Mfanyabiashara ashusha tuhuma nzito kwa RTO Arusha

Mfanyabiashara ashusha tuhuma nzito kwa RTO Arusha

Ukweli ni kwamba Jeshi la Polisi na TRA baeo ni vinara wa rushwa. Nitaamini kuwa PCCB inafanya kazi siku nitakapoona inashughulika na Polisi na TRA. Mpaka sasa sijaona jitihada zozote za PCCB dhidi ya taasisi hizi mbili vinara wa rushwa.

Mkuu kwa utafiti wangu mdogo (na usio rasmi) nilioufanya.. Nimebaini kuwa wanaoongoza kwa rushwa nchi hii ni Ikulu, PCCB, CCM, TRA, Polisi, JWTZ, TPA, wakifuatiwa na wananchi wenyewe.
Kwa anayetaka kuhoji zaidi asubiri nitaanzisha uzi wa kuweka vielelezo vyote bayana..
Kwa hiyo hitimisho langu ni kuwa rushwa haitakaa iishe..
Muhimu ni mtu mmoja mmoja kupambania haki yake!
 
Siyo traffic tu, central police Arusha inanuka Rushwa

Mkuu pale si tu pananuka Rushwa...
Hata ramani, michoro, muundo na rangi za yale majengo ni tafsiri mujarabu ya neno RUSHWA..
Tukirudi kwa Police Traffic... yaani hawa imefikia hatua mbaya sana..
Kwa sasa wanacheza kibati na madereva.. kwa siku kuanzia elfu 2 kwa kila gari!
 
Hi huwa najiuliza kwanini PCCB hawawakamati traffic police na wanasikia malalamiko ya wananchi kila siku, lakini pia mamlaka zinazohusika kwanini zinashindwa kuweka maeneo maalumu ya ukaguzi wa magari na maeneo hayo kufungwe CCTV cameras for transparency reasons?

Mimi naona tunatumia gharama kubwa kujifanya tynadhibiti hili mara lile wakati mambo hayo yangeweza kufanywa kisayansi zaidi ili kupunguza gharama za kuajiri wala rushwa
Hawapendi hivyo vifaa viwekwe kwa sababu wanadhibiti kinafki.
 
Mtu akiniambia eti sasa hivi rushwa imedhibitiwa huwa namuona hajui asemalo. Kwa sasa rushwa imeshika kasi, bali kinachofanyika ni kutoripotiwa na vyombo vya habari ili serikali ipakwe mafuta kwa mfano mgongo wa chupa kwamba inafanya kazi. Ukweli ni kuwa rushwa iko palepale bali haitangazwi. Ushahidi wa rushwa kwamba bado ipo sana, ni ile majuzi wafanyabishara walipokutana na rais na kuamua kufunguka. 90% walionyesha kwamba rushwa ipo. Namuunga mkono huyo Mberesero kwani kasema ukweli.
Labda amedhibiti rushwa kwa walimu wa msingi kutochukua pesa ya tuition kwa wanafunzi ila kwa vitengo vingine iko pale pale.
 
Mfanyabiashara na Mmiliki wa Mabasi ya kusafirisha abiria mikoani kutoka kampuni ya KIMOTCO ,Benedict Mberesero,amewalalamikia askari wa usalama barabarani katika Jiji la Arusha,kwa vitendo vya Rushwa iliyokithiri akidai wamegeuka mamlaka ya mapato TRA.

Akiongea katika kikao cha wadau wa usafirishaji jijini Arusha,mbele ya Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Nchini,(SACP)Futunatus Musilimu, alimshutumu Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha ,RTO Joseph Bukombe kuwa amekuwa kinara kwa kuongoza kikosi cha askari kukusanya Rushwa kutoka kwa wasafirishaji .

Amedai kuwa vibanda vya ukaguzi wa mabasi katika eneo la kituo kikuu cha mabasi jijini hapa ,vimegeuka vibanda vya kukusanya Rushwa kwa mabasi mbalimbali yanayoelekea mikoani na fedha hizo huwasilishwa kwa wakubwa .

"Napenda niseme ya Moyoni naona watu wamekuwa waoga kusema ,ukweli ni kwamba suala la Rushwa ni kubwa kwa Trafiki hapa Arusha naomba uchunguze mwenyewe ujionee" Alisema Ben

Aliongeza kuwa hivi karibuni alibambikiwa kesi ya matumizi mabaya ya Silaha ambapo alipigwa na askari wa usalama barabarani na kutupwa selo kituo cha Polisi kwa makosa aliyodai ni ya usalama barabarani.

"Namshukuru RPC alilishughulikia suala langu na bila yeye bila shaka ningekuwa nimefungwa kwa kubambikiwa kesi za uongo kwani si kweli kwamba Mimi nilitishia askari kwa silaha" Alisema .

Alimtuhumu RTO Bukombe kutoa ushirikiano pindi anapopigiwa Simu kwa nia ya kuomba msaada.

Akijibu hoja hizo ,RTO Bukombe Alisema tuhuma zilizoelekezwa kwake hazina ukweli Bali ni chiki zilizolenga kumchafua.

Alisema mabasi ya Kimotco yanaongoza kwa kuvunja sheria za usalama barabarani na pindi anapochukua hatua inaonekana kwamba RTO Bukombe mbaya na kuanza kumchafua kwa kusema askari anawatuma kukusanya Rushwa.

Ends.....View attachment 1145584
"...nao askari wakauliza, nasisi je tufanye nini? Yohana akawajibu; msimdhulumu mtu, wala msimshitaki mtu kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu...."

Bukombe hata ujitetee vipi, askari kujitenga na yale Yohana aliwashauri mfanye ama msifanye ni vigumu. Aliyo yasema Mberesero tunayashuhudia kila mahala.
 
Saa mbovu leo imepatia majira!!
 
Tangu awali matraffic wa Arusha ni walaku sana, huyu rto wasasa amewanyoosha matajiri wengi sijui kama watambakiza
Yaani kama mke wangu haedeshi tena gari hapa Arusha
 
Hiyo ndo tofauti ya akili na mihemuko. Weweni aina ya watu wale ambao hudhani; upepo ukivuma uelekeo wao basi ndo kuna upepo.

Kama wewe ndio mfano wa wenye akili, acha niendelee kuwa mjinga.
 
Rushwa ina njia mbili, aidha UNALAZIMISHWA utoe rushwa ili uachiwe kwa sababu unamakosa au unataka mambo yako yaende haraka au UMELAZIMISHWA utoe rushwa kwasababu umebabikiwa makosa au pia wanakukwamisha ili utoe rushwa.
Sasa wenye mabasi ya magari tuseme hawataki kutoa rushwa basi wahakikishe hawana makosa kwenye magari yao na Kama yanamakisa wkubali kutoa faini tu na sio zaidi. Na wenye mabasi wakizungushwa na kukwamishwa basi inabidi wafanye mgomo wa angalau siku mmoja tu. Na wenye mabasi wote waungane, ikitokea kwamba wamelazimishwa kutoa rushwa au wanazungushwa na kucheleweshwa hadi watoe rushwa basi hapo wafanye mawsiliano na wagome. Hilo suala nina uhakika litashughulikiwa mara mmoja. Na wakivabikiwa makosa wajitahidi kushibitisha kwamba hawana makosa, siku hizi kuna njia kibao ya kumnasa mtu. Si lazima umchukue video unaweza ukarekodi kwenye simu yako pia.
Tuwe wakweli jamani...ma Bus ya KIMOTCO yapo kwenye hali ya ki Mortuary zaidi kwani hata huyo Afande Musilimu akichukua askari kutoka Somalia na kukagua.gari yoyote ya KIMOTCO ataikuta na karai la matatizo, huyo tajiri nafikiri ni wale waliozoea kupiga na kuona hakuna taabu yaani"Bussiness as usual"
 
Mkuu kwa utafiti wangu mdogo (na usio rasmi) nilioufanya.. Nimebaini kuwa wanaoongoza kwa rushwa nchi hii ni Ikulu, PCCB, CCM, TRA, Polisi, JWTZ wakifuatiwa na wananchi wenyewe.
Kwa anayetaka kuhoji zaidi asubiri nitaanzisha uzi wa kuweka vielelezo vyote bayana..
Kwa hiyo hitimilisho langu ni kuwa rushwa haitakaa iishe..
Muhimu ni mtu mmoja mmoja kupambania haki yake!

Absolutely right.
 
Hi huwa najiuliza kwanini PCCB hawawakamati traffic police na wanasikia malalamiko ya wananchi kila siku, lakini pia mamlaka zinazohusika kwanini zinashindwa kuweka maeneo maalumu ya ukaguzi wa magari na maeneo hayo kufungwe CCTV cameras for transparency reasons?

Mimi naona tunatumia gharama kubwa kujifanya tynadhibiti hili mara lile wakati mambo hayo yangeweza kufanywa kisayansi zaidi ili kupunguza gharama za kuajiri wala rushwa
Tatizo kila anaepangwa kazi Arusha anaambiwa usipo tajirika autakaa utajirike kwa maana hiyo hakuna cha Takukuru,Polisi,Tra,Hospital wala custom au immigration
 
Tuwe wakweli jamani...ma Bus ya KIMOTCO yapo kwenye hali ya ki Mortuary zaidi kwani hata huyo Afande Musilimu akichukua askari kutoka Somalia na kukagua.gari yoyote ya KIMOTCO ataikuta na karai la matatizo, huyo tajiri nafikiri ni wale waliozoea kupiga na kuona hakuna taabu yaani"Bussiness as usual"
Mabasi ya Kimotco unayo zungumzia wewe ni yale ya zamani ya kwenda Simanjiro. Hivi sasa wana mabasi mazuri Classic yenye mpaka Wifi
 
Labda amedhibiti rushwa kwa walimu wa msingi kutochukua pesa ya tuition kwa wanafunzi ila kwa vitengo vingine iko pale pale.
Kwani hiyo ni rushwa?Hiyo ni extra duty allowance inayolipwa na mzazi kwa mwalimu anayemfundisha mtoto wake,japo imekatazwa.
 
Nakubaliana na wewe kabisa.
Pia ile kozi inayoendeshwa pale polisi mess, unalipa
1.10,000 kiingilio na kitabu na alama za barabarani
2.85,000 cheti
3. 3,500 kiti ulichokalia

Inasikitisha sana
Jeshi la kukusanya rushwa Tanzania
 
Mabasi ya Kimotco unayo zungumzia wewe ni yale ya zamani ya kwenda Simanjiro. Hivi sasa wana mabasi mazuri Classic yenye mpaka Wifi
Alaah? Mie nilikuwa nazungumzia yale ya Mwanza - Arusha yanayoshindana na mghambas kuelekeza watu kibra
 
Kwa maeneo mengi ya nchi yetu bora umiliki shamba la bangi - kumiliki gari kila siku pressure iko juu
 
Itakua rto amewawawekea targets kubwa.
Kama Muslim haamua kumlinda huyu RTO naungana na Ben.. Trafiki Arusha ni tatizo kubwa. Na hii inachangiwa na wingi wao barabarani. Yaani kutoka kwa Morombo kwa mfano, hadi ufike posta mpya kuna vituo vya askari wa usalama barabarani zaidi ya saba. Unajiuliza hivi kuna umuhimu gani wa vituo vyote hivyo? Zaidi ya usumbufu.. Na kuongeza foleni. Kwa rushwa niseme kwa Tanzania nzima Trafic Arusha wanaongoza. Huwezi kusimamishwa hata kama huna kosa usiwaachie polisi chochote. Inahitajika mageuzi makubwa sana trafiki Arusha. Nazunguka maeneo mengi Tanzania lakini Arusha ni kiboko kwa rushwa na usumbufu usio na maana. rto asiseme kuna chuki.
 
Back
Top Bottom