena nilishauri kuwa ni vyema tuliachie baraza la ardhi liamue," alisema Pendaeli na kuongeza:

  "Nico wa Bunge na Andrew walikuwa upande mmoja na huyu askari na baadhi ya ndugu wengine walikuwa pia upande mmoja, hivyo wakaanza kupigana ngumi lakini watu wakawasihi wakaacha."

  "Lakini kabla ya kuondoka huyu askari akaomba maji, walipomletea akakataa glasi akanywea kwenye kidumu kile cha lita tano. Alipokunywa mara
  moja tu akapiga chini lile dumu kisha akakimbia hadi kwenye gari alimokuwa Nico wa Bunge akampiga risasi moja ya usoni kisha akamfuata Andrew akampiga risasi ya begani, wakati akikimbia akampiga risasi nyingine kiunoni, akaanguka na kufariki dunia," alisema Pendaeli.

  Baada ya matukio alisema watu wote walikimbia akiwamo askari huyo ambaye hata hivyo, alisema alikimbia kama mita 50 kutoka nyumbani hapo kisha naye akajipiga risasi kifuani na kufariki dunia papohapo.

  "Nilikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na askari walipofika na kumpekua mfukoni mwake (muuaji) wakakuta kikaratasi kilichosema: mtu yeyote asisumbuliwe kwa mauaji haya," alisema Pen
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hahahahah mwali we nlikuwa na haraka na mie ah! haya ntasubiri ila ndo dah kanikosesha umbea wa kupiga kwenye daladala sasa!

  Mie mzima shosti niko kule nakusaidia kumwombea kaka msamaha kwa Kabakabana.
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwani Ye ni wakala wa magazeti Baba?
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Uchizi! Ekari mbili za ardhi Singida au Masaki? Smile miwani yangu ina giza, msaada.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Nashauri sinema za Kinaijeria zipigwe marufuku......
   
 16. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ahahaaa kingast bwana mi sitaki ushaidi nadhani masaki angeua ukoo mzima
   
 17. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi nilifikiri hasira ni kwa wahehe tu, hata singida du
   
 18. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  ni shamba tu?au lina madini ya uranium?
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  ukoo tu? ama angetumia weapons of mass destruction hadi sie wa bunju tukome! ningekuwa mkewe huyo, adhabu yake kwanza hicho kinyumba alichojenga nampa mke wa mhanga buree, na pensheni yake naolea serengeti boy huku nikichekecha akili how did i end up with such a fool coward man! kha!
   
 20. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  mshahara wa polisi, ndo chanzo cha mauaji hayo. Utakuta shamba lenyewe hata rutuba halina, na mtu ukijipanga ukiwa na milioni, unapata zaidi ya hilo. Askari polisi na kamshahara kake kadogo, angekopa hata ura, kisha akanunua ardhi ya kutosha ili kumaliza ugomvi.
   
Loading...