Mfanyabiashara wa madini ya dhahabu Mwanza akamatwa kwa tuhuma za kuwajeruhi watu wawili kwa risasi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli

Mfanyabiashara wa madini ya dhahabu jijini Mwanza, Salum Othuman (44) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa tuhuma za kuwajeruhi watu wawili, akiwemo mpenzi wake Happiness Israel (32).

Anadaiwa kumpiga risasi ya mguuni mpenzi wake baada ya kutokea ugomvi wakati wakiwa chumbani kwenye hoteli ya Kilimanjaro mjini Geita.

Leo Alhamisi Februari 27, 2020 Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea jana Februari 26, 2020.

Amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya tukio hilo, alimbeba Happiness aliyekuwa akichuruzika damu kwa lengo la kutoroka lakini meneja wa hoteli hiyo, John Maftar(43) alimuona na alipomtaka asiondoke alitishia kumpiga risasi.

Mwabulambo amesema baada ya meneja kusogea pembeni mtuhumiwa aliingia kwenye gari lake na kumgonga, kisha kugonga geti na kuondoka eneo hilo.

Amebainisha kuwa polisi walimkamata na Happiness alipewa huduma ya kwanza na kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Bugando baada ya kubainika mfupa wake wa paja umepasuka.

Amesema Maftar amepata majeraha maeneo mbalimbali mwilini, anaendelea na matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Geita.

Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Paulo Lyimo amesema mtuhumiwa ni mteja wao wa mara kwa mara.

Amesema siku hiyo asubuhi akiwa na mpenzi wake chumbani, wahudumu wa hoteli walisikia mlio wa risasi na baadaye alitoka chumbani akiwa amembeba Happiness.

“Wahudumu hao walisema alimuweka kwenye gari na alipozuiwa asiondoke alimtishia meneja kwa bastola na alipojihami, mtuhumiwa aligonga geti na kumburuza meneja kisha kukimbia hadi pale alipokamatwa kwa msaada wa polisi na madereva bodaboda waliokuwa wakifukuzia gari yake .
 
MH AFANDE SIRRO
HUYU JAMAA ANATESA WATU SANA MWZ.GEITA.MARA HASA ANAPOKUWA NA KUNDI ZA WATU

KWA HILO LA MABINTI INAWEZAKUWA AMEMNYIMA SEHEMU ISIOTAKIWA AKAONA AMPASUE NA BASTOLA

AMekuwa akijiamini SNA na bastola YAKE SEHEMU ambazo hata azitakiwi kuongelea ama kuzungumzia silaha

Najuaa baddhi ya Ma rafiki zake n wakuu wa POLISI mwz..tunaombaa kwa hilii Baba Sirro wamweke wamweke NDANI na silaha anyanganywe afungwee I we fundishoooo kwa jamiii

Mwz kunaa wapuuzi wengii sanaa hasaa wakilewa wamekuwa wakijitapa na kuweka hata bastola.mezani hukuu wanakunywa pombe

Wana umbumbu sana wa silahaa igeni WACHAGA ama watu wa madini arushaa
 
Jamaa sijuwi kavurugwa nini na Happiness?Sema kwa msala huo inabidi akanyee debe sana lupango.
 
MH AFANDE SIRRO
HUYU JAMAA ANATESA WATU SANA MWZ.GEITA.MARA HASA ANAPOKUWA NA KUNDI ZA WATU

KWA HILO LA MABINTI INAWEZAKUWA AMEMNYIMA SEHEMU ISIOTAKIWA AKAONA AMPASUE NA BASTOLA

AMekuwa akijiamini SNA na bastola YAKE SEHEMU ambazo hata azitakiwi kuongelea ama kuzungumzia silaha

Najuaa baddhi ya Ma rafiki zake n wakuu wa POLISI mwz..tunaombaa kwa hilii Baba Sirro wamweke wamweke NDANI na silaha anyanganywe afungwee I we fundishoooo kwa jamiii

Mwz kunaa wapuuzi wengii sanaa hasaa wakilewa wamekuwa wakijitapa na kuweka hata bastola.mezani hukuu wanakunywa pombe

Wana umbumbu sana wa silahaa igeni WACHAGA ama watu wa madini arushaa
Wawe wanawaua kama msuya alivyouwa ama unamaanishaje
 
Operesheni tokomeza itakua ilikusahau,hiki sio kiswahili cha mtanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom